Wezi Wapora Duka na Kumsahau Mtoto Wao


MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,878
Likes
5,072
Points
280

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,878 5,072 280
4157734.jpg


Polisi nchini Marekani wanawatafuta wezi waliovamia duka moja la madini na vito vya thamani na kuiba kabla ya kukimbia na kumuacha mtoto wao. Polisi wa Philadelphia nchini Marekani wanawatafuta wezi wawili walioiba vito vya thamani kwenye duka moja mjini humo kabla ya kukimbia na kumuacha mtoto wa kiume wa miaka minne.

Polisi walisema kuwa mwanaume na mwanamke waliingia kwenye duka la Platinum & Ice Jewelry wakiwa na mtoto na kuomba waonyeshe baadhi ya pete.

Ghafla wezi hao walichukua trei lililokuwa limejaa pete za dhahabu zenye thamani ya jumla ya dola laki moja na kukimbia nalo.

Wezi hao walimburuza mtoto huyo mita chache kabla ya kumtelekeza baada ya mmoja wa wafanyakazi wa duka hilo kuwakimbiza.

Polisi wanaendelea kuwatafuta wezi hao ambao walifanikiwa kutoweka eneo hilo na trei hilo la pete za dhahabu.

Mtoto wao amechukuliwa na kuhifadhiwa kwenye nyumba ya ustawi wa jamii.
 

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Messages
42,310
Likes
38,169
Points
280

Bujibuji

JF-Expert Member
Joined Feb 4, 2009
42,310 38,169 280
Hao walikuwa wanatafuta kujilikana.
Wazumbu ni mazumbukuku haswa,
wakitaka kufahamika watafanya kila wawezalo ili kutimiza adhma yao.
Sasa kwanini walienda kuiba wakiwa na mtoto wao?
 

Forum statistics

Threads 1,204,019
Members 457,048
Posts 28,138,417