Sehemu ya Hotuba ya Mwenyekitu wa CCM, Rais Alo Hassan Mwinyi wakati akizungumza na wazee wa Chama, Viongozi wa Taifa,
Mashirika ya UMMA na watu binafsi juu ya ufafanuzi wa maamuzi ya Halmashauri kuu ya Taifa katika kikao chake cha Zanzibar:
Diamond Jubilee Dar es Salaam, Tarehe 25/2/1991
Inasomeka hivi:
Mfano kuna mwananchi mmoja alikwenda kwenye kiwanda cha Umma kutaka huduma ya kusafishiwa ngozi zake. Alipofika hapo alikuta pamelala paka Yaani palikuwa kimya, hapakuwa na kazi yoyote inayofanyika. Kumbe kile kiwanda kilikuwa kimefungwa kwa kukosekana fedha za kukiendeshea ........... umeme ulikatwa na wafanyakazi walipewa likizo.
Meneja alimfahamisha huyo mteja kuwa kiwanda kimefungwa kwa sababu ya deni la maji na umeme pamoja na pesa za mishahara ya wafanyakazi. Huyo mteja alikubali kulipa arubuni (advance ) ya milioni saba ili kukikwamua kiwanda. Wiki ya pili yake kiwanda kilianza kufanya kazi zake za kuzalisha kama kawaida.
Kisa cha kiwanda hicho kusimama kazi ni kukosa fedha za kuendeshea. Kiswahili cha siku hizi huitwa ukwasi. Kwa hiyo kazi ilisimama.
Katika hali kama hii, tumeona ni vyema kuwaruhusu wananchi wote pamoja na wakulima, na wafanyakazi wa shirika lenyewe wakiwemo wanachama wa CCM kununua hisa chache kwa kila atakaetaka
Swali
Mfanyabiashara huyu wa Ngozi ni nani zaidi ya Rostamu???
heckton chuwa na flora temba, moshi
waziri mkuu mstaafu, bw. Cleopa msuya, amesema serikali haikulifuta azimio la arusha na kubadilishana na lile la zanzibar, bali hayo ni mawazo ya wachache waliokuwa na tamaa ya kunyakua mali ya umma.
Bw. Msuya alitoa kauli hiyo juzi wakati wa mahafali ya kumi ya kidato cha nne ya shule ya sekondari ya mt. Maria goreti ya mjini moshi, mkoani kilimanjarokwa mujibu wa katiba ya tanzania na kusisitiza kuwa, siasa ya tanzania bado ni ya ujamaa na kujitegemea.
mimi nilikuwa kwenye kile kikao cha zanzibar, tulichokubaliana kuwa kulingana na mabadiliko yaliyokuwepo wakati huo, mtu akiweza kujiingizia kipato kwa njia ya halali afanye hivyo ili mradi azingatie maadili mema na sio kuliua azimio la arusha, alisema.
Alisema lengo lilikuwa ni kupotosha wale waliokuwa na tafsiri mbaya kuhusu azimio la arusha kwa kuwa ilifikia wakati mtu akifuga kuku ishirini, thelatini au hata mia moja ni sawa lakini akiwa na kuku zaidi ya mia mbili tena wa halali anaitwa kabaila jambo ambali alisema ilikuwa ni tafsri potofu ya azimio la arusha.
lakini wachache wenye uchu wa kunyakua mali ya umma wakaanza kufanya hivyo kwa kisingizio cha kikao kile cha zanzibar huku wakitafsiri maazimio ya kikao kile visivyo ili kuhalalisha tamaa zao, alisema.
Aliongeza: wananchi watashinda vita dhidi ya ufisadi kuwa bado wanalitaka azimio la arusha na ndio maana mnaona kwenye vyombo vya habari kila siku watu wakipambana na wavamizi wa ardhi na mali nyingine za umma.
Kuhusu dhana kuwa watanzania wanaogopa shirikisho la afrika mashariki, bw. Msuya alisema dhana hiyo si kweli na kwamba ukweli ni kwamba watanzania wanafuatilia suala hilo kwa umakini kutokana na hadhi na heshima ya tanzania kimataifa.
sisi hatuogopi shirikisho bali tunachukua tahadhari na umakini mkubwa, lengo letu ni kuwa maamuzi yetu yasije kutuunganisha na matatizo ya wengine, alisema.
Alisema kuwa kuna baadhi ya wanachama wa jumuiya ya afrika mashariki ambao bado hali zao kiusalama bado si nzuri na ndio sababu ya hadhari ya tanzania na kwamba si vyema tanzania ikaacha utaifa wake na kujiunga shirikisho bila ya kuwa na hadhari juu ya hali yake ya baadaye.
ushauri wangu ni kwamba tuimarishe eneo la biashara kwanza miongoni mwa mataifa yetu ya afrika mashariki na ndipo tufikirie ushirikiano wa kisiasa, alisema.
"Wananchi watashinda vita dhidi ya ufisadi kuwa bado wanalitaka Azimio la Arusha na ndio maana mnaona kwenye vyombo vya habari kila siku watu wakipambana na wavamizi wa ardhi na mali nyingine za umma".
Narudia!.....mtu yoyote mwenye azimio la Zanzibar naomba anionyeshe au aniambie ni maktaba gani nitalipata hilo azimio,au website gani?...was it official?..how?
Duh mkuu mbona unafanya uvivu kutafuta? haya BofyaNarudia!.....mtu yoyote mwenye azimio la Zanzibar naomba anionyeshe au aniambie ni maktaba gani nitalipata hilo azimio,au website gani?...was it official?..how?
Mkuu mimi nakuheshimu sana, naomba tusileteane mambo ya kihuni. Lile si azimio, si official declaration of anything. Uliyonielekeza ni makala ya mtu wa kawaida tu kama mimi.Duh mkuu mbona unafanya uvivu kutafuta? haya Bofya
Mkuu mimi nakuheshimu sana, naomba tusileteane mambo ya kihuni. Lile si azimio, si official declaration of anything. Uliyonielekeza ni makala ya mtu wa kawaida tu kama mimi.
Kwa heshima na taadhima naomba nilione azimio la Zanzibar mnalolizungumzia!..liko wapi?
Angalau articles of Union zipo wazi(but I really don't care about Zanzibar).Naomba hilo azimio linyeshwe au watu waache kulizungumzia....ni uwongo uliokithiri.Hutaweza kulipata kwani limefanywa SIRI kama mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Mbona mkali hivyo! mkuu nimepitia haraka Google nikaona hiyo kama haikupeleki kwenye Azimio la Zanzibar basi haijawa tatizo naomba isome hotuba ya Mwinyi hapa au bado ni uhuni?..BofyaMkuu mimi nakuheshimu sana, naomba tusileteane mambo ya kihuni. Lile si azimio, si official declaration of anything. Uliyonielekeza ni makala ya mtu wa kawaida tu kama mimi.
Kwa heshima na taadhima naomba nilione azimio la Zanzibar mnalolizungumzia!..liko wapi?
Bwana hilo Azimio lilikuwa kimeo halikuandikwa hata huyo Mzee CD hana copy yake, anaongea tu ndio maana kila mtu analitafsiri anavyoona inamfaa yeyeNaomba copy ya azimio hilo.