Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,047
- 79,390
Hajambo wote!
1. Bado Niko Morogoro hapa kama nilivyowaambia.
2. Mwezi wa kumi na moja na kumi na mbili nilibahatika kutembelea Mkoa wa Arusha, Moshi Mjini, Babati mjini, Korogwe Mjini, Dodoma Mjini, Kahama Mjini, na Sasa nipo zangu hapa Morogoro.
3. Aiseeh! What goes on here?
4. Dec 31 nilifika hapa nikazurura weee. Kuanzia Bigwa mpaka Mjini. Mwaka mpya nikaamkia Nanenane nikarudi mpaka mafisa, Msamvu mpaka kihonda.
5. Morogoro mmetia fora. Haaa! Sio kwa Fremu zote hizi za Mikopo. Yaani Kila mtaa Kila barabara. Yaani unaweza ukakuta kwenye msururu wa fremu Saba zilizopangana ukaona ofisi za mikopo hata tatu.
6. Sasa nikataka kujua wanatoa mikopo kiasi gani.
7. Nikafika maeneo kama matano hivi tofauti. Matatu yalikuwa Kihonda, mawili yalikuwa mafisa.
8. Kwanza hakuna mkopo wa milioni moja. Mimi nimefika nilitaka mkopo wa angalau milioni mbili hivi. Nikaambiwa wao mikopo yao haizidi milioni moja.
9. Nikawauliza mikopo yenu ni kwaajili ya nini. Wakaniambia kwaajili ya biashara. Mmmh! Nikawaambia wanipe elimu kama biashara gani. Ambayo mtu atafanya kwa mkopo wa shilingi laki nne au laki mbili. Na riba yao imechangamka.
10. Wakawa wanababaika.
11. Dhamana ya mkopo wako ni Ghetto lako. Kitanda, kabati, godoro, na Tv. Kama unafriji sawa.
Mnakumbuka mwaka 2019 niliwahi andika asilimia kubwa ya nyumba na maghetto ya watanzania samani zake hazifiki milioni mbilli? Kuna watu wakanibishia hapa.
12. Maafisa mikopo wa Morogoro wao sababu ya kutotoa mikopo mikubwa mbali na mitaji Yao kuwa midogo lakini sababu nyingine ni wakopaji vitu wanavyoweka dhamana havina thamani kubwa unayofika milioni 2.
13. Bado najiuliza kwa nini mji huu wa Morogoro uwe na ofisi nyingi za mikopo kuliko Mji wowote Tanzania? Wana morogoro mpo hapa mnijibu.
14. Laki tatu au nne mtu atafanyia biashara ipi ya kumtoa kwenye umaskini zaidi ya mkopo huo kumzamisha kwenye unmaskini mkubwa.
15. Mikopo hii inachangia kwa kiasi gani kuvunja mahusiano ya ndoa pale mambo yanapoenda swege mnege? Ingawaje hapa Morogoro vijana wake ambao wengi hujifikiri kama wajanja lakini wanawake wananguvu kuliko wanaume. Yaani upande wa ujombani.
16. Katika miji yote niliyoipita ukiwepo Dar. Mji wa Morogoro unatatizo la vibaka wavunjaji wa maduka ya watu.
17. Serikali na vyombo vya ulinzi umejipangaje kudhibiti matukio ya uhalifu wa wizi wa kuvunja maduka na fremu unaoendelea katika mji wa Morogoro.
18. Je itumike Ile mbinu ya kupiga chuma za kichwa kama ilivyotumika kule Dar kwa panya road?
Unajua Dar Kule kwa SASA uvunjaji wa maduka na wizi mdogomdogo umepungua.
Mtaa ninaoishi watu wanaacha nguo kwenye kamba usiku kucha. Mwaka wa nne sijawahi sikia mtu yeyote kaibiwa iwe ni nyumbani au dukani.
19. Morogoro nimefika hata sina Siku mbili. Taarifa nazopata ni hizo.
Baadhi ya maduka ya watu ninaowajua likiwepo moja na dadaangu yalivunjwa miezi kadhaa nyuma. Jambo ambalo niliposikia lilinishangaza kwani Nina Siku nyingi sijasikia taarifa za namna hiyo.
20. Kazi kwenu Wana morogoro kunipa ABC za mnafaidikaje na mikopo midogo kiasi hiki na ambayo imejaa mitaa karibu yote.
21. Hofu Yangu ni msije mkaathirika kisaikolojia na kujenga utamaduni mpya wa mikopo. Tena Mikopo ya kujikimu sio kujikwamua kimaisha
TaikonMaster
Kwa sasa Morogoro