What if? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

What if?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkandara, Jul 26, 2010.

 1. M

  Mkandara Verified User

  #1
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu zangu najaribu kutazama possibilities hapa kwa akili ya kufikirika!..
  Mathlan Dr.Slaa akipata mgombea mwenza na mgomea Urais wa Zanzibar kuwa Salim A. Salim (ambaye aoondoke CCM) itakuwa vipi?

  Nimefikiria hili kwa sababu siwezi kuficha - I still have faith in this guy kwamba ni mwana Mapinduzi na anaweza kuondoka CCM kujiunga na ukombozi huu kwa sababu he has nothing to loose!
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  He Just Can't Mkuu
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Jul 26, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Itakuwa poa.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Hata mimi nadhani hivyo, lakini ndio ktk akili ya kufikirika!
  Hivi kweli hakuna kabisa tumaini yaani He just can't -hawezi?
  Je, viongozi wezee (waasisi) waliostaafu hawawezi pia! na kwa sababu gani hasa - FEAR?..
   
 5. Richard

  Richard JF-Expert Member

  #5
  Jul 26, 2010
  Joined: Oct 23, 2006
  Messages: 8,253
  Likes Received: 4,275
  Trophy Points: 280
  Mkuu heshima mbele,

  Wazo lako si baya ni katika kujenga.

  Dr Slaa na Dr Salim ni watu wenye upeo na mchakato wa kuleta maendeleo kwa faida ya wengi.

  Tatizo nilionalo ni kwamba wale wote walio katika mfumo ulioasisiwa yaani political establishment ya Tanzania haitapenda kuona wazo hili likiwepo kwa sababu kutakuwa na vikwazo dhidi ya watu hawa waliomo ndani ya mfumo huu endapo Dr Salim atakuwa raisi wa Zanzibar.

  Mfumo wa siasa wa Tanzania ulijengwa na hayati Mwalimu kati ya mwaka 1962 na 1985 na ni mfumo huu ndio ulimweka nje ya Tanzania tangu akiwa kijana mdogo na kumleta kusaidia tu pale alipokuwa (waziri mkuu na waziri wa ulinzi)

  Kwa hio sidhani kama mfumo huu ambao sasa hivi unaanza kutoa vijana walio watoto wa waasisi hawa kwenye siasa, utakuwa tayari kuona mabadiliko ya kumweka Dr Salim awe raisi wa Zanzibar.
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hapo ndipo penye matatizo Mkuu, kila Siyo wote walio katika CCM wanapenda la hasha ila Tatizo kwa Wengi SIASA ni AJIRA They FEAR WHTA IF WAKIUKOSA URAIS? WAKAWAPIGIE MAGOTI AKINA MAKAMBA YA KUOMBA MSAMAHA NA KUOMBA KUREJESHWA KUNDINI?
   
 7. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #7
  Jul 26, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Salim hana ubavu wa kutoka CCM; kwa yale waliomtendea mwaka 2005 angekwisha hama toka chama hicho siku nyingi!!
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu this is a very interesting perspective. Mh. Slaa alipo chaguliwa kuwa mgombea wa Chadema nikasema upinzani sasa umepata mtu mwenye personality na star power ya kuwezi kushindana na Kikwete. Lakini pia nikasema kutokana na propaganda machine na public relation na marketing campaigns za CCM bado personality na star power ya Slaa pekee haita tosha kumpa ushindi.

  SO mkuu nikawa nina waza ni nini kinacho weza kumpa Mh. Slaa added advantage wakati wa uchaguzi? Nika jisemea kuwa mafanikio ya Mh. Slaa katika uchaguzi huu uta tegemea sana na nani atakuwa mbombea mwenza wake. Mkuu Mkandara kwenye post yako naona ingekua vyema zaidi ungeuliza in broad terms kuwa mgombea mwenza yupi watu wanadhani angemfaa Dr. Slaa ili tupate mapendekezo ya majina mengi zaidi of course Mh SAS angeweza kuwa mmoja wapo.

  Mimi binafsi sijui wanasiasa wengi wa Zanzibar kwa hiyo siwezi sana kutaja majina ila nita toa vigezo vya mgombea mwenza ambavyo naamini vitamsaidia sana Mh. Slaa. Baadhi ya vigezo nitakavyo taja labda SAS anavyo au la. You judge mkuu.
  1) Mgombea mwenza ni makamo wa raisi mtarajiwa. Kwa sababu makamo wa raisi ni wa kwanza kwenye mstari wa kumrithi raisi iwapo chochote kita tokea mimi naamini kabisa kwama makamo wa raisi ni lazima awe mtu ambae ana weza kuwa raisi ikibidi. Kwa maana makamo wa raisi mwenyewe awe presidential material. Huwa mimi napenda kuamini kuwa anaye mfuatia raisi na yeye ana vigezo vya kuwa raisi.

