Wewe mpenda usiyependwa njoo hapa

Wewe mpenda usiyependwa njoo hapa

Dr Dre

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2015
Posts
2,669
Reaction score
2,859
USIMPE MOYO WAKO MTU ASIYEJALI HISIA ZAKO
Kila simu upige wewe na akipokea mkiongea sekunde kadhaa utamsikia “Ngoja nitakucheki baadaye” kisha anakata simu halafu hakutafuti mpaka umtafute wewe.
Kila siku yuko bize kuonana na wewe mpaka anapokuhitaji anapokuwa na shida flani ambyao anataka umsaidie au umtimizie.
Yuko online lakini hajibu meseji zako ingawa anachat na marafiki zake.
Hawezi kuongozana na wewe wala kukusindikiza sehmu ila akikuhitaji anataka umsindikize, tena anakupa taarifa wakati anaondoka hata sio masaa kadhaa kabla na usipoenda ni lawama na matusi.
Hakujali kwa chochote hata kukutumia meseji umeamkaje lakini bado unajipendekeza kutuma mamia ya meseji. Unamatatizo gani? Unakasoro gani? Hembu acha kumpa moyo wako mtu ambaye hata hakuthamini na kukupa muda wake.
Sisemi akupende kama unavyompenda lakini angalau akujali kama mwanadamu, akupe hata muda wake kidogo. Mtu wa namna hiyo hata ukifanikiwa kuingia naye kwenye ndoa ni mabalaa tu unajitafutia, punguza kujipendekeza na kujishusha kana kwamba unamalori ya kasoro!
 
Duh kwel mapenz matam,
Ujue iyo ndo radha ya mapenzi mkuu,kuumizan ndo utam wake uo
 
Aiseeee
Mie napendwa bhanaa, nimepita tuu kuwasalimia
Bora unaejitambua na kuelew unapendwa ila kumbuka kumpenda pia anaekupenda .ujue wanawake shukran ndogo San ,unawez mjali kwa kumpa kila kitu ila cku ukishindwa kumnunulia vocha ndo utajua mwanamke ni nan katika ii dunia
 
Mi bora niachane nae,ni heri nikaumie mbele kwa mbele hukoo kuliko kuishi maisha uliyoelezea hapo juu

Ila pole ziwaendee kwa wanayoyaishi hayo
zimewafikia
 
Bora unaejitambua na kuelew unapendwa ila kumbuka kumpenda pia anaekupenda .ujue wanawake shukran ndogo San ,unawez mjali kwa kumpa kila kitu ila cku ukishindwa kumnunulia vocha ndo utajua mwanamke ni nan katika ii dunia
Utaachaje kujua ka wapendwa jamanii, halafu sio wanawake tu huwa Wanasema kosa moja hufuta mema tisini na kenda. Kama mtu hajali ni hajali tu awe mwanaume au mwanamke
 
Back
Top Bottom