Wezi wa BoT - EPA warejesha bilioni 50 hadi leo

Kamanda

Senior Member
Dec 5, 2007
150
176
WanaJF muda huu Waziri wa Mipango na Fedha Mustapha Mkullo, sijui naye ni alhaj au vipi, anatangaza kuwa bilioni 50/- kati ya bilioni 133/- zilizoibwa na wajanja-wajanja wetu, zimerejeshwa Benki Kuu ya Tanzania.

Mkullo anasema kuwa fedha za mwisho kufikisha kiasi hicho ziliingia leo asubuhi sana kutoka akaunti moja ya mwizi ambaye hata hivyo, kama kawaida, kwamba hana haja ya kumtaja kwa sasa.

Anasema hivi sasa kuwa fedha hizo zinazorejeshwa hazina riba. Kila mwizi anarejesha kama alivyochukua, bila kujali kama alizitumia kufanya biashara au vinginevyo.

Wakati akisema hivyo, wananchi nao, kama ilivyo kwa JF, wanataka kurejesha tu isiwe nongwa, wakamatwe na washitakiwe.
 
JAKAYA!!!! HEBU TUPA MZOGA UACHANE MAINZI
 
kikwete inchi kama imekushinda si uachie ngazi?????
 
Huu ni ujinga mkubwa. Wakishindwa kuwachukulia hatua za maana hawa wezi, basi wananchi tuwe tayari kuchukua sheria mikononi mwetu kama vile tunavyofanya kwa vibaka barabarani.

Huu ni usanii tu na si ajabu pesa zinazosemwa zimerudishwa ni pesa hewa.
 
Me nataka kujua zaidi kama RA amerudisha kamzigo ketu maana yeye na Jeetu walichota nyingi sana aise.... "hakuna mtu mbaya kama mhindi masikini" (page 119,makuadi wa soko huria, Chachage, S.L)
 
sasa Tuandamane, why r u swearing (ku2mia lugha ya ma2c).
Warudishe, na riba juu! Sisi 2kichukua vimkopo vidogo kwa kufuata utaratibu 2nadaiwa riba...let em pay thru their noses, kama hawakuzizungusha na kupata faida watajaza wenyewe
 
Huu ni ujinga mkubwa. Wakishindwa kuwachukulia hatua za maana hawa wezi, basi wananchi tuwe tayari kuchukua sheria mikononi mwetu kama vile tunavyofanya kwa vibaka barabarani.

Huu ni usanii tu na si ajabu pesa zinazosemwa zimerudishwa ni pesa hewa.

Mtanzania hata mimi nilikuwa na mawazo kama ya kwako. Hivi kuna ugumu gani kusema nanihii alihusika na ufisadi, amerejesha Shs kadhaa. Mbona wakati wa vita ya wahujumu uchumi miaka ya 80, waliokamatwa walifahamika???
 
Hivi wana JF

Hivi nchi yetu ya Tanzania tunaelekea wapi haswa? mbona ujanja na usanii umekuwa mwingi kwa viongozi wetu ambao tumewapa dhamana ya kuliongoza taifa na watu wake?

Maana si rais tuu hata viongozi wengine wenye dhamani nyeti kama AG, Hosea et al....they are just sitting and getting their fat paycheck doing nothing!

Honestly, hata kwa kipofu na mjinga, hii hali inatishia uhai wa taifa letu.

I dont know what to say, But Iam really afraid where JK is taking this country!
 
sasa Tuandamane, why r u swearing (ku2mia lugha ya ma2c).
Warudishe, na riba juu! Sisi 2kichukua vimkopo vidogo kwa kufuata utaratibu 2nadaiwa riba...let em pay thru their noses, kama hawakuzizungusha na kupata faida watajaza wenyewe

NIMECHOKA NA SERIKALI YANGU KUNIDANGANYA KILASIKU KAMA MJINGA, KIFUPI SERIKALI INANITUKANA WAKATI MIMI NDO NINAWAFANYA WAISHI (KWA KODI NILIPAYO) KWANINI NISIWATUKANE BWANA.. WASHENZI TU HAWA
 
sasa Tuandamane, why r u swearing (ku2mia lugha ya ma2c).
Warudishe, na riba juu! Sisi 2kichukua vimkopo vidogo kwa kufuata utaratibu 2nadaiwa riba...let em pay thru their noses, kama hawakuzizungusha na kupata faida watajaza wenyewe