  2) Mgombea mwenza mwenyewe lazima awe na personality na star power ili kuongeza nguvu kwenye campaign ya mheshimiwa. Asiwe a political compromise. Awe mtu ambae anaongeza kitu kwenye campaign. Ambae ana jina linalo jitegemea na si mgombea ambae itabidi atumie jina la Slaa kuji patia mwenyewe umaarufu. Hii itasaidia kuleta mvuta kwenye kampeni ya Slaa na pia kuondoa usumbufu wa kujaribu kumtambulisha kwa watu kwa maana muda huo hamna.

  3) Opposites attract. Ningependa mgombea mwenza nawe awe na sifa za ziada ambazo Slaa hana. Awe na uzoefu unao tofautiana na Slaa. Mfano ni Obama alivyo mchagua Joe Biden kuwa mgombea wake mwenza. Alimchagua mtu ambae ana foreign policy experience ambayo Obama mwenyewe alikua ana lack. Pia hii ita saidia kuonyesha wananchi kwamba chama kina wakilisha Watanzania wengi na siyo kikundi fulani tu katika jamii.

  4) Mgombea mwenza huyo awe na historia safi. Kwa maana asije na mzigo wowote toka nyuma. Maana kuna watu wengine sawa ni maarufu na sawa wana uzoefu lakini wana record ambayo ina weza isiwe mbaya sana lakini ikawa ina contradict image au ujumbe wa mgombea uraisi.

  5) Mgombea mwenza asiwe opportunist. Asiwe ana tumia kampeni ya Slaa kujaribu kutimiza nia na azma binafsi. Awepo hapo kwa mapenzi aliyo nayo kwa wananchi na kuwa tumikia. Awe mtu ambae watu wanaweza kumuona kama possible replacement ya Slaa na hii ni kwa manufaa ya chama kwa sababu bila mtu wa kupokea tochi mbeleni hata ushindi uki patikana uta kuwa wa ki"one hit wonder".

  Mkuu nina vigezo vingine lakini najua options zipo chache kwa hiyo ngoja niache hizi tano ili wigo wa majina uwe mkubwa zaidi. Najua SAS ana baadhi ya hivi vigezo lakini labda kuna mtu ambae ana vyote au zaidi.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Jul 26, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,177
  Trophy Points: 280
  Salim Ahmed Salim is not all he is trumped up to be. And I can go toe to toe on that with anybody who says otherwise.

  He may be a little better than Mr. Zero bin Sumaye, but that does not mean much.
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu Mkandara umeota kama alivyoota Freeman Mbowe kuwa wanampeleka Dr.Slaa kumshinda Kikwete wakati hawajakitayarisha chama chao kuchukuwa dola...mtu ndiye lakini mda tu siwo...ni sawa kwa Dr.salim!
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwanafalsafa1,
  Hakika nawe umezungumza yaliyokuwa akilini mwangu kabla sijaiweka mada hii. Nimejaribu sana kufikiria mtu ambaye ataweza kumsaidia sana Dr.Slaa katika nafasi ambazo anapwaya uzoefu kiutawala na mtu huyo atokee visiwani au mwenye asili ya huko, ndipo jina la Salim linapokuja. Hakika sipendi kabisa mfumo uliopo wa kuchagua viongozi wa juu kwa kutazama wanatoka wapi ikiwa kweli tunatambua na kukubali Muungano tulokuwa nao. Huu n mfumo huu unaashiria zaidi uroho wa madaraka zaidi wa uwakilishi wa katiba kwani dhahiri inaoynyesha hatuna imani na katiba au tunaamini maslahi yatalindwa ikiwa na tuna mtu kiti cha juu. Dhana hii imehindikana toka mwanzo na hakika sii Jumbe, Mwinyi wala Shein wameweza kutetea au kuwakilisha upande mmoja wa Jamhuri zaidi ya wabunge wa pande hizi mbili.

