Hili ni somo ambalo linachanganya wengi sana ila kwa ufahamu wangu mfupi ni kuwa kwa sasa hivi kuna aina 3 za wayahudi.....
1 ASHKENAZI ambo walikimbia mateso ya utawala wa warumi na kuelekea upande wa kaskazini na kuishi katika dola ya KHAZARIA (kiasili sio wayahudi ila mfalme wao KHAGAN BULAN aliikubali dini hiyo na wafuasi wake wote wakawa wayahudi ) na baadae wakatawanyika kuelekea ujerumani na nchi nyengine za ulaya.kama historia ya wangoni walipotimuliwa na wazulu walikumba makabila mengine na kuyafanya waye wangoni.
2 SEPHARDIC / MIZRAHI hili ndilo kundi linalokisiwa kuwa ni wayahudi wa asili ambao walikuwa hapo falastina / palestina kabla na baada ya utawala wa warumi na mpaka waingereza walipokuwa wanitawala palestina wao walikuwepo hapo.wengine walihamia afrika ya kaskazini mpaka hispania / ureno (iberia) .baada ya vita ya kanisa CRUSADES vilivyoandaliwa na mfalme 2nd FERDINAND WA ARAGON na malkia 1st ISABEL WA KASTILLA ambao waliwatimua WAISALAMU na WAYAHUDI kutoka IBERIA ,waliobakia waliambia ni lazima wawe wakristo.mpaka leo kundi hili la wayahudi unaweza kulikuta MOROKO,TUNISIA,kiujumla wapo afrika ya kaskazini.Sefardik / Mizrahi wanapatikana afrika ya kaskazini, YEMEN,IRAN,SIRIA MPAKA INDIA.
3 kuna makabila tele ulimwenguni ambayo yanadai / kuwa ni ya kiyahudi ambapo afrika pia yapo mfano
ETHIOPIA (beta israel) inasemekana wana asili tangu enzi za nabii suleiman na malkia sheba/saba.
WALEMBA (ZIMBABWE) NK YAPO MENGI SANA.
HITLER katika final plan alisema kuwa wayahudi wote walioko ujerumani atawahamishia madagascar (MADAGASCAR PLAN) ,waingerza baada ya vita walikuwa na mpango wa kuwaleta uganda ( BRITISH UGANDA PLAN) ila baadae ndipo wakapelekwa hapo na kupewa ardhi ilokuwa imetengwa kwa nchi ya palestina.
kuna wengine wauoana huu mgogoro ni kuwa wa kidini,wengine wanaona ni wa kimaslahi zaidi (ardhi,maji nk ) suluhisho ni kuunda taifa moja lenye makabila hayo na wapange utaratibu wa kuishi kama ni shirikisho au vynginevyo..kwani hivi sasa wapo waarabu ambao wana uraia wa israil.kufanya mataifa ma2 ambapo waisrail hawakubali ile ramani ya mwaka 67 na wala hawawataki wale wakimbizi walong`olewa majumbani mwao wakati wa vita ................