The Technologist
JF-Expert Member
- Jun 7, 2015
- 1,394
- 2,801
Sikiliza mkuu,Sasa kuna mtu mkamilifu? Kama Yesu alikataa kuitwa mwema, wewe ni nani? Kutotoa fungu la kumi kanisani kwa kuwa Mchungaji naye ana dhambi, ni hoja isiyo sahihi (muflisi).
Umechanganya! Kuhani alikuwa anafungwa kamba pale alipokuwa anaingia Patakatifu pa Patakatifu tu, kila mara moja kwa mwaka kwa ajili ya kujisafisha na upatanisho wa Waisraeli. Dhabihu na zaka zilitolewa nje ya hema ya hekalu.
Mind you, amri ya zaka ni ya milele, hakuna sehemu kwenye Biblia ilipobatilishwa. Kasome Malaki sura ya mwisho.
Zingatia hili: sehemu sahihi ya kutoa fungu la kumi, zaka ni hekaluni peke yake. Wa kukabidhiwa ni Mchungaji/kuhani anayehudumu kwa muda huo.
Ukipeleka kwa wahitaji, hiyo si zaka bali inakuwa sadaka ya kawaida.
Hayo yapo na yanatokea, hatukatai, ila suala la zaka halibadiliki.
Nioneshe hapo Kanisani kwako Yule Yesu aliyesema Viwete watatembea, viziwi wataskia, vipofu wataona alafu watu watajazwa Roho Mtakatifu nitakuunga mkono...
Fungu la kumi watu watoe ila watoe Kwa watu wenye nahitaji ya kweli.
Mtumishi halisi wa kweli wa Mungu huyo ukitoa zaka kwake tayari una baraka za Mungu, wengi Wana mambo mawili, maisha mawili...