  Hata hivyo tupo ktk Taifa la Wagagagigikoko, watu wanaotazama vitu kwa rangi zake hivyo inatulazimu nasi kutazama ubora wa viongozi kwa vigezo vyao. Mimi siamini kabisa kwamba Salim hawezi kutoka CCM kwani kuna hotuba zilizopita amenipa moyo wa kufikiria yule Salim wa Umma party kaibuka tena. Na sidhani kama Salim ni mwoga na wala hana historia hiyo hasa ukimtazama enzi zake za UN alipowakalia kooni Marekani na UK kuhusiana na South Afrika. He had fought for Freedom and Justice all his youth na huu ndio wakati wake baada ya kutupiwa matope mwaka 2005. kama alivyosema Bulesi. Hakuwa na sababu ya kutoka wakati ule ule pasipo kuwashtua na wakaanza kumshughulikia mapema ila akiondoka leo inaweka akili zaidi...
  Waswahili wanasema Unaweza mtoa mtu shamba lakini huwezi kuuondoa Ushamba kwa mtu huyo!
   
 12. M

  Mkandara Verified User

  #12
  Jul 26, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kiranga,
  Mkuu unaposema toe to toe una maana gani? ebu nipe jina la mtu yeyote Tanzania ambaye mimi siwezi kwenda toe to toe na wewe!..mkuu hakuna binadamu asiyekuwa na mapungufu lakini pamoja na yote haya Salim - stand on his own.. Hakuna mwakilishi wetu hata mmoja aliyeweza kupata Umaarufu duniani zaidi yake akiwa waziri wa mambo ya nje, UN na hata OUA toka tumepata Uhuru. Pima kwa nafasi moja moja au zote kwa ujumla wake hata Nyerere mwenyewe alihofia uwezo wa Salim.
  Ukisema chuki binafsi hizo zinakubalika popote!
   
 13. B

  Bibi Ntilie JF-Expert Member

  #13
  Jul 26, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 245
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Chuki binafsi nazo huwa na matatizo yake! It seems Dr. Salim stepped on your toe at one point or another. Lakini tukichukulia historia yake kama kiongozi wa kitaifa na kimataifa aliyoianza tangu ana umri wa miaka 22, nani anayeweza kumshinda Salim kwa uwezo na uzoefu wa kuongoza?
   
 14. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #14
  Jul 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,287
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  That kind of poaching Chadema wakiiweza ndo itasaidia. Asikudanganye mtu, chaguzi nyingi za Afrika watu huchagua watu, si vyama wala sera. Ukiwaambia watanzania kuwa sera zako ni center right, au ni left, n.k. hata hueleweki. Watu ambao wana records au wenye uwezo wa kujenga hoja zikasimama ndo wanaochagulika. Pengine Salim may not be appropriate kwa sababu ya kufanya kazi sana ndani ya machinery ya CCM. He is more like them, na anaweza asiwe sauti ya mabadiliko tunayotaka. Ni mtazamo tu...
   
 15. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #15
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mkandara,

  Ndiyo tatizo la politics za compromise ambazo ahziangalii madhara ya huko mbeleni. Nina uhakika mfumo huu uliwekwa kwanza ili Zanzibar iliyo na wananchi wachache na eneo dogo zaidi wasione kama Muungano uta wameza kabisa. Kwa hiyo mfumo huu ulipewa kwa Zanzibar ili nao wajione kwamba wata kuwa na nguvu kwenye Muungano. Ubaya ni kwamba mfumo huu huu ndiyo una leta matatizo hadi leo ya watu kujiona Wazanzibar au Watanzania Bara. It was a good political move for the short time but bad for nation building in the long run.

  Pia mkuu huu mfumo wa kusema nafasi hizi zipewe watu wa eneno fulani naona kama lina tupunguzia wigo wa viongozi wanaofaa. Kwa maana kwamba kama "nafasi" au "muda" ni ya mtu wa eneno fulani basi hatuangalii nani anayefaa zaidi kutoka Tanzania bali nani anafaa zaidi kutoka upande fulani. Mimi naona hili ni tatizo nalo kama kupeana uongozi kutokana na udini au ukabila sema jamii yetu ime kubali hali hii na katiba yetu ime halalisha mfumo huu.


  Mkuu wakati wa mkutano wa kumtafuta mgombea wa CCM kule Chamwino uliyo fanyika Mei 2005 nilikua mtoto wa miaka kumi na tano. Wala sikuangalia ubora wa wagombea bali nami niliswekwa na mvuta na utashi wa kisiasa alio kuwa nao Kikwete. Looking back nadhani SAS ndiyo aliye kuwa the most qualified. Bahati mbaya huyu mkuu alifanyiwa fitna na Wazanzibari wenyewe(watu hao hao wanao lilia kupokezana which na mimi naona ni ujinga unao tupunguzia wigo wa qualifications na watu wanaofaa). Nakubali kweli kwa wakati ule asinge weza kuondoka hivi hivi maana kwanza asingekua na pakwenda. Pia alihitaji muda wa kurecover kutoka kwenye matokeo ya 2005. Nakubaliana na wewe kwamba muda huu ungekua muda mzuri.

  Tatizo ni kwamba kama mkuu Junius anavyo sema the chances are slim to non. SAS nina uhakika kama akihama CCM kwa usalama wake na future yake ni lazima aondoke pale ata kapo dhani kuna chance ya ushindi. SAS aende Chadema halafu CCM wachukue madaraka nasikitika kusema kwamba mzee huyu ana weza kuwa katika hali ngumu. Swali ni kwamba tu je yeye yupo tayari kutake a risk for the chance of making history? Ujasiri wa namna hiyo ni wachache sana walio nayo. Katika umri alionao yeye nina uhakika he is less of a risk taker now then he would have been if he was younger.

  Lakini pia tuna rudi pale pale lakini ndiyo hivyo ngoja niseme tu kuwa ukimuacha SAS sioni mtu Zanzibar ambae ana weza kushika mzigo wa makamo wa raisi. Ingekua ina wezekana kuchagua tokea Tanzania nzima ningeweza kutaja baadhi. Ila kwa Zanzibar the only one with the personality to take this chance is SAS. Kwa faida ya demokrasia Tanzania I hope SAS ata pata ujumbe huu na kufikiria. Pia sasa ni changamoto kwa Chadema kucome up with a VP candidate wanao ona atafaa na wamshawishi kuwa "Yes they can!"
   
 16. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #16
  Jul 26, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huyu Hamadi aliye kuwa msemaji wa kambi ya upinzani bungeni aweza faa na kufanya vyema, ni mzuri wa kujenga hoja, na hajaharibiwa na mfumo wa kifisadi!

  Salim, yes is good, but kwa umri wake si rahisi kuingia katika mpambano kama huu!
   
 17. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #17
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kwamba chaguzi nyingi za Afrika watu wanachagua mtu sio sera ni kweli lakini kumbuka kuwa chaguzi za Tanzania sio sawa na chaguzi za Afrika, inatatiza kidogo kuona kuwa waTanzania wanachagua mgombea kutokana na chama...

  Kuhusu Dr. Salim kuwa mgombea mwenza, mimi ningefurahi zaidi kuona Dr. Slaa anaunganisha nguvu na Maalim Seif. Ndugu yetu Prof. Lipumba akae pembeni. Kura zote za CUF kwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ziunganishwe na kura za CHADEMA nadhani moto wake utakuwa sio mdogo...
   
 18. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #18
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hamadi ana tajwa tajwa sana kama mtu mwenye uwezo lakini tatizo ni kwamba hana "star power". Kama mkuu kipimapembe alivyo sema kwamba Tanzania watu huchagua watu na wala si falsafa na sera. Hamad kwa nijuavyo mimi ni maarufu kwao lakini si Tanzania nzima. Hata kuwa msaada mkubwa sana in terms of kuvuta kura. Ana weza kusaidia kupata kura za Zanzibar kwa kiasi fulani lakini with 1 million people Zanzibar is really never a deciding factor kwenye national elections. hamad aweza kuwa kiongozi mzuri sana wa kitaifa lakini anabidi ajenge national profile nje ya circles za Bunge na kwa muda huu mchache uliyo bakia kwa 2010 hato weza.
   
 19. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #19
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Mkuu I beg to differ. Tanzania kama nchi zingine za Afrika ina chagua mtu siyo chama. Sema CCM wanajua hilo na wana build personalities ndani ya chama ndiyo maana kuna muonekano kuwa watu wana chagua chama. Angalia uchaguzi wa 2005....watu walichagua chama au watu walimchagua Kikwete? It's all about personality building and propaganda mkuu nashauri uchunguze hilo.
   
 20. Bantugbro

  Bantugbro JF-Expert Member

  #20
  Jul 26, 2010
  Joined: Feb 22, 2009
  Messages: 2,684
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu, watu walimchagua Kikwete kwa sababu alikuwa ni mgombea wa CCM na hivyo hivyo ingekuwa kwa mgombea yeyote wa CCM. Suala la Kikwete kushinda kwa kishindo hilo ni jingine na halimaanishi kwamba angeshindwa kama hangekuwa na mvuto!!!
   
Loading...