Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,742
- 25,678
“Muambie hata aende akajitembulishe kwenu kwanza, usikubali tu kumbebea mimba mtu ambaye hata kwenu hajulikani, kama anakupenda basi ataleta hata Barua ya posa na kutoa Mahari!” Agness alimuambia rafiki yake ambaye alionekana kuchanganyikiwa, ni muda mrefu sana Neema alikua anasumbuliwa na mpenzi wake Jeremiah akimuambia kuwa anataka kuzaa naye.
Kila mara alimuambia kuwa hawezi kubeba mimba kabla ya ndoa kwani nyumbani kwao hawatamuelewa, lakini kila alipokataa Jeremy alipunguza mapenzi na kujifanya kukasirika akijifanya kuwa kaumizwa. Ushauri wa Agness aliuona mzuri kidogo kwani angalau ilimaanisha kuwa alikua anaenda kutambulika na ilikua ni hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye ndoa.
Siku iliyofuata alimfuata Jeremy na kumuambia kuwa kama anataka abebe mimba yake basi angalau akajitambulishe kwao, tofauti na alivyotarajia labda Jeremy atakataa haikua hivyo, alikubali na kuanza maandalizi ya kutambulishwa. Alianza kwa kwenda yeye mwenyewe kisha kutuma watu na hata kumlipia Mahari.
Hapo ndipo Neema alianza kujiona kama mke wa Jeremy alimuamini na kwakua wote walikua na kazi zao wakati wakiwa katika maandalizi ya kufunga ndoa, ingawa Jeremy hakusema ni lini atamuoa, Neema alipata ujauzito. Mambo yalikua mazuri Jeremy akionyesha upendo zaidi na kumjali, kitendo cha kuwa Baba mtarajiwa kilimfurahisha sana.
Bado walikua hawaishi pamoja, ingawa Neema alitamani iwe hivyo lakini kila siku Jeremy alikataa akimuambia itakua vizuri kama wakiishi pamoja baada ya ndoa na si kabla ya hapo. Neema hakuona sababu kwani muda mwingi walikua pamoja hasa nyumbani kwa Neema ambapo Jeremy alipenda kwenda, kula na mara nyingi kulala huko huko.
Pamoja na hayo hakutaka kumharakisha hivyo alivumilia mpaka pale atakapokua tayari. Jumamosi moja Neema akiwa kazini alianza kujisikia vibaya, ilikua ni mchana na kwakua muda wa kutoka kazini ulikua unakaribia aliomba ruhusa na kuruhusiwa kuondoka. Alimpigia simu Jeremy ili kumuambia kuwa hajisikii vizuri na anataka kwenda Hospitalini lakini simu haikupokelewa.
.. Malizia unahisi nini kilitokea?
🤔🤔😭😭😭