comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Watumishi waliobainika na vyeti feki, watalazimika kusubiri mafao yao hadi utaratibu wa kuwalipa utakapofanyika.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki alitoa kauli hiyo jana bungeni wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Amina Mollel.
Amina alitaka kujua ni hatua gani zitachukuliwa ili kuwalipa mafao yao wafanyakazi waliobainika na vyeti feki.
Waziri Kairuki alisema, ofisi yake itaandaa utaratibu wa mafao ya wafanyakazi hao na pindi utakapokamilika, watajulishwa na kulipwa haki zao, kauli hiyo imekuja baada ya kilio kikuu kuhusu hatima ya maisha ya watumishi waliobainika kuwa na vyeti feki hivyo kuondolewa kazini, hatimae serikali imekisikia na inaandaa mpango wa kuwalipa watumishi hao kwa kuwa wamehudumu katika nafasi mbalimbali serikalini kwa muda mrefu, Waziri ofisi ya Rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Angellah Kairuki ameeleza hayo kwa kuthamini michango ya watumishi hao.
Aidha Katibu Mkuu Utumishi Dr Laurean Ndumbaro anategemea kutangaza matokeo ya rufaa ya watumishi waliokata rufaa dhidi ya vyeti feki sambamba na kutangaza majina ya watumishi wengine wa serikali kuu wenye vyeti feki ifikapo tarehe 15.5.2017 siku ya jumatatu
Chanzo: Gazeti Uhuru