WFP yaonya kuhusu baa la njaa mwaka 2021

WFP yaonya kuhusu baa la njaa mwaka 2021

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,378
Mkuu wa shirika la mpango wa chakula duniani WFP ameonya kuwa huenda idadi kubwa ya watu wakakumbwa na baa la njaa mwaka ujao.

David Beasley amesema iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa, idadi kubwa ya watu huenda wakakabaliwa na uhaba wa chakula ndani ya miezi michache ijayo.

Mkuu huyo wa shirika la mpango wa chakula duniani amesema hali huenda ikawa mbaya zaidi mwaka ujao hata kuliko mwaka huu.Hali hiyo ya uhaba wa chakula inatokea wakati huu ambapo ulimwengu unakabiliwa na janga la virusi vya Corona.

Katika mahojiano na shirika la habari la Marekani la Associated Press, Beasley amesema shirika hilo lililoshinda ya tuzo ya Nobel linatuma ujumbe kwa ulimwengu kwamba hali inazidi kuwa mbaya.

Beasley amesema shirika hilo linahitaji bilioni 15 za Kimarekani mwaka ujao ili kuendesha mipango yake ya kusambaza misaada.
 
...Ni wakati Sasa kwa Tanzania ku export vyakula kwenda nje hasa bara la ulaya, Maana uku Michele na mahindi ni bei nafuu kabisa na maghara yamejaa vyakula
 
Mbona hawajataja sababu itakayopelekea? Lakini hawajatoa hata mapendekezo ya nini kifanyike zaidi ya kusema hatua madhunuti zisipo chukuliwa haraka. Hatua gani hizo?

Mi naona point yao ipo hapa
Beasley amesema shirika hilo linahitaji bilioni 15 za Kimarekani mwaka ujao ili kuendesha mipango yake ya kusambaza misaada.

wanataka hiyo noti tu mengine mbwembwe za kutishana
 
Tunafanya kilimo cha kijamaa kisicho na tija miaka na miaka. Nyakati kama hizi ndiyo tutaona madhara yake.
 
Alafu kuna wapuuzi walikuwa wanataka lockdown,hii tatizo lote limesababishwa na Corona,sasa tungejifungua tungelia sasa hivi.

Kenya wameiga ulaya ila kwa mujibu wa WFP,moja ya nchi itakayo kutana na balaa la njaa la kutisha ni Kenya.
 
Back
Top Bottom