Ze Heby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 5,910
- 6,716
Unajua leo bwana nikiwa najiandaa kwenda kazini nimekaa nikawaza,
Nini hiki? Yaani nifanye kazi kwa ajili ya watu, nikiwa na malengo ya kuwa financially free.
Kweli kabisa, yaani niwe financially free kwa kulipwa kwa muda wa kazi?
Ni ujinga wa hali ya juu, mtu unajua Mshahara wako ni fixed, na unategemea ipo siku utakuwa na hela ya kufanya unalo taka?
Kweli sisi wamatumbi ni sawa na mwanyama wa mwituni kabisa, hatuna mafikirio ya mbele, huwa unawaza kuhusu survival na ngono tu.
Imagine unatumikishwa day to day, na hakuna siku utakuwa free, mpaka unastaafu na miaka 60. Utakacho ambulia ni mafao tu, ambayo yatakukuta hauna plan, na mwishowe hiyo hela utakosa mianya mzuri ya kuji multiply.
Sasa nani atakuja kukuamsha kutoka kwenye hilo jeneza la kuajiriwa?
Basi, bwana nisiwachoshe ngoja Twende tukaendelee kufanya jambo lile lile kwa miaka 50 straight.
Hii haiko straight kama inavyoelezwa. Tunapaswa kufahamu kuwa financial freedom haitokani na chanzo cha mapato yako, bali jinsi unavyotumia kipato chako. Kwa mfano, mtu anaepata kipato chake kwenye ajira anaweza kukitumia kujijengea uhuru wa kifedha na akawa huru kifedha kuliko hata aliejiajiri. Hakuna formula moja kwa watu wote. Kuna watu wengi tu wameajiriwa na wanapata pesa nzuri sana na wamefanya uwekezaji wao na wanaweza kustaafu ajira mapema.