What's wrong? mbona umeme haukatiki?

IslamTZ

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
309
182
Ndugu zangu
Kuna tatizo wenzangu sijui mmeliona?
Tangu jumamosi umeme upo, kuna mtu anajua kuna tatizo gani atuarifu tujue.
 
Ndugu,
Huko duniani mvua zinanyesha kwa hiyo maji yanatosha kwa sasa ila tunakoenda yakiisha tutarudi tuliko toka .
 
Nimevuka daraja la Mkapa jioni hii, mto rufiji umefurika maji vibaya sana, inaelekea mabwawa yanapata maji ya kutosha kuzalisha umeme.
 
MUngu mkubwa kawakumbuka wanawe wanaonyanyasika na dowans.tusubiri huo wa NSSF na huo wa upepo singida.
 
Isije kuwa mitambo ya Dowans tayari imenunuliwa....maana hiyo ni sirikali na sio serikali....
 
MUngu mkubwa kawakumbuka wanawe wanaonyanyasika na dowans.tusubiri huo wa NSSF na huo wa upepo singida.

Imani ni kitu chema lokissa lakini huo wa nssf na singida hautausikia tena mpaka mgao mwingine utapoanza ndo utamuona tena kikwete kwenye hotuba zake anagusia hayo maswala na lazaro nyarando kwenye vipindi vya asubuhi kwenye luninga
 
Ukianza mgao twaambiana, ukiisha kimya .. no word. ha ha ha ha Ndo mambo gani hayo yakhe kikwete na fisadi mwenzako Ngeleja?
 
IPTL went up to 70MW from 10MW. Sirikali imekubali kununua mafuta. Migodi also imepunguziwa umeme. And Dowans, InshaAllah will be switched on soon. And mgao will be history until for now.
 
Ukianza mgao twaambiana, ukiisha kimya .. no word. ha ha ha ha Ndo mambo gani hayo yakhe kikwete na fisadi mwenzako Ngeleja?
<br />
<br />

Katibu mkuu madini na nishati ndugu jairo alisema wametoa hela ya mafuta for IPTL and within 3 days tutashudia makali ya mgao kupungua? ww ulikuwa london hukumsikia?
 
Ukianza mgao twaambiana, ukiisha kimya .. no word. ha ha ha ha Ndo mambo gani hayo yakhe kikwete na fisadi mwenzako Ngeleja?
<br />
<br />

It was the same day zito akitoa tamko la ziara yake kiwira kwenye ofisi za bunge? Na jiro akazoza from wizarani Problem wanasiasa husikika zaidi kuliko watendaji
 
Sasa naanza kuona faida na umuhimu wa siasa ya vyama vingi:A S 39:!
 
Technical explanation...Kidatu is running @ full capacity as its small dam is full due to rains in MG

IPTL has gone up to 80MW from 10MW and the past few weeks Songas gas was down now its full capacity

If Dowans is injected to the grid it will ease but not finish loadshedding...Hale and Nyumba ya Mungu r running @ full capacity

Mtera is only 40 MW bt tht is understandable
 
nashkuru kwa mtoa mada na wachangia mada topic ya ukwel n coment pia mnastahili chupa moja moja ya tusker barid...
 
Ndugu zangu
Kuna tatizo wenzangu sijui mmeliona?
Tangu jumamosi umeme upo, kuna mtu anajua kuna tatizo gani atuarifu tujue.

HATUKUBALI, TUNATAKA GIZA LETU!
Haiwezekani wakati Julai Makamba (jina lingine la Januari linalotokana na mwezi ambao Dowans ilisajiliwa huko Costa Rica, na mzee Makamba akaamua kumpa mwanae kwa heshima ya Rostam) anaelekea kufanikiwa kuwashawishi Wabunge kupitisha mabadiliko ya sheria ya manunuzi ili kuipa Serikali mamlaka ya kununua mitambo chakavu (jicho lote liko kwenye mitambo ya Dowans), mvua zinaanza kunyesha na kuifanya Mtera kuzalisha umeme zaidi; wakati dili linakaribia kuiva huku RA na EL wanachekelea, halafu giza linatoweka! HAIWEZEKANI, HAIWEZEKANI! TUTAANZISHA MAANDAMANO MAKUBWA KAMA YA CHADEMA KUPINGA UNYANG'ANYI HUU WA DILI, WA MVUA KUNYESHA NA KUANZA KUJAZA BWAWA LA MTERA!
 
