Wenye uelewa Mdogo wa Lugha ya Kiingereza wameshaunda Neno Linalotumiwa kwa kasi sana.

SHIEKA

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
8,244
4,258
Nikiwa mtumiaji mkubwa wa usafiri wa daladala mkoani Kilimanjaro nilianza kulisikia hili neno likitumiwa sana na makondakta wa daladala. Nilisikia sana usemi huu: "Haya, panda fasta wale wa Kwa Sadala, Boma mpaka Sanya. Fanya fasta!"Hii ilikuwa mwanzo mwa miaka ya 2000 - 2002 - 2005 hivi.Nikawaza: eee! hiyo fasta ndo ana maana gani? Kwa nini asiseme tu "panda haraka?" Nikajua hawa watu wanataka kuonesha kuwa hata wao ung'eng'e upo! Sasa hivi hili neno fasta limeshamiri sana kila mahali - hata hapa JF hutumiwa sana. Si la Kiswahili wala kiingereza ila kwa kweli ni kiingereza kibovu - tena sana. Maneno 'haraka' au 'upesi' yameshapewa likizo na neno fasta kuingia kazini! Mimi naona huu ndio mwanzo wa kuua lugha yetu ya Kiswahili. Au mwaonaje wadau?
 
Kawaida ya lugha ni kwamba huwa ziko hai - zinakua. Katika kukua hukopa/kutohoa maneno ya lugha nyingine. Kwa bahati mbaya mara nyingine hata lugha inapokuwa na neno mwafaka tayari kama katika mfano ulioutoa, bado maneno mapya huzuka na hatimaye kukubalika. Sio rahisi kuzuia tabia hii ya lugha.
 
Kawaida ya lugha ni kwamba huwa ziko hai - zinakua. Katika kukua hukopa/kutohoa maneno ya lugha nyingine. Kwa bahati mbaya mara nyingine hata lugha inapokwa na neno mwafaka tayari kama katika mfano ulioutoa, bado maneno mapya huzuka na hatimaye kukubalika. Sio rahisi kuzuia tabia hii ya lugha.
Ni kweli kabisa usemavyo ndugu pmwasyoke. Lakini kinachonishangaza kwa nini sisi waelewa tunaingia kwenye mkumbo huu wa kutumia maneno ambayo ni 'lugha mbovu?eg 'Njoo hapa fasta' Au hii ifuatayo ninayoisikia mara nyingi sana: 'Kuwa care tafadhali' Hiyo si kutohoa wala nini, ni uelewa mdogo unahalalishwa. Afadhali hii ambayo nayo inatumika sana: 'Yule dada ninamfeel ile mbaya'
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kabisa usemavyo ndugu pmwasyoke. Lakini kinachonishangaza kwa nini sisi waelewa tunaingia kwenye mkumbo huu wa kutumia maneno ambayo ni 'lugha mbovu?eg 'Njoo hapa fasta' Au hii ifuatayo ninayoisikia mara nyingi sana: 'Kuwa care tafadhali' Hiyo si kutohoa wala nini, ni uelewa mdogo unahalalishwa. Afadhali hii ambayo nayo inatumika sana: 'Yule dada ninamfeel ile mbaya'

Nadhani watu wengi wana silika ya kudhania kuchanganya maneno ya kigeni katika Kiswahili (au katika lugha zao nyingine) inaashiria ujuaji. Hili linajengeka hadi hata bila kudhamiria tunatumia Kiswanglish. Hii hutuathiri hata sisi tuliobahatika kusoma kwa kiwango kikubwa kulinganisha na wananchi wengi. Ukisikiliza majadliano mbalimbali bungeni, vyuoni, katika vyombo vya habari, kwenye mabaa, n.k. utushuhudia ugonjwa huu. Ndiyo hali halisi na Kiswahili kinapokea tu maneno yanayoingizwa bila sababu na yanayoingizwa kwa sababu. Naamini lugha nyingine pia hukumbwa na suala hili.
 
Back
Top Bottom