Wenye viwanda watishia kuvifunga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye viwanda watishia kuvifunga

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Rutashubanyuma, Jan 22, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  Wenye viwanda watishia kuvifunga Friday, 21 January 2011 19:53

  Raymond Kaminyoge
  WAMILIKI wa viwanda nchini, wametishia kufunga viwanda vyao kutokana na gharama kubwa za uendeshaji zinazotokana na mgao wa umeme unaoendelea.

  Walisema hayo jijini Dar es Salaam jana, kwenye mkutano wa wadau wa viwanda ulioandaliwa na Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), ili kutoa mapendekezo kwa serikali jinsi wanavyoweza kupata umeme wa uhakika.

  Walisema zaidi ya asilimia 30 ya gharama zote za uzalishaji kwenye viwanda, zinatumika kulipia umeme.

  “Hali ni mbaya, umeme umekuwa tatizo sugu nchi hii, kwa wiki zaidi ya saa 30 viwanda havifanyi kazi kwa sababu hakuna umeme, tutajiendeshaje wakati muda wote huo hatuzalishi,” alisema Arfil Kumar wa Kiwanda cha Kutengeneza Mabati cha Alaf.

  Kumar alisema asilimia 14 ya Watanzania ndio waliounganishwa na umeme wa gridi ya taifa, waliosalia hawana nishati hiyo.

  “Cha kushangaza ni kwamba licha ya idadi ndogo ya Watanzania wanaotumia umeme wa Tanesco, umeme wanaupata kwa mgao, asilimia 85 ya Watanzania wataunganishwa vipi umeme hakuna?” alihoji Kumar.

  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Uchumi, Jehovanes Aikael, alisema alitembelea viwanda 60 mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Tanga, Kilimanjaro, Iringa na Mwanza na kufanya mahojiano na wamiliki.


  Aikael alisema kwenye mahojiano hayo, alibaini kwamba mgao wa umeme ni tatizo kubwa tofauti na inavyoonekana.
  Alisema hata pale umeme unapopatikana, wenye viwanda hivyo walimweleza kuwa, haukuwa na nguvu ya kuendesha mitambo.

  “Kwa hiyo kutokuwa na umeme wa uhakika ni kikwazo kikubwa kwa wawekezaji wa viwanda, kwani wanashindwa kufikia malengo yao waliyojiwekea,” alisema.

  Alisema baadhi ya wenye viwanda wanaonyesha kukata tamaa kutokana mitambo yao kutofanya kazi kwa kukosa umeme, licha ya kuinunua kwa gharama kubwa.

  Kwa upande wake, Juma Isevya, mmiliki wa kiwanda cha kusindika maziwa, alisema serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka ili umeme wa uhakika uweze kupatikana.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 22, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 414,921
  Trophy Points: 280
  Hata mkifunga kazi.............who cares but yourself.........................................wakati wa uchaguzi mlishabikia na kukidhamini chama cha mafisadi sasa vuneni mlichopanda.............................................
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 22, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,267
  Likes Received: 19,409
  Trophy Points: 280
  kura mliwapigia wenyewe na cha kusnagaza kwenye sherehe yao ya ccm utawaona watu kibao na t shirt na kanga za ccm wakipiga makofi na kushangilia ilihali nyumbani wameacha giza.
   
 4. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #4
  Jan 22, 2011
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Hivi unafikiri huwa wanachangia kwa kupenda? Ile ni biashara kama zilivyo biashara zingine. Kuna ambao waliwekeza sana kwa Lyatonga Mrema mwaka 1995 matokeo yake wakafulia.

  Unatambua ya kwamba nature ya industries zetu ni labour intensive, sasa hii inaweza isikuguse wewe moja moja ila wenye mali wakiamua kufunga viwanda vyao inamaanisha kuna familia zitakosa mikate yao ya kila siku. Hawa nao watakula wapi?

