Wezi wa Tanesco ni Sengerema Engineering Goup Ltd | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wezi wa Tanesco ni Sengerema Engineering Goup Ltd

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by DALA, Jul 12, 2012.

 1. DALA

  DALA JF-Expert Member

  #1
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 874
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 80
  Salaam kwa wote,

  Mimi ninamiliki biashara ya car wash maeneo ya Mabibo kwenye barabara ya kuelekea Loyola opposite na Jambo Garden.

  Nilikamilisha taratobu za kuomba huduma za Za umeme na kufanikiwa kulipa kiasi cha 1,175, 500/= kama gharama za kuunganishiwa umeme 06/02/2012. Mpaka leo, sijaletewa umeme zaidi ya nguzo waliouleta karibia miezi miwili iliyopita.

  Leo mida ya saa tano na nusu nilipigiwa simu na kijana wangu akinitaarifu kwamba kuna watu kutoka Tanesco wamekuja kung'oa nguzo ikabidi niongee nao kwenye simu, jamaa wakaniambia kwamba wanalazimika kung'oa nguzo kwasababu watu wanalalamika eti serikali haikuwalipa fidia nilipomuuliza maswali mawili matatu nikaona anashindwa kunipa majibu yakuridhisha ikabidi niende kuongeanao ana kwa ana.

  Nilishangaa kukuta gari aina ya Canter yenye namba T845 ASH inayomilikiwa na kampuni ya Sengerema Engeneering Group Ltd.

  Tulibishana matokeo yake walishindwa kung'oa nguzo baada ya kuishiwa hoja ikabidi niende Tanesco Magomeni kufuatilia.

  Nilichoambiwa ni kwamba hawa ni independent contractors wa Tanesco ila kuna wakati wanaiba vifaa kama hivyo kwa matumizi yao ya kampuni. Mapokeo ya Tanesco kwa kiasi yamenionyesha picha kwamba watumishi wa Tanesco wanalielewa hili ila ninashangaa hawachukui hatua stahiki kuondokana na watu kama hawa katka uchumi wetu.

  Tunakokwenda mbali kweli. Ngoja tuone!
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 12, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Pole sana, kwahiyo kama ni kampuni ya ya watu binafsi nani aliaambia waziweke awali hizo nguzo ni Tanesco au waliamua kuziweka wao? Hapo kunatatizo.
   
 3. DALA

  DALA JF-Expert Member

  #3
  Jul 12, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 874
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 80
  Hawa kwa kifupi ni wezi hawakuweka nguzo! Wanapita kuiba nguzo kutoka pale ambapo Tanesco wameweka bila kukamilisha kwa kufunga nyaya na mita! Actually walipoona kwamba nimewakalia vibaya ilibidi waondoke!
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Jul 12, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hii kampuni naijua huwa inafanya kazi za TANESCO. Sijui kama deal hizi huwa hazina mawaa. Hii ikimfikia Prof. Muhongo basi ata deal nao.
   
 5. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #5
  Jul 12, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Sengerema Engeneering Goup Ltd - Sounds like kampuni ya Ngeleja mbunge wa Sengerema
   
 6. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #6
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Dala, hadi leo kwa nini hujapta umeme? Waziri alitoa press release kuwa wale wote waliolipia wanatakiwa wawe wamepata umeme ifikapo 30 Juni. Kama Tanesco wameshindwa kukupa umeme unatakiwa kutoa taarifa Wizarani. Alitoa na namba za simu.
  Nenda Wizarani na risiti zako Mkuu na umwone muhisika.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Jul 13, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,688
  Likes Received: 82,549
  Trophy Points: 280
  Una akili sana wewe, inaelekea aliipigia debe ili ishinde zabuni ya mabilioni pale TANESCO.
   
 8. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #8
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sengerema ni jimbo la aliekuwa waziri wa zamanai wa nishati na madini ndugu Ngeleja aka Megawat, so its sound ni kama kampuni yake ndo maana its untouchable
   
 9. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #9
  Jul 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Naomba hizo number alizotoa Waziri Muhongo huku kuna watu wengi tu wamelipia lakini hawajafungiwa umeme, TANESCO wanadai hawana nguzo.
   
 10. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #10
  Jul 13, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280

  Huenda ikawa ni ya kwake, si unajua katoka hapo hapo wizara ya 'Umeme'?
   
 11. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #11
  Jul 13, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  BAK nimejaribu tu kuunganisha some dots. Maana Ngeleja ambaye ni mbunge wa Sengerema alikuwa waziri wa nishatii na madini na TANESCO ilikuwa chini yake. Na kwa kuwa walishaona rais ni dhaifu basi jamaa wanaunda tu vikampuni na kujipatia tenda za kuiba pesa za walipa kodi kama watakavyo. Too bad.
   
 12. Mtumpole

  Mtumpole JF-Expert Member

  #12
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 30, 2010
  Messages: 1,444
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  Hii bei ya 1,175,500 ni malipo ya umeme wa haina gani? Ebu fuatilia, utakuwa umeingizwa mjini.
   
 13. R

  Recover Member

  #13
  Jul 13, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sidhani kama ni kampuni ya ngeleja,MKurugenzi mkuu wa kampuni hii anaitwa Joseph Masindi yupo pale ubungo NSSF building ndio ofisi yao.Sijui sana kuhusu utendaji wao wa kazi,ila kama ni kweli basi duh sitajaribu kuwatumia nikipata tenda
   
 14. DALA

  DALA JF-Expert Member

  #14
  Jul 13, 2012
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 874
  Likes Received: 443
  Trophy Points: 80
  Ibra, nimepiga maktime mpaka nimechoka! Kama nchi inahujumiwa hivi unategemea nini? Tanesco hawaishiwi mistari, suluhisho ni kuweka serikali itakayokuwa na sauti kwa taasisi zake otherwise hapa hakuna kitu! The system is too corrupt to bring us development we want!
   
Loading...