BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,766
- 23,217
Bado Kesi iko mahakamani lakini tumebomolewa nyumba na kunyang'anywa ardhi tulitegemea mbunge ungekuja kusaidia namna ya kutafuta haki mahakamani lakini uko kimya. Wananchi masikini wamefungua kesi lakini kabla ya hukumu tumeondolewa kwa nguvu.
Nusu heka madale ndio unalalamika njoo Mpiji Majoe tukupe 1 heka.
Kama unataka kujua yuko wapi, yuko kawe na tangu wiki iliyopita amekuwa akikutana na wapiga kura wake maeneo mbalimbali.
Ni jumamosi tu alikuja hapa kizabizabina mmoja wa huko magamba akijifanya kumlalamikia Halima Mdee ushahidi wa kazi zake ulipofunguliwa hapa aliondioka bila kuaga. Sasa na wewe kama una nia ya dhati ya kutaka kujua mdee amefanya nini unaweza kufanya homework yako vyema kwa kusearch hapa hapa JF utaona thread zote za Mdee na majibu yake.
Bado sijaona umaana wa kumlaumu mbunge wenu wa Kawe katika jambo hili,tatizo wengi tunadhani ubunge ni zaidi ya sheria na taratibu zote zinazoongoza maisha yetu ya kila siku,sitaki kuingia sana katika kinachoendelea huko kwenye mgogoro lakini nimekuwa nikiona wananchi wengi wanadhani mbunge ndio suluhisho la kila matatizo yao jambo ambalo si kweli,mbunge anabaki kuwa mwakilishi wa wananchi kwenye chombo cha kutunga sheria huku akiwa na jukumu pia la kusimamia shughuli zote za maendeleo katika eneo husika,kumfanya mbunge kuwa ndio polisi,mahakama,idara ya ardhi na vyovyote vile ambavyo watu wanataka awe si jambo jema na tunakuwa hatumtendei haki mbunge yeyote bila kujali anatoka eneo gani.
Tubaki kuelewa kuwa si kila jambo basi linatakiwa kufanywa na mbunge,je mkuu wa wilaya anafanya kazi gani?Mkurugenzi kazi yake nini?Maafisa ardhi kazi yao nini?Tusipende kuwatwisha mizigo wabunge wetu kwa vitu ambavyo hawana maamuzi navyo
hebu tuongee ukweli wakuu,Mh Halima Mdee yuko wapi??naombeni jibu hapo,vilevile tunaomba record ya utendaji kazi jimboni mwake,tusiwe tunabisha kila hoja inayoletwa hapa bila kuwa na ushahidi!
Kumbe nyie wajinga ndio mmevamia viwanja vyetu sio?
Hata mimi nasikitika Halima Mdee ametuacha amekuwa kimya kama hakuna lilitoke jimboni kwake. mimi nina kiwanja nusu heka na nimejenga kanyumba kangu kadogo jamaa wamekabomoa?
wanasema eti sisi ni wakimbizi wanadangany'a public sisi ni wakimbizi kutika Congo mara sijui Burundi ili public iwasupport na kuona imefanya vyema. lakini yote haya yakitokea Halima Mdee amekuwa kimya yani nikikumbuka siku ya uchaguzi mwaka juzi niliamka alfajiri kwenda kumpa Mdee kura yangu yani roho inaniuma.
nashangaa kwanini hawa wabunge wanafuatilia mambo ya majimbo mengine alafu yao wanayanyamazia tu.
Halima Mdee tunakuomba basi ongea hata neno tukusikia sisi tunajua wewe unaujua ukweli wote dada yetu
Kama una jazba ya mambo yako ya kimaisha, haidha huna ajira, umebwaga na kicheche wako au umepatwa na jambo lolote linalofanana na hayo niliyoyaorodhesha basi usitumie uwanja huu wa great thinkes kuja kujifariji kwa kutoa mineno yako ambayo kimsingi haina mantiki katika hoja tajwa hapo juu. Sio lazima utoe maoni wala mawazo kama unajua hayajazi hata kikombe cha kahawa, ni bora ubaki nayo kichwani usubiri yapevuke ndio uyatoe maana ndio yanaweza kuleta manufaa zaidi.
Swala la mwananchi kutoa malalamiko yake kumuelekezea mbunge wake ni jambo ambalo linakubalika kabisa na hapa ndio maala sahihi kabisa kuyaleta ili kundi kubwa la watu waliolewa na mapenzi ya upinzani waamshwe kwa mifano sahihi kabisa, kwamba kuweka chama pinzani sio mwarubaini wa matatizo yanayotukabili wananchi, kama wengi wenu humu mnavyojiaminisha.
