Wezi wenye 'leseni ya kukuibia' Kariakoo

Wizara ya Mambo ya ndani inahitaji waziri Kama yule mama wa afya. Sio huyu my friend mtu wa watu
Mama wa afya Ummy? Maana huyu mpya ndio kwanza kaanza!
 
Mkuu sayansi kuna mafundi simu wa kueleweka?
 
Hawa walinitapeli mwaka jana Samora Avenue mkabala na maktaba ya British Council. Waliniuzia simu mbovu aina ya Vituz kwa 250,000 na t-shirt ya bure. Wanatembea na Noah.
 
Polisi kumejaa rushwa
uwezo wapolisi wengi kutafakuri ni zero
Mkuu inabidi tuanze na hawa jamaa wa k/koo na mizizi ya polisi wachafu wanaochafua jeshi letu

Siku watakapokagua vyeti vya shule vya Polisi wetu ndipo litageuka na kuwa safi vinginevyo ni kutwanga maji kwenye kinu
 
Ile safisha vyeti fake ilipaswa kupita huku pia. Naamini Polisi wa Tanzania ni moja ya corrupt organization, na wameshaona hawana la kufanywa. Ushauri wangu, Jeshi la Polisi lisukwe upya.
Haitoshi kulisuka upya bila kuboresha mishahara yao! Mishahara midogo wanayopata nadhani ndiyo inawafanya wapokee rushwa kirahisi ukizingatia na kazi wanazofanya ambazo nyingine ni hatarishi.
 
Wanajua wajibu wao ila hawataki kufanya kazi.
 


Tanzania kuna vituko sana kuanzia hao wauzaji hadi wanunuaji. Utanunuaje simu imeandikwa bundy (Bundi?) Ulisikia wapi?
 
Hii nchi viongozi wameishalemaa hadi haki itendewe ni eti namba moja hadi aseme, wengine wote ni kama wapo kwenye usingizi wa pono
 
Mkuu wizi na utapeli ni kila kona na mamlaka hazijaamka. Kuna wauza magari wengi matapeli na wana show rooms utafikiri ni watu wa maana kumbe wahuni tu.

Kuna uhuni dawa yake ni kudeal nao kihuni tu maana sheria haitokusaidia kuna mapungufu mengi.
 
Nimeuza simu Kkoo kwa zaidi ya miaka 5 kwa alichokisema mtoa mada ni kweli mtupu na tatizo ni watanzania kupenda vitu bei rahisi kwa Kariakoo asilimia 90 ya smart phone zinazouzwa ni used na za wizi.
Na unaweza ondoka Kkoo endapo ukiwa mkuda au kutokula pamoja na aliowataja mtoa mada.

Ushauri wangu unapoenda kununua simu Kkoo mwambie akupe simu ambayo iko ndani ya boksi ambalo halijafunguliwa na ujiridhishe kuwa imei iliyopo kwenye simu na na boksi ziko sawa.
 
Watu mkija kariakoo mje na wazoefu, sisi tunajua michezo yao yote tena hata mafundi simu wanawapiga sana dada zetu hasa wale wenye wameweka miamvuli kwa nje aisee, utawaonea huruma ila unakausha ndio maisha
Kweli mkuu, wale jamaa ukiwaachia simu imekula kwako hadi baadhi ya vifaa wanaiba wanakuwekea feki
 
Kwa brand kama LG au Sony wakikuwekea
Ndani itel huwezi jua kama sio mjanja

Ni wezi sana sana hapo kkoo na polisi wanajua kila kitu
ohoo hii balaa ... Sasa utafaham baada ya kufungua cover au hata kwa kuiangalia tu mkuu! Maana ni ngumu sana kupigwa kwa namna hiyo labda simu kama hautoiwasha hapohapo mbele yao. na kila brand ya simu ina namna yake ya ku display once inapokuwa ON
 
Wabongo ni tatizo kubwa sana, kwanini msiende kununua simu kwa wahindi au mlimani city.
 
Ndio maana nakwambia Nyie Dawa yenu nikusomewa visomo na kufukiwa mbuzi mzima ili uoze utumbo.


Unafurahia kula hela za wanaume.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…