  Matatizo ya umeme yameathiri kila mtu hapa Tanzania ukiondoa labda wale kwenye mtandao wa juu wa uongozi na wale wenye fedha za kumwaga za kununua na kuyawasha majenereta, solar panels na labda wenye nishati ya samadi. Cha msingi ni kutafuta suluhisho la kudumu la matatizo haya na pia kuwawajibisha wazembe wa Tanesco na wizara husika kwa kuanza na kuwatimua kazi na hata kuwafungulia mashtaka wakurugenzi wakuu wa kipindi hiki na vya nyuma na pia hata hao waliowahi kushika wizara.
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kweli, si walichangia chama ili kishinde kiwasaidie baada ya uchaguzi, wakakililie huku huko!
   
 6. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #6
  Jan 22, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Nadhani umefanya vema kuwakumbusha. Kwani nchi hii inajari hata tukifunga viwanda vyote. Inahuuu??
   
 7. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #7
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  tuna hasira ndio lakini inapofikia kwenye masuala ya uchumi kama hayo ujue waathirika ni nchi nzima ingawa Unaweza usione impacts zake direct.
  Kilio chao ni kilio chetu pia kwa namna moja au nyingine.
   
 8. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #8
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Sasa hvi hata zile mbwembwe za ngeleja sizisikii amekaa kimya maana alivyokuwa ana bwabwaja
   
 9. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #9
  Jan 22, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Inauma sana na inatia hasira
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Jan 22, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  pole mkuu, punguza usije ukajitia kitanzi bure tukukose.
   
 11. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #11
  Jan 23, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  WATANZANIA NI WANGAPI HADI SASA (2005 - 2010) WENYE MAISHA BORA NA HADI HIVI SASA (2010 -2015) WAO WANAJIBIDISHA TU KUTAFUTA KIADA CHAKE NCHINI????

  Watanzania wenzangu tuambizane ukweli hapa na tusifichane hali halisi ndani ya mifuko yetu. Mpaka hivi sasa wengi wetu HATUZUNGUMZII TENAUCHUMI wa maisha yetuTanzania bali hali halisi ni UCHUMA wa maisha yetu nchini. Je, wewe????

  Baya zaidi, ajabu ninayoiona nkule bado CCM na JOPO LA MAFISADI wangependa Watanzania wote tukaseme tu YOTE NI MAISHA na kukimbilia kitanndani, baada kucheka na Masanja TBC, huku CC ya CCM wakibariki Dowans walimpwe.

  Huku waliosbobea katika uchumi nchini wanatutahadharisha KIAMA DOWANS WAKILIPWA na kuongeza kuongeza kwamba tunachoona mpaka sasa kwa gharama ya maisha eti hapo bado ni mwanzo tu wa mapinduzi ya sinema nzima wa ahadi ya Maisha BORA ZAIDI kwa kila Mtanzania; na katika kutimiza hilo Mhe Kikwete na CCM wametuhakikishia dhamira zao za kutufikisha huko kwa Nguvu Zaidi, Ari Zaidi na Kasi Zaidi.

  Sasa Mtu endapo utakuwa hauoni MAISHA BORA ZAIDI basi wala usisubiri kuambiwa na mtu, Wenye kuona UGUMU ZAIDI KWA KILA NAFSI YAKE huyu si Mtanzania tena maana WATANZANIA WOTE waliopata ahadi hizo tangu siku nyingi tu (2005 - 2010) maisha yao ni bora kabisa hivi sasa (2010 - 2015) wanacho kitafu kiukweli ni Uziada wa UBORA HUO WA MAISHA.
  HOJA YANGU:

  Kwa mantki hiyo Mhe Kikwete na CCM, watu wa Takwimu nchini acheni kutu fikicha ukweli, Watanzania ni wastani wa watu wangapi nchini maana hili la watu milioni 46 wala sihitaji tafsiri ya mtaalamu kubani kwamba si kweli.
   
 12. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #12
  Jan 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  vwanda vikfungwa,bidhaa ztapungua sokoni,bei itapanda,na hela hakuna ya kununua,ITS PAIN
   
 13. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #13
  Jan 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mambo mengine acha tu unaingia cost mara tatu zaidi kwasababu ya kutokuwa na umeme
   
 14. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #14
  Jan 23, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Ngoja waje wagome, ila sijui bwana aarrghhhhh!!!!!
   
Loading...