NADHANI WAJUA KITAKACHO FATA MARA BAADA YA WANANCHI KUCHOKA KUTUKANA, KUNAWAKATI HUWA NAWAZA NA KUSIKITIKA AMBAYO OSAMA ANAWALENGA KWA MASHAMBULIZI RAIA WA MAREKANI WASIO NA HATIA WAKATI UKWELI KABISA HII KAZI INGEKUWA BARABARA KAMA ANGILENGA KWA VIONGOZI WETU
 
Jamani ujinga huu hawajaanza leo! Mi nakumbuka kuna ishu ya upatu (pyramid scheme)ambao ulichezeshwa na wake za vigogo, wakawalaghai akina dada, akina mama na akina bibi zetu! Ile kesi ilifunguliwa mahakamani ya madai lakini cha ajabu wale waliokuwa wako kimbelmbele walilipwa pesa zao na hawa waanawake wakaingia mitini.
Sasa na hii wanataka kutulete mazingaombwe hayohayo. Lakini haitawezekana! Sisi wanaJF tuna kazi ndogo sana. Ni kuhakikisha kama kaziyako ni ya uandishi ufanye kazi ya kuandika makala kama ni mfanyakazi wa kawaida anza kuchangisha mawazo wafanyakazi wenzako. Hii ndo grass root movement! Na mi naamini kabisa tuanze petition - inawezekana! ni sisi tu kuamua!
Hivi Tanzania issue ya petition ipo, ili tumwandikie rais na tuipublish kwenye magazeti!
 
Mtanzania hata mimi nilikuwa na mawazo kama ya kwako. Hivi kuna ugumu gani kusema nanihii alihusika na ufisadi, amerejesha Shs kadhaa. Mbona wakati wa vita ya wahujumu uchumi miaka ya 80, waliokamatwa walifahamika???

Nakuunga mkono mzee, hawa jamaa wanatuchezea mazingaombwe. Kama waliweza kututanzgazia majina ya makampuni yaliyohusika leo wanashindwaje kutueleza kampuni so and so wamerudisha kiasi fulani. Ni kweli inawezekana kabisa zikawa ni pesa hewa.

Hivi kazi kubwa ya hawa jamaa ilikuwa ni nini hasa. Kurushisha pesa tu au kuzifualia na kuwafikisha jamaa mahali panapostahili kuwa judged na vyombo husika.

Dalili za mvua ni mawingu. Sioni dalili zozote zaidi ya utapeli tunaofanyiwa. Hivi kweli timu inayo wa-include AG na Hosea ambao tayari wako implecated kwenye skandali la RICHMONDULI kweli wataweza kutufanya kazi tunayotarajia. Hawa jamaa kama kweli ni wachapakazi wazuru na ni wasafi wangesha tusaidia kweli ile issue. Kushindwa kwao tayari kuna tuondolea imani. IGP I am not sure, lakini kwa njisi ninavyoona kesi ya Dito inavyopotea hewani, imani inaniishia. MUNGU TUSAIDIE WADANGANYIKA!!!!!
 
Ebu tujikumbushe kidogo hotuba aliyoitoa Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Bungeni tarehe 30 Desemba, 2005 kuhusu Rushwa (ufisadi):

"Tutaongeza kasi ya kupambana na rushwa kisayansi kwa kushambulia kiini chake, na kuziba mianya yake. Tutajitahidi kuongeza mishahara na kuboresha maslahi ya watumishi wa umma ili kupunguza vishawishi vya rushwa. Tutaendelea pia kuongeza uwazi katika maamuzi ya Serikali hasa katika manunuzi na mikataba. Tutaimarisha uwezo wa kifedha na kiutendaji wa taasisi zilizo mstari wa mbele kwenye vita dhidi ya rushwa, hususan Taasisi ya Kuzuia Rushwa, Jeshi la Polisi na Mahakama. Lakini yote hayo ni bure iwapo wananchi hawatajitokeza kusaidia vyombo hivyo. Naomba ushirikiano huo kutoka kwa wananchi.