Ningependa kumaliza kwa kusema, viongozi wa chadema hawana utayali wa kuona mabadiliko kwa umma wa watanzania, bali wapo tayari kuutumia umma kwa ajili ya mabadiliko yao binafsi, kwenye hili la mabadiliko yao binafsi linajionesha waziwazi kwa kuona viongozi wa chadema wanavyoshinda na kula bata marekani mara kwa mara, wakitembelea magari ya kifahari na kupanga kwenye apartment za gharama kubwa, all in all wanawanyonya wanachama wao effectively na kuwatekenya kwa maneno matamu kama M4C na mengine mengi ya namna hiyo, wewe unaendelea kuenyeka huku wenzako wanapanda pipa tu. Badilika ubadili Taifa.
Haya maswala ya viwanja/aridhi siyo kwamba yanashughulikiwa na halmashauri ya mji/wilaya? Kama ndivyo, hao madiwani wenu wanafanya kazi gani? Hao ndo immediate representatives wenu, mbona hamuwawajibishi kwa maswala hayo ambayo yako mikononi mwao?
Kosa mlofanya ubunge mmempa MDEE urais mkampa JK Iliyobomoa ni serikali yenu dhalimu ulitaka afanyeje angekuwepo siku ya tukio angeweza kupigwa risasi na hao policcm. ushauri wangu andamaneni hadi magogoni kwa huyo mliyempa uraisWakati mwingine tunafikiri wapinzani ni dawa ya matizo yetu kumbe si kweli ukimya wa Halima Mdee kwenye tatizo letu la Madale hakika nimeushangaa sana.
Yaani ukavamie viwanja vya watu kwa mapanga na marungu alafu utegemee Halima Mdee aje kutetea uovu wako?
Apo tunadanganyana!
Kosa mlofanya ubunge mmempa MDEE urais mkampa JK Iliyobomoa ni serikali yenu dhalimu ulitaka afanyeje angekuwepo siku ya tukio angeweza kupigwa risasi na hao policcm. ushauri wangu andamaneni hadi magogoni kwa huyo mliyempa urais
Mama Porojo, Maralia Sugu, tandale one, yaani signature nyinginyingi tu, kesho utasema unaishi tandale kwa tumbo ooh mbunge wangu Mnyika, wiki ijayo utakuja na ile ya kike uliyoweka kapicha ka kuvutia utajifanya unaishi Arumeru. In short hamtawabadili mtazamo watanzania kwa JF, face book na hii mitandao ya jamii. Mwambie nape asimamie serikali yake kutekeleza ilani yao ya 2010. Hilo ndilo jibu, kushindwa hilo ndio anguko lenyewe, kumsakama Halima Mdee haitawasaidia, wapiga kura wameelimika. M4C daima, "Changes are innevitable, if you do not change, change will change YOU". Nape anajua, Mukama anajua, ila wanawaficha tu. Ndio maana leo tuna vyama vingi, unadhani CCM ilipenda vyama vingi, ililazimishwa na wind of change. Mwambie ndugu yako Komba, kama alifikiri alikuwa anaimba tu kuburudisha hadhira, basi hiyo ndio maana yake "The wind of change is sweeping accross the african continent. In fact is in Tanzania for real.
Kosa mlofanya ubunge mmempa MDEE urais mkampa JK Iliyobomoa ni serikali yenu dhalimu ulitaka afanyeje angekuwepo siku ya tukio angeweza kupigwa risasi na hao policcm. ushauri wangu andamaneni hadi magogoni kwa huyo mliyempa urais
wa kwanza alikuwa yupi we chakubimbi? yaani uvunje sheria halafu upinzani ukutetee we gamba? mbona hamuishi mambo nyie lakini? sasa hapo unataka kusema hafai ubunge kwa kuwa hajaja kukuona baada ya wewe kuvunja sheria? mtajifunza lini kuishi kwenye mstari jamani? mmezoea hadi mnaona kuwa ni utaratibu kuvunja sheria kha!
Hivi kweli mmevamia mashamba/viwanja vya watu na wenyewe na hati zipo na mawe niliyaona wakati wa taarifa ya havari kwa baadhi ya maeneo halafu mnataka mbunge aje asema ni mali yenu? CDM na wanasimamia haki, ukiona CDM mbunge hakufika jua hilo suala liko nje ya uwezo wake. Kama mna hati miliki ya maeneo nashauri jiungeni pamoja mkamwone mbunge, hana matatizo kabisa.