Unaelewa kwa nini Sulemani alisema anayezini anaharibu nafsi yake, anatoa heshima yake kwa mwingine?
DHambi ni dhambi,iwe inaharibu heshima ama haiharibu,mtu ambaye anaharibu heshima yake kwa kuzini alafu akaomba msahama ili asiadhibiwe bado ni jambo jema kwa sababu heshima yake hakuiharibu kwa watu wote.
So adhabu ya Mungu na kukosa heshima bora uepuke adhabu ya Mungu kwanza hayo mambo ya heshima yanaweza kuwa fixed kadri Muda unavyoenda.
Utasamehewa ila side effect ya zinaa yako kwenye uchumi wako itabaki.
Kumbuka pia wqpo wanaozini bila kuathirika kiuchumi,sisi masikini ndio tunazini hovyo na kuhonga huku vipato vikiwa haviruhusu.
So kuna watu wanazini na bado Mungu anawabariki kiuchumi kwa sababu baraka za Mungu zinazidi machukizo ya zinaa.
Kupewa msamaha na Mungu hakukufanyi usiwajibike kwa kosa/dhambi uliyoitenda. Umeelewa?
Kuwajibika kwa kosa kokote ambako sio kuwajibika mbele za Mungu basi kuwajibika huko kunategemra na hali ya Mtu.
Kama wewe ni masikini umezini na kuhonga pesa ya kula basi utawajibika kwa kulala njaa.
Kama ni masikini umehonga pesa ya pango basi utawajibika kwa kulala nje.
Kama ni masikini umehonga pesa ya matibabu basi utawajibika kwa kuugua muda mrefu.
Mbali na hapo wapo wanaozini huku wakiwa na vipato vyao na wala zinaa haiwaathiri kwa chochote katika maisha ya kawaida mbali na ile athari ya kwamba ni dhambi mbele za Mungu.
Mwisho, hutokuwa na heshima hata kwa huyo Mungu
Mungu ninayemuamini Mimi hata ukiwa umeua na kuzini mara nyingi alafu UKATUBU basi heshima yako kwake iko pale pale kwa sababu Mungu ninayemuamini ni mwingi wa kusamehe na anawajua waja wake kwa sababu kawaumba.
Mungu wangu hana vinyongo kwa sababu dhambi ninazofanya yeye hazimdhuru wala kumnufaisha kwa nini aniondolee heshima moja kwa moja wakati namuomba msamaha ?
Mungu unayemuelezea huyo ni Mungu wa vinyongo na waja
Yaani unatenda dhambi kwa makusudi ili utub
Kwa hiyo BORA NITENDE DHAMBI KWA MAKUSUDI ILI NISITUBU ?
Utapima mwenyewe kipi bora kati ya kutenda dhambi kwa makusudi ili utubu na kutenda dhambi kwa makusudi ili usitubu.😄😄