Wewe mdada kama mtu humtaki mwambie ukweli

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
3,900
6,658
Wanawake hasa wadada, mnapotongozwa na Wanaume na kujibu; Nipo kwenye mahusiano huku ikiwa si kweli, haupo kwenye mahusiano yoyote; Upo unasikilizia kwa Mwanaume atakayekuja, ila jibu la nipo kwenye mahusiano, uwa kama njia rahisi kwenu ya kumkataa Mwanamume yule usiyempenda kwa sababu na vigezo unavyojua wewe wenyewe; Mbaya.

Kama Mtu humpendi ni bora umwambie kweli na akitaka kujua sababu za kwa nini hutaki, humtaki au humpendi; Mpe sababu zote zilizopelekea umkatae au ukatae; Sababu zako ziwe za kweli ili iwe home work kwakeyeye kujichunguza na kuzifanyiakazi sabubu zilizo ndani ya uwezo wake, zilizopelekea wewe umkatae ili asije kukataliwa tena na mwingine kwa sababu hizohizo; Mbaya Sana. Sikutaki Sababu ni mchafu, unanuka kikwapa; Si hivyo tu' anaelewa au?

Yanini upate dhambi na kufunga milango yako ya mahusiano kwa kusema uongo. Nipo kwenye mahusiano kumbe uongo! So?

Kumbuka kinywa chako pia kinauwezo wa kujiloga ju ya Hatima yako mwenyewe!
 
Tatizo sio wao tatizo ni wewe, gentleman ukitongoza mara 1 jibu lolote atalokupa mwanamke liheshimu huwezi jua amekusitiri kiasi gani, achana nae fanya mambo yako wanawake ni wengi sana.

Mwanamke akikupenda wala hupati tabu naye.
Kwa hiyo jibu la kwanza akikuambia kuwa yupo kwenye relation, unatakiwa umuache si ndiyo?
 
Usijejidanganya kuna mwanamke yuko singo au ana mpenzi mmoja
Kama adam alikuwa mwanaume pekee duniani na bado eve akachepuka wewe ni nani upone😂😂😂
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom