which is the best university in tz?

i think this question goes beyond its intent. kwa uchangiaji, utaona vijana wa vyuo vyetu wanavyohaibisha vyuo na labda muuliza swali atajua ni chuo gani aende. chukua waliochangia kwa kila chuo kimtazamo na kihoja, hapo utajua ni chuo gani kilichobest Tanzania. sio kwa grade za mitandaoni, wala majengo wala uwingi bali uelewa wa hao wachangiaji utakupa jibu. pole mdogo wangu. wengine wanachangia utadhani hawakuelewa thread, na hivyo kureflect chuo kinavyowaandaa..
 
Udsm ndiyo sehemu sahihi kwako kama point zako zitakuruhusu, hivyo vingine ni si-hasa tu.
 
hiyo dit na vingine ulivyovitaja vinatoa ajira moja kwa moja au bado ni husteling ya mtu!anyway sijasikia MUCCOBS cha moshi!pia kama ninahitaji chuo chenye wapendwa na ibada ni kp?

dogo usidanganyike kirahisi hivyo, hakuna chuo utachosoma umalize ufatwe na makampuni eti kuja kukuomba uwafanyie kazi, hali ya ajira Tanzania sio nzuri kama zamani kwahiyo la ajira we jiandae kukomaa.

Kuhusu la vyuo vya wapendwa kinadharia vipo lakini kiutendaji HAKUNA, we jichunge kimpango wako ila hakuna msaada wa mazingira utakao upata utakao kuweka mbali na maovu utakapo ingia chuo ukilinganisha na mashule ya kidini ya huko chini.
 
kwa aliyesoma masomo ya ECA the best university in SAUT, maana walianza kufundisha mambo hayo tangia zamani wakiwa NTC, nenda hata Bodi ya Uhasibu watakueleza akina nani wanafaulu mitihani ya bodi yao baada ya kumaliza university. Kama ukikosa SAUT nenda Mzumbe ndo wa pili katika utaalamu huo wa uhasibu. SUA, UDSM, UDOM etc wote katika hilo si wa kwanza. Kama wataka kubadili fani na kuingia uhandisi wa aina yoyote, basi UDSM, Kilimo jaribu SUA ila nahisi ni wazuri kwa 'nutrition' zaidi kuliko mifugo na kilimo kwa ujumla. Vinginevyo kujiunga na vyuo waweza kuomba pia ushauri TCU.

Mbona hujamueleza kuhusu maksi atakazopata. Kama kaangukia pua namshauri aje SAUT maana hata four hapo anajiweka tu na elimu atapata. Lakin kama atapata div one basi aende bcom udsm au agri economix pale Sua.

Aksante
 
Kulingana na ranking za Tanzania udsm ndo the best universirty,ila kulingana na combination yako ya ECA naona unapendelea masomo ya biashara,kwa hivyo nakushauri ukasome Mzumbe BAF,sema uwe na uhakika wa kupata div 1 point 3 had 6,kwa hilo halina ubishi ktk uhasibu mzumbe is the best university na ndiyo maana katika mitihani ya ACCA chuo klichopunguziwa mitihani ni Mzumbe tu.,au nenda UDSM au UDOM ingawaje wengi wanakidharau bt lecturer wengi wa pale hasa department ya accounting,business administration ni graduates wa Mzumbe na Udsm

acha uongo bwana kuhusu BAF yenu hiyo. kuna waliofeli wakashindikana na bado wanasoma hapo. Kuhusu elimu ya uhasibu kweli mko vizuri lakini sio cutoff points. umedanganya
 
aah aah kama anataka university.....