Katika harakati za kupambana na rushwa yapo mambo mawili mengine ambayo tutayaangalia kwa karibu. La kwanza ni mikataba. Tutaangalia upya taratibu za mikataba mbalimbali inayoingiwa na Serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kuongeza uwazi na uwajibikaji. Mikataba ni mwanya mkubwa wa rushwa hasa zile kubwa kubwa za wanaotafuta utajiri.

Kadhalika, hatuna budi kuchukua hatua thabiti za kuzuia watumishi wa umma kutumia nafasi zao kujitajirisha na kujilimbikizia mali. Sisemi kwamba ni haramu mtu kuwa tajiri au kuwa na mali. Ninachosema mimi kuwa ni haramu ni kutumia nafasi yako ya utumishi au uongozi wa umma kujipatia manufaa ya kujitajirisha au kujilimbikizia mali.

Jambo hili ndilo linalokera sana watu kuona mtu ambaye hana chochote lakini miezi michache tu baada ya kupata cheo anakuwa tajiri mkubwa. Ona majumba ya fahari, ona madaladala, teksi bubu, anaishi maisha ya kifahari na kadhalika. Wananchi wanayo haki kuhoji, na wanayo haki kupata majibu. Ndugu zangu, naomba tuwe waadilifu. Tusilaumiane. Nataka Tume ya Maadili ya Viongozi isione haya kutuuliza jinsi tulivyozipata mali tunazosema tunazo. Nitawasaidia kujenga uwezo wa kufanya hivyo kama tatizo lenu ni hilo".

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete...ulisema mwenyewe....sasa tunataka majibu sahihi ni akina nani hao wanaorejesha hizo pesa na kwanini hadi sasa hawapo Keko au Segerea...ulituambia mwenyewe kwamba tunayo haki ya kuhoji...sasa twambie tuwajue wezi wetu ni akina nani?
 
Jamani nimejaa matusi ktk Nafsi yangu ila najistahi
Huu uongo wa perememde wakawadanganye watoto wao nyumbani.
Nadhani hii ni CHEMSHO la kwanza la Mkulo na yatakuja mengi.

TUNATAKA WALIOHUSIKA WACHUKULIWE HATUA full stop. Kurudisha haitoshi, ina maana walipokuwa wanaiba walifanya bahati mbaya??

Naunga mkono hoja ya petition.
 
Heshima Mbele,

Mie sina jazba ila ningependa kujua ni kina nani wamerudisha pesa ya EPA?na wataajwe kwa majina.na kwanini wamerudisha pesa bila riba na wameichukua kwa muda mrefu??tuambiwe majina yao na lazima wawe na slip.Mlioko BanK naomba mtuambie ni kina nani wametoa pesa hizo.!na ningependenda list iwe wazi.Mziki wa leo uko wapi?ni walipoti ya EPA nadhani..Mwanakijiji uweke mapema coz nimeshamaliza mazoezi
 
Nakubaliana na wengi kuwa huu ni usanii. Kuna uwezekano wa mambo yafuatayo
1 Fedha walizochukua ni nyingi zaidi ya 133bn/=, lakini kwa kuwa tunajua hizo tu, basi, watasema wamelipa deni. Tukitaka kujua ni kiasi gani hasa walikchukua ukaguzi uende zaidi ya 2005, uanzie 2000.
2 Wanarejesha hizo ili waonewe huruma na wasamehewe. Inabidi kujiuliza ni watanzania wangapi wamekufa kwa wao kuchukua hizo fedha zetu? Ukosefu wa dawa, wanafunzi kukosa walimu na madarasa, kukalia mawe nk.ni kero walizozisababisha
3 Fedha zinarudishwa kwa kutumia account bandia ili tracing ya wahusika iwe ngumu zaidi.
Tuwe macho, hivi kweli JF tumekosa mjasiri wa kutupatia majina ya hao waliorudisha?
 
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo katika hili la wanaorudisha kutokutajwa majina. Inawezekana kabisa ni mtego mzuri tu umewekwa ili kwanza pesa zirudishwe zote kisha ndipo serikali iende mahakami kuwashtaki.

