Wenye uchu walipotosha Azimio la Z'bar - Msuya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenye uchu walipotosha Azimio la Z'bar - Msuya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=3][/h]

  Heckton Chuwa na Flora Temba, Moshi

  WAZIRI Mkuu mstaafu, Bw. Cleopa Msuya, amesema serikali haikulifuta Azimio la Arusha na kubadilishana na lile la Zanzibar, bali hayo ni mawazo ya wachache waliokuwa na
  tamaa ya kunyakua mali ya umma.

  Bw. Msuya alitoa kauli hiyo juzi wakati wa mahafali ya kumi ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari ya Mt. Maria Goreti ya mjini Moshi, mkoani Kilimanjarokwa mujibu wa Katiba ya Tanzania na kusisitiza kuwa, siasa ya Tanzania bado ni ya Ujamaa na Kujitegemea.

  “Mimi nilikuwa kwenye kile kikao cha Zanzibar, tulichokubaliana kuwa kulingana na mabadiliko yaliyokuwepo wakati huo, mtu akiweza kujiingizia kipato kwa njia ya halali afanye hivyo ili mradi azingatie maadili mema na sio kuliua Azimio la Arusha”, alisema.

  Alisema lengo lilikuwa ni kupotosha wale waliokuwa na tafsiri mbaya kuhusu Azimio la Arusha kwa kuwa ilifikia wakati mtu akifuga kuku ishirini, thelatini au hata mia moja ni sawa lakini akiwa na kuku zaidi ya mia mbili tena wa halali anaitwa kabaila jambo ambali alisema ilikuwa ni tafsri potofu ya Azimio la Arusha.

  “Lakini wachache wenye uchu wa kunyakua mali ya umma wakaanza kufanya hivyo kwa kisingizio cha kikao kile cha Zanzibar huku wakitafsiri maazimio ya kikao kile visivyo ili kuhalalisha tamaa zao”, alisema.

  Aliongeza: “Wananchi watashinda vita dhidi ya ufisadi kuwa bado wanalitaka Azimio la Arusha na ndio maana mnaona kwenye vyombo vya habari kila siku watu wakipambana na wavamizi wa ardhi na mali nyingine za umma”.

  Kuhusu dhana kuwa Watanzania wanaogopa Shirikisho la Afrika Mashariki, Bw. Msuya alisema dhana hiyo si kweli na kwamba ukweli ni kwamba watanzania wanafuatilia suala hilo kwa umakini kutokana na hadhi na heshima ya Tanzania kimataifa.

  “Sisi hatuogopi shirikisho bali tunachukua tahadhari na umakini mkubwa, lengo letu ni kuwa maamuzi yetu yasije kutuunganisha na matatizo ya wengine”, alisema.

  Alisema kuwa kuna baadhi ya wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao bado hali zao kiusalama bado si nzuri na ndio sababu ya hadhari ya Tanzania na kwamba si vyema Tanzania ikaacha utaifa wake na kujiunga shirikisho bila ya kuwa na hadhari juu ya hali yake ya baadaye.

  “Ushauri wangu ni kwamba tuimarishe eneo la biashara kwanza miongoni mwa mataifa yetu ya Afrika Mashariki na ndipo tufikirie ushirikiano wa kisiasa”, alisema.
   
 2. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sehemu ya Hotuba ya Mwenyekitu wa CCM, Rais Alo Hassan Mwinyi wakati akizungumza na wazee wa Chama, Viongozi wa Taifa,
  Mashirika ya UMMA na watu binafsi juu ya ufafanuzi wa maamuzi ya Halmashauri kuu ya Taifa katika kikao chake cha Zanzibar:
  Diamond Jubilee Dar es Salaam, Tarehe 25/2/1991
  Inasomeka hivi:

  Mfano kuna mwananchi mmoja alikwenda kwenye kiwanda cha Umma kutaka huduma ya kusafishiwa ngozi zake. Alipofika hapo alikuta "pamelala paka" Yaani palikuwa kimya, hapakuwa na kazi yoyote inayofanyika. Kumbe kile kiwanda kilikuwa kimefungwa kwa kukosekana fedha za kukiendeshea ........... umeme ulikatwa na wafanyakazi walipewa likizo.

  Meneja alimfahamisha huyo mteja kuwa kiwanda kimefungwa kwa sababu ya deni la maji na umeme pamoja na pesa za mishahara ya wafanyakazi. Huyo mteja alikubali kulipa arubuni (advance ) ya milioni saba ili kukikwamua kiwanda. Wiki ya pili yake kiwanda kilianza kufanya kazi zake za kuzalisha kama kawaida.

  Kisa cha kiwanda hicho kusimama kazi ni kukosa fedha za kuendeshea. Kiswahili cha siku hizi huitwa ukwasi. Kwa hiyo kazi ilisimama.

  Katika hali kama hii, tumeona ni vyema kuwaruhusu wananchi wote pamoja na wakulima, na wafanyakazi wa shirika lenyewe wakiwemo wanachama wa CCM kununua hisa chache kwa kila atakaetaka

  Swali
  Mfanyabiashara huyu wa Ngozi ni nani zaidi ya Rostamu???
   
 3. J

  JAY2da4 JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 11, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Taifa kwanza wewe ni kichwa kwa kweli,si mwingine ndo huyo.Ufisadi haukuanza leo,haya mambo yalianzia kwa Mwinyi.
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Sasa Huo Ukwasi Umetufikisha Wapi? Umezidisha Ulafi kwa Viongozi Wetu
   
 5. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  . . . Tunahitaji Azimio Jipya!
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Sep 2, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Azimio la Arusha mwisho wake ulikuwa CHUMBE. Halikufika Zanzibar.

  Hongera Karume 1
   
 7. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mzee Msuya, wenye vipato halali siyo matajiri wa mali. Ukiwa tajiri hasa wa mali, ni hekaheka mtindo mmoja.
   
 8. p

  politiki JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kama kawaida ya viongozi hawa wakiwa hasa kwenye power hawasemi kitu leo upo nje and you are no more effective ndio unapiga kelele wakati ulikuwa waziri mkuu ungeweza kufanya mengi kubadilisha hali hiyo swali langu kwako wewe kama msuya ulichukua jitihada gani wakati ulipokuwa na uwezo wa kufanya hivyo kubadilisha hali hiyo ???
   
 9. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  Naomba copy ya azimio hilo.
   
 10. kakomya

  kakomya Member

  #10
  Sep 3, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  It is long time now since such remarks could be heard from a former Nyerereian like Msuya. Many, including those who were long time Nyerere's political confidants like Kingunge, Mwinyi, Mkapa, to the incumbent Kikwete have since fallen off and have turned to be hegemonous bourgeoisie. The Arusha declaration, the declaration of humanity that CCM stalwarts celebrated its demise decades ago to pave way for their capitalistic ego is still spiritually alive in the hearts of many Tanzanians. The Tanzanian proletariat will eventually win the silent fight against the capitalists who have infected the york of the engine of our beloved humanistic declaration (CCM). The enemies of our beloved "Azimio" will perish and Tanzania will eventually regain its glorious past, this time not through the old, defunct and dilapidated CCM, but another movement that I believe will soon emerge to rekindle our lost hope.
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana tunafundishwa siku zote kuwa uongozi ni wito, na mtu hatafuti utajiri kwa kupitia uongozi, ingawa utajiri unaweza kumfuata mtu akiwa kiongozi kulingana na taratibu za nchi husikia, kama ilivyo kwa Malkia wa Uingereza

  Tanzania iliyoundwa kuanzia awamu ya pili hadi leo ni ile ya viongozi kutafuta utajiri. Mzee Ruksa alitengeneza matajiri wengi sana waliokuwa watumishi ndani ya serikali yake, na hadi leo kuna viongozi wengi sana wanaojijengea utajiri kutokana na nafasi zao serikalini. Hiyo iliwezekana tu kutokana na Azimioa la Zanzibar. Inawezekana Mwinyi mwenyewe hakujua madhara ya tamko lake lile kwa vile hakuwa amelichambua kwa kina, na hiyo ndiyo inayomwekea doa kubwa sana katika rekodi yake ingawa sera yake ya ruksa imeendelea kuwa maarufu kwa upande mwingine na kusababisha taifa tulilo nalo leo lisiwe na order ya kibishara bali MONEY SPEAKS.
   
 12. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  Narudia!.....mtu yoyote mwenye azimio la Zanzibar naomba anionyeshe au aniambie ni maktaba gani nitalipata hilo azimio,au website gani?...was it official?..how?
   
 13. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2011
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Kwa nini walichojadili Zanzibar walikifanya siri. Nani aliwakataza kukiandika kwa kukweka vitabuni tukisome.
   
 14. M

  Mkandara Verified User

  #14
  Sep 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh mkuu mbona unafanya uvivu kutafuta? haya Bofya
   
 15. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #15
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi nakuheshimu sana, naomba tusileteane mambo ya kihuni. Lile si azimio, si official declaration of anything. Uliyonielekeza ni makala ya mtu wa kawaida tu kama mimi.
  Kwa heshima na taadhima naomba nilione azimio la Zanzibar mnalolizungumzia!..liko wapi?
   
 16. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #16
  Sep 3, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0

  Hutaweza kulipata kwani limefanywa SIRI kama mkataba wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
   
 17. Kobello

  Kobello JF-Expert Member

  #17
  Sep 3, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 5,688
  Likes Received: 650
  Trophy Points: 280
  Angalau articles of Union zipo wazi(but I really don't care about Zanzibar).Naomba hilo azimio linyeshwe au watu waache kulizungumzia....ni uwongo uliokithiri.
  La Arusha lipo, la Zanzibar lipo wapi?
   
 18. M

  Mkandara Verified User

  #18
  Sep 3, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mbona mkali hivyo! mkuu nimepitia haraka Google nikaona hiyo kama haikupeleki kwenye Azimio la Zanzibar basi haijawa tatizo naomba isome hotuba ya Mwinyi hapa au bado ni uhuni?..Bofya
   
 19. F

  Falconer JF-Expert Member

  #19
  Sep 3, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Inasikitisha kuona wengi wenu muna ng'ang'ania siasa ya ujamaa wakati mwenyewe muasisi Julius K. Nyere alikiri kuwa amefeli baada ya jaribio la miaka 25 ya siasa hizo. Kwani kuna kosa gani Rostam kukiinua kiwanda ili walalahoi wapate ajira. ?. Acheni siasa za kumalizana. Rostam ni mwananchi kama wewe na mimi. Ana haki kuwa mmiliki kama yeyote yule. Alilokuwa amefanya kosa ni kutuzidi akili?. Mwacheni mfadhili mkuu aendelee na maisha yake.
   
 20. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #20
  Sep 3, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Bwana hilo Azimio lilikuwa kimeo halikuandikwa hata huyo Mzee CD hana copy yake, anaongea tu ndio maana kila mtu analitafsiri anavyoona inamfaa yeye
   
Loading...