Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,260
Nimeshuhudia sehemu nyingi za kuuza vyakula au vinywaji wakiwa hawazingatii kabisa kanuni za usafi, na sio kwa sababu wanafanya makusudi bali kwa sababu ya uelewa mdogo.
Haya ndiyo niliyoshudia kwenye migahwa, mama ntilie na Bar
1. Wakati wa kunawa mikono kabla ya kula usitegemee upewe sabuni ya kunawa ila ukimaliza kula sabuni ya kunawa itatafutwa popote ilipo na kama haipo itaenda kununuliwa ukiisubiria! Hali hii inaonyesha wahudumu na wateja wengi hawajui kinyume chake ndio sahihi na kwamba ukinawa bila sabuni hujanawa umejipaka maji tu kwenye uchafu wa mikono.
2. Nimeshuhudia wahudumu wakitumia majagi au mabakuli wanayonawishia wateja baada ya maji kuisha kuchotea maji mengine ambayo wanawanawishia wateja wengine.Nimeshuhudia pia ndoo inayotumika kukingia maji ya kunawia ikichotea maji yanayotumika kunawia mikono tena.
3. Nimeshuhudia maji waliyonawai wateja yakitumika kuoshea vitambaa vya kufuta meza za wateja kuwekea chakula.
Haya ni mambo yanayofanyika na wateja na wahudumu mara nyingi sio kwa sababu maji ni machache au hakuna sabuni bali kwa sababu ya ujinga wa kutofahamu nini umuhimu na jinsi ya kunawa mikono kwa usahihi kabla ya kula na mazingira ya ujumla ya usafi wa chakula.