Wenzetu wana marais sisi tuna Kikwete

Kamende

JF-Expert Member
Mar 1, 2008
416
45
Wakuu
Amani iwe kwenu.

Nimelazimika kuandika ukweli huu kwamba huko duniani ( katika nchi nyinginezo) wana marais ambao wananchi wao wakikumbwa na dhahama wanawajulia hali na kuwafikia mara moja. Wenzetu hao wana marais ambao maofisa wa serikali wakiboronga wanawajibishwa mara moja. Wenzetu wana marais ambao kama serikali ikifanya kosa la kugharimu maisha ya watu itaomba radhi hadharani. Kwa wenzetu wezi walioiba kikubwa ( km ilivyo kwa EPA) wanaadhibiwa kwa kuanzia aliyeiba kingi kuliko wenzake. (just to mention but a few)

Yawezekana mna mengi zaidi ya kuchambua ukweli huu "WENZETU WANA MARAIS; SISI TUNA KIKWETE"
 
Huenda huyo ndiye tunayestahili kuwa naye, kwani hakuletwa kwetu kwa nguvu bali tulimchagua sisi wenyewe; angalu mwaka 2005-na hata mwaka 2010, kwani hakuna kati yetu aliyesimama kusema kuwa huyo si tulieyamchagua, kama wanavyofanya wenzetu.
 
Watanzania tulikosea wenyewe hakuna wa kumlaumu,kama ni hivyo tuandamene kumpinga kama wenzetu wa misri na tunisia
 
  1. ninacho fahamu kikwete hakuchaguliwa na wananchi 2010,bali mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ndio aliye mteua hivyo haikuwa ridhaa ya watanzania walio wengi matokeo yetu waliyachakachua
 
Wananchi Walimchagua Yeye na CCM; kwahiyo kama ni matatizo sasa ni Yeye na CCM wanatakiwa kutatua hayo matatizo
 
Amepewa dhamana na wananchi kwahiyo kama anaboronga usimlaumu yeye walaumu wapiga kura.

Ungesema labda wenzetu wana wapiga kura sisi tuna vilaza!
 
Umesema yeye anajua na ndiyo maana wala hajaenda kuwashukuru kwani anajua hawajampa kura 2010 wamempa makame Nae bila shaka amekwishashukuru tayari
 
Huenda huyo ndiye tunayestahili kuwa naye, kwani hakuletwa kwetu kwa nguvu bali tulimchagua sisi wenyewe; angalu mwaka 2005-na hata mwaka 2010, kwani hakuna kati yetu aliyesimama kusema kuwa huyo si tulieyamchagua, kama wanavyofanya wenzetu.

Nakubali tulimchagua KIKWETE kwa bahati mbaya sana mwaka 2005. Lakini kwa 2010, tume yetu ya uchaguzi ndiyo ilituchagulia na sheria za nchi haziruhusu kuishtaki tume ya uchaguzi wala kuhoji matokeo ya uchaguzi wa raisi mahakamani.

Sasa kwa mazingira hayo tufanyeje?
 
Kwenye tafsiri kwamba Rais ni kiongozi wa juu kabisa wa serikali na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote na chini ya katiba yetu ni "mungu mtu".
Hii inapaswa kuamini mbele ya rais hamna la kumshinda, ndio maana kwenye baadhi ya mifano Jk Nyerere ameonekana ni dikteta.
Sasa chini ya hayo yote kuwa kama yalivyo lakini bado tunahuyu mtu dhaifu, asiye na maono ya uongozi na pia wala haonekani kujali.
Naona kweli wenzetu wana marais wakati sisi tuna Kikwete.
Mtu anayepaswa kuwa rais kwa maana ya amechaguliwa kidemokrasia na watu wake waliomwamini, lakini hayupo tayari wala hawezi kubeba madaraka ya kirais na kiutumishi mkuu mbele ya waliomchagua, achilia mbali mamlaka yake mengine kikatiba.
Kweli tuna JK na sio rais kama wenzetu..............
 
Wakuu
Amani iwe kwenu.

Nimelazimika kuandika ukweli huu kwamba huko duniani ( katika nchi nyinginezo) wana marais ambao wananchi wao wakikumbwa na dhahama wanawajulia hali na kuwafikia mara moja. Wenzetu hao wana marais ambao maofisa wa serikali wakiboronga wanawajibishwa mara moja. Wenzetu wana marais ambao kama serikali ikifanya kosa la kugharimu maisha ya watu itaomba radhi hadharani. Kwa wenzetu wezi walioiba kikubwa ( km ilivyo kwa EPA) wanaadhibiwa kwa kuanzia aliyeiba kingi kuliko wenzake. (just to mention but a few)

Yawezekana mna mengi zaidi ya kuchambua ukweli huu "WENZETU WANA MARAIS; SISI TUNA KIKWETE"
heshima mbele mkuu!tunae bingwa wa kuchekacheka hata ktk mambo magumu.mzee wa kutalii,muasisi wa udini!ama kweli wenzetu wana MARAISI SISI TUNA JAKAYA!
 
Sisi tuna kilaza

Natamani hata tungekuwa na jina jingine linalomwelezea kali zaidi kuliko hili. His government is the most hopeless ever na yeye anaonekana hata hajali. Imefika mahali binafsi sielewi kazi ya serikali ni nini na kwanini tuendelee kulipa kodi kwani barabara zimejaa potholes (hapa Dar), hospitalini hakuna dawa na mama wajawazito wanajifungulia sakafuni, shule hazina waalimu wala madawati (nina uncle anasoma std 4 hapa dar, juzi nimegombana naye how come bag limechoka ndani ya mwezi mmoja akanieleza kumbe hilo ndio dawati lake, anakaa chini na kuandika juu ya bag kama dawati). Shule nyingi za Dar ni std 6 na 7 tu ndio wenye madawati. Nikiorodhesha matatizo hapa sitayamaliza lakini tuliowapa dhamana ya kutuongoza wako poa wanaona hamna shida.Natamani tupate solution ya kudumu ili tusijeruhusu tena mtu asiye na uwezo kuwa rais bila kujali anatoka chama gani.
 
Watanzania tunahitaji Mkono wa Mungu utusaidie.... watanzania wengi wamekata tamaa, na hawaoni mwelekeo.
 
Habari ndio hiyo, Hatuna Rais, Tuna mfalme, kazi yake ni kutembea tu na vingora na kutabasamu mbele ya kamera! Imekula kwetu!

Huenda huyo ndiye tunayestahili kuwa naye, kwani hakuletwa kwetu kwa nguvu bali tulimchagua sisi wenyewe; angalu mwaka 2005-na hata mwaka 2010, kwani hakuna kati yetu aliyesimama kusema kuwa huyo si tulieyamchagua, kama wanavyofanya wenzetu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom