Ndugu unachozungumza kina ukweli kwa asilimia kubwa kwa wachezaji wa kitanzania wakikaa benchi basi na wao wanakuwa kama wamekata tamaa hivi. Ila wapo wachache wanaojitambua na mara nyingi sana napenda kuwatolea mfano Juma Abdul na Muzamiru Yasin. Juma Abdul watu wengi walishajua kapotea wakati wa Zahera pale alipomuibua Boxer lakini kwa kuwa Juma Abdul alikuwa anajitambua alipambana na pale alipopewa nafasi alifanya "come back" ya hatari. Muzamiru naye ni kama alishapotea Simba na kila mpenda soka nchini alimshangaa pale alipoamua kuongeza mkataba huku akisema kuwa atapambania namba yake Simba. Kwa kweli ni ujasiri wa hali ya juu unaopatikana kwa mchezaji wa kitanzania. N a kweli na yeye akafanya "come back" ya hatari.
Kwa wachezaji wa kitanzania kwao benchi maana yake ni kuwa uwezo umeshuka na yeye morali inashuka na kiwango chake kinaporomoka kabisa. Na hata pale anapopewa nafasi anashindwa kabisa kufanya vitu vya hatari kiasi kocha amshahau yule aliyekuwa anampiga benchi. Kwa mfano nawaangalia Kichuya na Luis walipewa nafasi kwenye mechi moja kama sikosei ilikuwa kati ya Simba na JKT lakini alichofanya Luis ni kumuonyesha kocha kuwa anakitu cha ziada cha kuisaidia timu ipate matokeo mazuri "team work" lakini mwenzake Kichuya yeye alitaka kuwaonyesha mashabiki kuwa mpira anauweza. Matokeo yake mpaka leo benchi linamhusu.
Nikihitimisha kwa upande wangu kuhusu Gadiel ni kuwa kila kitu kipo kwenye ubongo wake. Afanya mazoezi ya nguvu, arekebishe mapungufu yake kidogo sana kwenye kushambulia, namna ya kupiga krosi na asiwe analazimisha kupiga chenga kama Mohamed Husein kwani hana kipaji hicho na si lazima sana apige chenga. Baada ya hapo asubiri tu apewe hata dakika 15 uwanjani zinatosha kabisa kumshawishi kocha kuwa yeye naye ana msaada kwenye timu. Na kwa Gadiel kiukweli huwa anapata muda kiasi wa kucheza tofauti na wachezaji wengine ambao toka ligi ianze hawajawahi hata kukaa benchi. N a la muhimu kwa Gadiel na hata wachezaji wengine wanaokalia benchi wasitumie muda mwingi kuwaza watu wanowasema vibaya kuhusu viwamgo vyao badala yake wafanye mazoezi kwa bidii ili wawazibe midomo kama walivyofanya akina Juma Abdul, Saidi Makapu na Muzamiru Yasini.