WanaJF muda huu Waziri wa Mipango na Fedha Mustapha Mkullo, sijui naye ni alhaj au vipi, anatangaza kuwa bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania.
Mkullo anasema kuwa fedha za mwisho kufikisha kiasi hicho ziliingia leo asubuhi sana kutoka akaunti moja ya mwizi ambaye hata hivyo, kama kawaida, kwamba hana haja ya kumtaja kwa sasa.
Anasema hivi sasa kuwa fedha hizo zinazorejeshwa hazina riba. Kila mwizi anarejesha kama alivyochukua, bila kujali kama alizitumia kufanya biashara au vinginevyo.
Wakati akisema hivyo, wananchi nao, kama ilivyo kwa JF, wanataka kurejesha tu isiwe nongwa, wakamatwe na washitakiwe.

Huu ni ujinga mkubwa. Wakishindwa kuwachukulia hatua za maana hawa wezi, basi wananchi tuwe tayari kuchukua sheria mikononi mwetu kama vile tunavyofanya kwa vibaka barabarani.
Huu ni usanii tu na si ajabu pesa zinazosemwa zimerudishwa ni pesa hewa.
sasa Tuandamane, why r u swearing (ku2mia lugha ya ma2c).
Warudishe, na riba juu! Sisi 2kichukua vimkopo vidogo kwa kufuata utaratibu 2nadaiwa riba...let em pay thru their noses, kama hawakuzizungusha na kupata faida watajaza wenyewe

Mtanzania hata mimi nilikuwa na mawazo kama ya kwako. Hivi kuna ugumu gani kusema nanihii alihusika na ufisadi, amerejesha Shs kadhaa. Mbona wakati wa vita ya wahujumu uchumi miaka ya 80, waliokamatwa walifahamika???
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo katika hili la wanaorudisha kutokutajwa majina. Inawezekana kabisa ni mtego mzuri tu umewekwa ili kwanza pesa zirudishwe zote kisha ndipo serikali iende mahakami kuwashtaki.
Unajua mambo yakishafika mahakamani ndio basi tena, inabidi sheria ianze kuchukua mkondo wake na inaweza kuchukua muda mrefu sana. Na watu wa mambo ya fedha mnafahamu kitu kinaitwa time value of money, na ndio maana mnauliza mbona wamerudisha bila riba.
Waacheni kwanza warudishe pesa zote, kisha ndipo hatua za kisheria dhidi yao ifuate. Taarifa zisizo rasmi nilizozipata zinasema kwamba, tayari baadhi yao wameshanyang'anywa pasi zao za kusafiria.