Amefanya mengi sana huyu dada wana kawe ndio tunaojua
Wakazi wa kawe? Mbona swali linaeleweka?
Tuhabarisheni mazuri ya mh. Mdee jimboni kwake?
angetusaidia barabara ya makongo juu- (kule ndanindani kwenda kwake) siyo pale chuo cha ardhi angeitengeneza yeye kama yeye "HALIMA MDEE" na sisi tufaidiiii!!!! kupitia mbunge wetu!!!kama waheshimiwa wengine walivyofanya m.f kuelekea kijijini kwa mtoto wa mkulima n.k
Non-emotional and Politically unbiased answers only please......
hakuna
Swali dogo tu lakini majibu kibao. Watu wanazuguka tu hapa! hapa tunataka data kama hizi, mfano "kabla ya mdee hajachukua jimbo kulikua na kero ya maji kwa wananchi na kwa sasa Mdee amewezesha upatikanaji ya maji kwa asilimia hizi, mfano mwingine labda Kawe kulikua na kero ya barabara, Mdee amewezesha kusimamia utekel;ezaji wa miradi kadhaa ya barabara kwa awsilimia kadhaaa, lingine mfano wakazi wa kawe walikiua na kero za viwanja, Mdee mpaka sasa amewewezesha kusimamia na kutekeleza migogoro kadhaaa! na vile vile tukubali kusema mapungufu yake ili tuweze kumsaidi, mfano, kabla ya Mdee kuchukua jimbo kulikua na hali ya amani na utulivu lakini sasa vitendo vya ujambazi vimekithiri!
Hebut tujaribu kujibu hili swala kwa muundo huu! maana mwanzisha thread ameomba mafanikia kwa jimbo la kawe
Hivi Dr. Makongoro Mahanga, mbunge wa Segerea ameshafanya nini bungeni kuwawakilisha wananchi wake?
Hivi Mheshimiwa Abas Mtemvu, mbunge wa Temeke ameshafanya nini bungeni/jimboni kwake?
Hivi Mheshimiwa Mwaiposa Eugeni Elishiringa wa Ukonga ameshafanya nini bungeni/jimboni kwake?
Hivi Mheshimiwa Ndugulile Faustine Engelbert mnamjua ni mbunge wa wapi? Mmeshamsikia? Kwa lipi la uwakilishi wa watu wake/watanzania wanyonge?
Basi hawa tuwalinganishe na aliyoyafanya Mh. Mdee ndani ya bunge na Jimboni kwake.
Nitajie mambo 3 aliyofanya katika katika jimbo la kawe
tunataka watu kama wewe wenye uwezo wa kutetea kwa mifano na sio kuleta ushabiki na matusi.Ngoja nikutajie mimi:
1:Amepigania chuo cha IMTU Kilikuwa kinatoza ada kwa dola za marekani sasa kinatoza kwa fedha za TZ, pia ada ya imesshuka na kuwa fixed.
2:barabara ya kutoka millenium tower kupitia njia shule ya chekechea hindu mandal , kupitia hadi jirani na nyumba ya meya wa kinondoni kutokea shoppers plaza ipo ktk hatua ya kuweka lami.
3: daraja la njia shortcut ukitokea rose garden bar kuja jirani na nyumba ya ridhiwani ( kutokea chuo cha school of journalism mikocheni)limejengwa, japo najua wengi wanahisi ni shinikizo la riz1, but remember mh mdee ndiye anakaa vikao vya maamuzi kupitisha.
hiyo ni kwa sisi wa mikocheni, pia mh mara nyingi anakuja kusikiliza kero zetu ,tatizo ktk vikao mkiitwa hamji! nahisi mleta hoja ni mtoto wa rita mlaki nini? maana umejibiwa humu jamvini na mwanaukweli na wengineo ila naona kichwa kigumu.
That said, let us also give a sober look at what president Kikwete has done for Tanzania for the past 7 years.Nilitaka kumwambia maana naishi kunduchi ambalo pia mbunge ni Mdee. Maji/umeme kawe ni vitu ambavyo si tatizo la kuumiza kichwa. Kile kichwa.... Ukitaka kuamini transfoma iharibike halafu tanesco walete longolongo, we mwambie wanamjua. Litabadilishwa siku hiyo hiyo
amejihaidi kutuwakilisha wanakawe kwa kuongea lugha za kihuni bungeni. eg. njuke et alNon-emotional and Politically unbiased answers only please......
tujulisheni ni basi yapi ha​yo sisi wanakerekwe....
Jee amefanya hivyo... mara nyingi bungeni mimi huwa naona anatetea mambo mengine.... kwanini asiwe kama Ndesamburo kule Moshi....