Mkuu, ukitaka masomo ya uhandisi nenda udsm au st joseph college of engineering. Ila kama ni masomo ya biashara nakushauri nenda Mzumbe, sheria nenda Tumaini University Iringa, mass communication nenda SAUT-Mwanza. Udsm kilikuwa bora lakini miaka ya karibuni kinalega lega mfano Wanafunzi wa sheria wa udsm siku hizi wanafeli sana law school na sokoni wachovu sana. Kwa maoni yangu muuliza swali ukitaka sheria usiende udsm.
 
kama unapenda kusoma chuo huku unajifunza dini ya kiislamu---morogoro muslim university and zanzibar muslim universty
kama unapenda kusoma chuo huku unafunza dini ya kikristo--st.john,kcmc,sauti,
kama unapenda kusoma chuo huku ukitaka kujifunza tamaduni za kichagga--muccobs
kama unapenda kusoma chuo lakini una malengo ya kuajiriwa vijijini na kuwa karibu na wakulima----sua
 
by mr speed
UDSM TU VYUO VYINGINE NI VYA KATA .UNAMAINDI KUSOMA YEBOYEBO? NENDA
Nenda Mwenge na posta jioni uone wenzako wa UDSM wanavyozunguka na bahasha na kubaki kusema wana elimu bora.Usimpoteze mwenzako kwa tambo na majigambo yasiyo na msingi wowote. Mpe ushauri kwanini UDSM unaona ni bora ili afanye uamuzi sahihi.

Kwa vyuo tulivyosoma wengine (havipo Tanzania) tukifika UDSM tunashaangaa mnachokisifia, na tukiwaona madr na lecturers wa UDSM(baadhi) wasivyo kuwa wanaandika 'journal, artilces na books' na kufanya tafiti zenye tija tunajihoji kama tupo serious na elimu ya juu. Pia ukienda UDSM library utashaangaa haina vitabu bora, vilivyopo ni vya zamani, ukienda vyuo vikubwa ukiona library za wenzetu utajihoji kama UDSM wanasoma au wanaenda kushinda kwenye majengo? Angalia majengo yalivyo mabovu na mabweni pia, wakufunzi wanadhani ukibania marks wanafunzi ndio sifa; huko ni kuwaharibu wanafunzi, chuo kila siku kuna migomo. Nikuulize ni lini siku za karibuni UDSM wamefanya utafiti au ugunduzi mkubwa wa kisayansi? Ni makampuni/mashirika mangapi yana mikataba ya uvumbuzi au maendeleo ya kiteknolojia na UDSM? Kumbuka chuo ni sehemu ya kuamsha akili na kumfanya mwanafunzi awe mweledi, awe mtafiti, na 'great thinker.'Umashuhuri na ubora wa UDSM umeshuka sana, na huo ni ukweli hii ya sasa sio UDSM ya 1960-2000 mwanzoni iliyokuwa ikivuma na kutoa wasomi mahili sana. Sasa hivi imebaki historia, tambo na majigambo yasiyo ya tija.
 
Hakuna chuo bora Tanzania Kama unao uwezo nakushauri ukasome Kenya cause all of their university are the best in the region but Kama ni Tanganyika Vyuo vinavyojitahidi ni SAUT Mwanza then Mzumbe! Why SAUT? Cause it is incorruptible institution in Tanganyika! And why Mzumbe? Cause it is the less corrupted public institution remained in Tanganyika.
 
Hakuna chuo bora Tanzania Kama unao uwezo nakushauri ukasome Kenya cause all of their university are the best in the region but Kama ni Tanganyika Vyuo vinavyojitahidi ni SAUT Mwanza then Mzumbe! Why SAUT? Cause it is incorruptible institution in Tanganyika! And why Mzumbe? Cause it is the less corrupted public institution remained in Tanganyika.

we ndio bogus kweli.
 
Hakuna chuo bora Tanzania Kama unao uwezo nakushauri ukasome Kenya cause all of their university are the best in the region but Kama ni Tanganyika Vyuo vinavyojitahidi ni SAUT Mwanza then Mzumbe! Why SAUT? Cause it is incorruptible institution in Tanganyika! And why Mzumbe? Cause it is the less corrupted public institution remained in Tanganyika.

We unaongea kinyume
 
nashukuru kwa ushauri wenu,lakini naomba wale wanaosoma ua walisha soma chuo wanipe weaknesses na strengths za chuo zao,please be open ili nipate picha halisi.
 
Back
Top Bottom