Unajua mambo yakishafika mahakamani ndio basi tena, inabidi sheria ianze kuchukua mkondo wake na inaweza kuchukua muda mrefu sana. Na watu wa mambo ya fedha mnafahamu kitu kinaitwa time value of money, na ndio maana mnauliza mbona wamerudisha bila riba.

Waacheni kwanza warudishe pesa zote, kisha ndipo hatua za kisheria dhidi yao ifuate. Taarifa zisizo rasmi nilizozipata zinasema kwamba, tayari baadhi yao wameshanyang'anywa pasi zao za kusafiria.
 
Hapa bado tunachezewa tu. Swali ni kwanini hawatajwi? Au ndio hawatajiki? inaonekana hiyo ni trick, au naye Mkullo ni waziri wa fedha jina, kuna mwenyewe anayeoperate under the carpet.
 
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo katika hili la wanaorudisha kutokutajwa majina. Inawezekana kabisa ni mtego mzuri tu umewekwa ili kwanza pesa zirudishwe zote kisha ndipo serikali iende mahakami kuwashtaki.

Unajua mambo yakishafika mahakamani ndio basi tena, inabidi sheria ianze kuchukua mkondo wake na inaweza kuchukua muda mrefu sana. Na watu wa mambo ya fedha mnafahamu kitu kinaitwa time value of money, na ndio maana mnauliza mbona wamerudisha bila riba.

Waacheni kwanza warudishe pesa zote, kisha ndipo hatua za kisheria dhidi yao ifuate. Taarifa zisizo rasmi nilizozipata zinasema kwamba, tayari baadhi yao wameshanyang'anywa pasi zao za kusafiria.

Ninapinga hoja yako kuwa tuwaache warudishe kimyakimya.
Ni budi waanikwe ili SISI wenye fedha zetu tujue kinachojiri kuhusu akaunti ya madeni ya nje. Ila naona kuna janja ya kufunika kombe hapa maana mbona ripoti kamili ya uchunguzi ya BOT haitolewi?? Au mpaka hoja ya kuteua kamati ya bunge ipitishwe???? Tunataka kila takataka imulikwe ili iwe rahisi kuichoma na kuondoa harufu ya uozo. Endapo hatua hazitachukuliwa basi nitaamini kuwa serikali imehusika kuwaibia wananchi hela zao
 
Mimi nina mtazamo tofauti kidogo katika hili la wanaorudisha kutokutajwa majina. Inawezekana kabisa ni mtego mzuri tu umewekwa ili kwanza pesa zirudishwe zote kisha ndipo serikali iende mahakami kuwashtaki.

Unajua mambo yakishafika mahakamani ndio basi tena, inabidi sheria ianze kuchukua mkondo wake na inaweza kuchukua muda mrefu sana. Na watu wa mambo ya fedha mnafahamu kitu kinaitwa time value of money, na ndio maana mnauliza mbona wamerudisha bila riba.

Waacheni kwanza warudishe pesa zote, kisha ndipo hatua za kisheria dhidi yao ifuate. Taarifa zisizo rasmi nilizozipata zinasema kwamba, tayari baadhi yao wameshanyang'anywa pasi zao za kusafiria.

Mkuu hii approach yako ya kusubiri warudishe wote., ndipo tuwaswage kortini...Hii SIO YENYEWE..

Hivi tuna uhakika gani kuwa watarudisha? Ni kweli kuwa suala wao kurudisha hii pesa ni suala muhimu kuliko hili la kortini, lakini binafsi nina wazo..tunachotaka waturudishie ni chetu..sio kwamba tunaomba na kuhitaji ridhaa yao ..hivyo tuwe aggressive jamani..Kwa nini tum'bembeleze mwizi wetu eti tumsubiri ajipange ili aturudishie chetu? Hiki ni chetu wajameniii..

Cha kufanya wakuu, ni kuwa-identify woote na kuwafilisi on the spot na kuwaswaga kortini baada kuwa tumejiridhisha kuwa wameturudishia chetu na compound interest isiyopungua 33%...

Hii ndio exact retrobution wanayostahili mafisadi kwa machungu waliyotupa watz..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom