Wezi wa Kariakoo wanatumia dawa au ni ujanja tu?

Jamani leo Sina raha hata kidogo wezi wamepitia simu yangu bila kujua...iko hivi , Leo nikiwa kwenye mishe zangu saa 3_4 hivi Mara nyingi nikiwa kariakoo natembea haraka kulingana na idadi ya watu coz ukitembea taratibu huwezi kupishana na watu , niko hapa mwaka wa 4 kwa hiyo mm si mgeni kwa jiji la Makonda....nikiwa natembea service road na mnavyojua wa dar kwenye service road Kuna watu wanasaka tonge na Maanisha machinga wanaouza vitu pembeni pembeni...kwa hyo njia kwa wapita kwa miguu haitoshi inabidi utumie nguvu kidogo ...sasa nikiwa napita Kuna jamaa kajikuaa (act) na mm ckutegemea akanipush na pembeni kulikuwa na wale wanaotengeneza simu nikayumba kidog nilivyorud nyuma kwa hasira coz jamaa niliona kafany kwa maksudi nikamrukia kwa miguu ...akanijibu ki ustarabu tu ...samahan kaka bahati mbaya nikaendelea na safar natembea hatua tano hivi naingiza mkono mfukoni cm hamna na pale hatujakaa hata dk moja .. .nikavuta kumbukumbu kipindi namrukia jamaa baad ya kunisukuma kulikuwa na wengine pemben na ndio wameniibia coz huy alienisukuma kwa makusudi nilimrukia kwa teke kifuatini akayumba ....muda huo ndio nadhani wameniibia coz hakureact hata kidogo. ....na mm baad ya kumwona hajareact nikamuacha na kuendelea na safar na ndio napiga hatua tano nakuta cna cm ....kinachonishangaz jamaa wanaiba faster na kupotea haraka sana ...nimerudi haraka sana cjawakuta na kutokana na idad ya watu waliokua pale wamejichangany ...Cha pili wale wanatumia dawa / kitu coz wametoa cm mfukoni chini ya dk1 bila kujua na mfuko ni marefu hata ukiweka cm haionekani ...naenda kumwomba mdog wg msamaha nilimtandika kwa hasir baad ya kuniomba na kung'ang'ania cm tukuwa kariakoo akitaka aone coz ilikuwa mpya ndio cku hyo tulinunua akajifany mjanja kariakoo akaniacha nyuma naongea na class mate yeye akaendelea na safar baad ya robo saa namkuta stendi amevimba macho eti kaibiwa nilimcharaz makofi kwa hasir na siku hyo kila mtu alifika nyuman kivyake ....MDOGO WANGU NISAMEHE KWA UJANJA WANGU NA MM LEO NIMEIBIWA NA WASELA MAVI......mpk sasa hv am more than 27 yrs ndio Mara ya kwanza kuibiwa bila mm kujua. dah..

Sent using Jamii Forums mobile app

Watu wanakata mpaka vidole vya mikono ili vilingane waweze kuiba vizuri, ukiwa Na hasira wataiba vitu vyako mpaka ukome, hata mtu akikufanyia kusudi gani usiingie katika ugomvi wake.
 
Hahahha k/koo haiishiwi wizi,.ila wengine wanatumia dawa nadhani..sio kwa kupotea huko ndani ya sekunde..
 
Mi niliwahi ibiwa tena kiboya kweli,
Mitaa ya tandika sokoni niliwakuta jamaa wanacheza michezo flani ivi ya kadi,zile kadi zina pande mbili upande wenye namba na usio na namba ,nikaangalia kwa makini kadi yenye namba kisha nikaweka fedha kama 60 thousands ivi,jamaa wakanambia umekula ongeza tena ili ule hela nyingi,nikaweka saa na simu aina ya OKING miaka ile zilikuwa zinauzwa 80 elfu,
Kufunua ivi bwana bwana ule upande nilioweka sio wenyewe! Nikaanzisha valangati pale la kutosha ,wale jamaa walikuwa wengi wakanizidi nguvu nikala vitasa pale na wakaondoka na mali zangu! Ikabidi niuze open shoes kwa buku tano ili walau nipate nauli ya kuendea kivule! Sijawahigi kumwambia mtu hii ishu coz baadae nilijiona ndezi kweli halafu ndio kwanza nilikuwa nina Krismasi moja mjini!
Mali zangu zimekwenda na vitasa juu nimerudi home uso umevimba! Sitasahau! Sasa iv nikiingia mitaa yenye tabsha kama iyo sitakagi utani na mtu kabisa ,,,sometimes natembea mkono mmoja mvukoni kama kizibo ili ile mikono ya hao hayawani isiingie mfukoni dadek


Sent using Jamii Forums mobile app
 
"sasa nikiwa napita Kuna jamaa kajikuaa (act) na mm ckutegemea akanipush na pembeni kulikuwa na wale wanaotengeneza simu nikayumba kidog nilivyorud nyuma kwa hasira coz jamaa niliona kafany kwa maksudi nikamrukia kwa miguu ...akanijibu ki ustarabu tu ...samahan kaka bahati mbaya nikaendelea na safar natembea hatua tano hivi naingiza mkono mfukoni cm hamna na pale hatujakaa hata dk moja ..."

Mkuu kwanza pole kwa kilichokukuta. Pili usijitaftie dhambi ya bure kwa kuhisi hao wa pembeni wasiohusika. Kutokana na uzoefu wangu nna uhakika wa asilimia zaidi ya 100 aliekupiga simu ni huyo jamaa aliekupush, na simu ilichomolewa the second alivyokupush. Ni kweli wapo wezi wanaotumia dawa, ila huo uliobiwa wewe ni wa kawaida tu

the Legend☆
 
Jamaa nahis alitokomea pasipo kujulikana

Sent using Jamii Forums mobile app
Daaahhh, k/koo ni noma imaisee kwa wezi.

Kuna jamaa aliporwa simu kwenye dala dala ilipokuwa kwenye foleni ile barabara ya China Plaza karibu na makutano ya barabara ya gerezani na ile ya posta.

Jamaa alikuwa anatumia simu ameishikilia mkono, kibaka kamvizia kwa nje akainyofoa akakimbia mbio sana, jamaa akajitahidi akatoka kwenye daladala kumfukuzia lakini akaishia kukuta ametokomea vichochoroni kwenye maduka ya simu, TV kwa upande kaskazini mwa barabara.

Mimi nilimuona huyo kibaka anakimbia nikawa nashangaa anakimbia nini kwa mbio hizo baadae nikamuona mtu aliyeporwa simu anamfukuzia ilihali kashatoweka.

Watu mara nyingi hawana ushirikiano wa kumblock kibaka na kuishia kimshangaa jinsi anavyotokomea huku wakiendelea na shughuli zao
 
Hapo Kkoo niliuziwa sabuni wakati nipo na hyo sabuni mfukoni nikaibiwa tena hyo sabuni wakizani simu daaaah

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG-20190224-WA0000.jpg
 
Tahadhari wazazi wanawapa Ada wanafunzi kipindi hiki shule zinapofunguliwa wawe makini na wezi Hawa wa mifukoni.ni rahisi zaidi kwa mtoto kuibiwa na watu Hawa kuliko mtu mzima .tumia mpesa .benki nenda mwenyewe mzazi kalipe.
 
Back
Top Bottom