Wenye vyeti feki kulipwa mafao yao..

Wenye vyeti feki kulipwa mafao yao..

Mmmmmh! Kuwaamini sisiemu ni kama kuota mabawa kwa binadamu. Siamini hadi nione wanawalipa.
 
Hapo they will wait and wait wabunge wa Awamu ya Saba ndo watakua wanauliza Maswali kuhusu Watumishi hewa wa awamu ya 5.
 
Katika vitu wanakosea ni kuwalipa mafao hao wezi.

Baada ya kilio kikuu kuhusu hatima ya maisha ya watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki hivyo kuondolewa kazini, hatimae serikali imekisikia na inaandaa mpango wa kuwalipa watumishi hao kwa kuwa wamehudumu katika nafasi mbalimbali serikalini kwa muda mrefu, Waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Angellah Kairuki ameeleza hayo kwa kuthamini michango ya watumishi hao.

Aidha Katibu Mkuu Utumishi Dr Laurean Ndumbaro anategemea kutangaza matokeo ya rufaa ya watumishi waliokata rufaa dhidi ya vyeti feki sambamba na kutangaza majina ya watumishi wengine wa serikali kuu wenye vyeti feki ifikapo tarehe 15.5.2017 siku ya jumatatu.

Chanzo: Gazeti Uhuru
 
Huruma iliyobora ni kuwapa chance warudi darasani QT watafute vyeti halali, halafu baada ya hapo qualifications zao nyingine zitambulike kuwa ni halali!. otherwise hawa wameshakuwa condemned to a very tough psychological torture!

Kipindi cha Mkapa wale walimu wazee wa UPE walipigwa presha warudi shule kama wanataka kuendelea na ualimu au Wapigwe chini, basi wale wazee walikomaa na shule na kuna waliofanikiwa kupata qualifications, kwa hiyo na hawa wenye vyeti feki wakipewa choice ya kurudi shule au kutumbuliwa naamini watarudi shule na watapata credits tu.

Mbona wahalifu wengine hawapewi unafuu huo?
 
Tumeshasema mapema. Wanajua wazi wamekosea. Wanajaribu kuwashawishi hao watumishi waondoke kimya kimya. Ningekuwa mimi sikubaki mpaka tupelekane mahakamani. Tangu lini serikali ikawa mahakama ya kuhukumu criminal offenses??
 
Shida iko wapi kwani?? Toeni pongezi kwa huu uamuzi basi sio kitu kuponda na kulalamika tu
Hakuna cha pongezi, wanatakiwa waende mahakamani ili wakapate haki zao. Wanatishwa bure. Watu wanaua lkn wanafikishwa Mahakamani ije kuwa vyeti feki? Tena nani amesema wakienda Mahakamani ni lazima wapatikane na hatia? Acheni kuwatisha bure.
 
Acha kutetea ujinga. Unajua watu wangapi wasio na pesa ya kununua cheti au kufoji wamekosa kazi sababu ya hawa watu?? Kuwa upinzani haimaanishi basi upinge kila kitu. Hii clean up ni muhimu sana na inatengeneza standards kwenye elimu yetu ili watu wawe serious shule
 
Kwa kuwalipa mafao na kututangazia feki wa serikali kuu na ipongeza sana serikali kwani inaanza kuleta imani kuwa hakuna aliye na vyeti feki atasalia
 
Baada ya kilio kikuu kuhusu hatima ya maisha ya watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki hivyo kuondolewa kazini, hatimae serikali imekisikia na inaandaa mpango wa kuwalipa watumishi hao kwa kuwa wamehudumu katika nafasi mbalimbali serikalini kwa muda mrefu, Waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Angellah Kairuki ameeleza hayo kwa kuthamini michango ya watumishi hao.

Aidha Katibu Mkuu Utumishi Dr Laurean Ndumbaro anategemea kutangaza matokeo ya rufaa ya watumishi waliokata rufaa dhidi ya vyeti feki sambamba na kutangaza majina ya watumishi wengine wa serikali kuu wenye vyeti feki ifikapo tarehe 15.5.2017 siku ya jumatatu.

Chanzo: Gazeti Uhuru
Hii ndio maana ya uongozi. Rais ni kama baba au mama hata kama mwanao ni mtukutu kiasi gani huwezi muua au kumuacha afe njaa wakati uwezo wa kumpa chakula unao. Rais kaonyesha ubinadamu wa hali ya juu sana. Huu ni mfano wa kuigwa
 
Huruma iliyobora ni kuwapa chance warudi darasani QT watafute vyeti halali, halafu baada ya hapo qualifications zao nyingine zitambulike kuwa ni halali!. otherwise hawa wameshakuwa condemned to a very tough psychological torture!

Kipindi cha Mkapa wale walimu wazee wa UPE walipigwa presha warudi shule kama wanataka kuendelea na ualimu au Wapigwe chini, basi wale wazee walikomaa na shule na kuna waliofanikiwa kupata qualifications, kwa hiyo na hawa wenye vyeti feki wakipewa choice ya kurudi shule au kutumbuliwa naamini watarudi shule na watapata credits tu.
Hayo ni mawazo ya busara sana kama serekali inathamini mchango wa watu hawa kwenye utumishi wao, ni vizuri ingeamua kuwarudisha kazini kisha wapewe muda wa miaka 3 ili warudi shule kutafuta vyeti halali. Kuwalipa mafao ni kupoteza fedha za serekali bila kutumia akili, kwa kuwa wakosaji wakubwa ni waajiri waliowafanyia usaili na kuwapa barua za confirmation baada ya kuwaona wanafaa kwa ajira.
 
Nadhani hii ni njia nzuri sana ya ku-handle jambo hili. Kuna mtu namfahamu alikuwa miongoni mwa top brain wakati akichukua Masters yake, na isitoshe Serikali imempeleka nje mara kadhaa na hata sasa hivi yuko nje ya nchi na huko alipo ni lulu, kwa ifupi yuko serious na anaijua kazi. Unfortunately, jina lake nimeliona miongoni mwa waliogushi cheti cha form four. Definitely plan ya namna hii inaweza kuliokoa taifa kupoteza brain za namna hii.
Pia yupo Doctor mmoja wa pale Muhimbili, aliokoa maisha ya ndugu yangu kwani alimfanyia operesheni ya Figo na sasa ndugu yangu amepona anaendelea na shuli zake kama kawaida. Imeniuma sana nilipoona jina lake kwani alikuwa hata ukimpigia simu usiku alikuwa anatuelekeza cha kufanya juu ya mgonjwa na kiukweli alikuwa na customer service nzuri kuliko wengine tuliowakuta pale.
 
Na hatuwezi kusema hao walikuwa wabaya zaidi ya wale walioihujumu nchi yetu kwa kuiingiza kwenye mikataba mibovu na kujilimbikizia utajiri kwenye mabenki ya ughaibuni, ingefaa nao wangeshughulikiwa ipasavyo
Hayo yanaitwa makaburi kaka ,alafu awaguswi
 
labda 2020 uchaguzi ukiwadia vinginevyo wanaweza kuwa kama wale wazee wastaafu wa Jumuiya ya AAfrika Mashariki.
Ndugu unaakili sana ndo kitakachowatokea hawa watu nyetfek yaani hapo wanafarjiwa tu yatakuwa kama wale Wa east Africa, tena hawa hata kuandamana watashndwa, wale wazee pomoja na kuandamana huishia patupu!
 
Back
Top Bottom