Ile mitambo ya Kidatu, Mtera, Nyumba ya Mungu na Pangani ilijengwa na Nyerere wakati huo idadi ya watanzania ikiwa haivuki milioni 25 kwa hiyo umeme ulikuwa unatosheleza hata wakati wa ukame uliosababisha njaa za mwaka 1974 na 1984 Dar haikuwahi kuwa giza totoro. Miaka 25 tangu Nyerere ameondoka madarakani, idadi ya watanzania imeongezeka tufikia zaidi ya milioni 40, lakini serikali zote zilizofuatia hazijawahi kuwa na mkakati wa kujenga mitambo mingine ya kuzalisha umeme. Badala yake wamekuwa wanafikiria kutafuta wawekezaji kwa ajili ya kuiba tu, halafu baadaye wanalalamika eti Nyerere hakutatua matatizo.
 
wa kwanza kaja na iptl, wapili kaja na netgroup solutions na kiwira watatu kaja , na aggreko, artumas, na richmond aka dowans
 
Jamani tulishasema kuwa ifikapo Machi mwishoni hakuna mgao TZ sababu mabwawa yatakuwa yamejaa.

Issue ni ufisadi wa temp generators na mitambo ya Dowans ndio inasababisha serikali na POLITICIANS kukaa kama wana vichaa.
Lakini sasa mambo yote safi, tender za emergency generators zimeshatoka na EL & RA wako busy kupata through 3rd parties.

Hakuna need ya TEMP Generators, TEMP SOLUTION ni serikali kununua FUEL YA IPTL for the next 12 months na KUORDER 200 MW GAS GENERATORS GE/WARTISLA ili ziwe nchini na kufungwa by DEC 2011. Ukiongeza na 160MW ambazo ziko njiani kuwa ready by late 2011, sulaa la mgao kwa 2012 halitakuwepo.

Lakini mabingwa wa ufisadi hawatafanya hivyo, watabuni solutions ambazo zinaiweka TANESCO WEAK FINANCIALLY SIKU ZOTE, kwa kutunga makampuni ili yauze umeme kwa Tanesco, na TANESCO ipangiwe bei chini ya cost na EWURA ili Tanesco wawe hawana jinsi.

Jiulize kwenye masuala ya umeme TZ, SONGAS Wako Profitable, IPTL wako Profitable, Artumas wako Profitable, Dowans wako Profitable, ila ni Tanesco tu ndio kila siku ina DEFICIT.

Halafu vichaa wengine wanataka NSSF iown KIWIRA ili Of COurse iwe Profitable, lakini ukitoa mawazo TANESCO waown na kuoperate KIWIRA utaona wanasiasa kama wanapandwa na kichaa wakikataa Kabisa kabisa. Wao wanataka Tanesco ifanye kazi ngumu ya Distribution lakini angle yenye profit ya Generation hiyo ni kwa Makampuni uchwara. Ujiulizi mbona serikali imetunga sheria makampuni independent waweze kugenerate power, lakini hakuna sheria ya Independent Distributors?? Jibu ni hakuna profit kabisa hapo.

God Bless Tanzania.
 
Hii mada imeniacha hoi kwa kicheko mpaka nimekosa cha kuchangia,kweli Tanzania yetu,yaani katika karne ya 21 watu tunashangaa umeme unapowaka siku tatu nne mfululizo wakati kwa wenzetu unaweza ukaishi miaka 20 na usione hata dakika moja ya kukosekana umeme.Ninalazimika kuamini kuwa wanasiasa hasa wa upinzani bado wana kazi kubwa ya kuelimisha watu ili wajue thamani ya utu wao na thamani ya kura zao.Maana kama watu wanafanya ujinga mnawapiga chini atakayefuata hataleta ujinga,lakini kwa mtindo huu.......wacha niwahi boksi mie naona nachelewa.
 
Back
Top Bottom