Wenye Samsung Galaxy Note 7 watakiwa kuzizima

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
Samsung imetoa wito kwa watu wenye simu aina ya Galaxy Note 7 kuzizima mara moja huku ikifanya uchunguzi kubaini ni kwa nini simu hizo, hata zile ambazo kampuni hiyo ilikuwa imethibitisha kwamba ni salama, zinawaka moto.

Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema itasitisha uuzaji wote wa simu hizo.

Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.

Chanzo: BBC
 
image.jpeg

Simu ya Samsung Note 7 ilishika moto ikifanyiwa uchunguzi maabarani Singapore

Samsung imetoa wito kwa watu wenye simu aina ya Galaxy Note 7 kuzizima mara moja huku ikifanya uchunguzi kubaini ni kwa nini simu hizo, hata zile ambazo kampuni hiyo ilikuwa imethibitisha kwamba ni salama, zinawaka moto.

Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema itasitisha uuzaji wote wa simu hizo.

Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.Walipewa simu mpya ambazo zilidaiwa kuwa salama.

Kwa nini betri za Lithium hulipuka?
Lakini sasa taarifa zimetokea kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto.
Mwanamume mmoja jimbo la Kentucky, Marekani anasema aliamka na kupata chumba chake cha kulala kimejaa moshi uliotokana na simu mpya ya Note 7 aliyokuwa ameipata baada ya kurejesha ya awali.
Siku chache awali, abiria kwenye ndege moja Marekani walitakiwa kuondoka kwa dharura ndegeni baada ya simu ya Note 7 kuanza kutoa moshi.

Samsung imesitisha mauzo ya Galaxy Note 7
"Kwa sababu usalama wa wateja ni jambo tunalotilia maanani zaidi, Samsung itawataka wasambazaji wote na wauzaji wake kote duniani kusitisha uuzaji na pia ubadilishaji wa simu za Galaxy Note 7 uchunguzi unapoendelea," kampuni hiyo imesema.

"Wateja walio na simu asili za Galaxy Note 7 au simu za Galaxy Note 7 za kubadilisha, wanafaa kuzizima na kuacha kuzitumia na badala yake kutumia njia nyingine (kuendelea na shughuli zao)," kampuni hiyo imeongeza.

Ni watu wangapi wameathirika?
Samsung inasema simu zilizoathirika ni takriban 2.5 milioni. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, simu 45,000 za Note 7 zimeuzwa Ulaya, na sana Uingereza. Zaidi ya asilimia 75 zilikuwa zimebadilishwa na wamiliki wake wakapewa simu nyingine za Note 7 au mitambo mingine ya Samsung.

Samsung sasa itashindwa na Apple?
Galaxy Note 7 ilitarajiwa na Samsung kuisaidia kushindana na simu ya Apple iPhone 7. Lakini baada ya matatizo hayo, Samsung imeathirika pakubwa na hisa zake kushuka. Hisa za Apple upande mwingine zimepanda sana thamani. Aidha, nembo ya Samsung kama kampuni ya kuaminika imeathirika pakubwa.

Wakala wa kulinda wateja Marekani amewahimiza watu kutotumia simu za Samsung ambazo wamebadilishiwa.
Mwenyekiti wa usalama katika tume hiyo ya Elliot Kaye amesema uamuzi wa Samsung wa kuacha kuuza simu hizo ni wa busara.
Chanzo: BBC Swahili.
 
Dah mie ndiyo maana samsung siziamini.
 
Die hard fans wa Samsung hawakuelewi,tangu kitambo teknolojia ya utengenezwaji wa betri uliwashinda .
 
Kukiri kosa na kulitafutia uvumbuzi ni step nzuri katika kutatua mgogoro.La sivyo.Hii ingeweza kuwa kujichimbia kwa kaburi kwa brand ya Samsung.Kama nawaona vile Apple na washindani wengine..........
 
iphon + blackberry samsung watasubir sana
 
Niliwahi kuchangia hapa kuwa sina Imani na battery za Samsung. Nilishambuliwa na watu wengi wakitetea kuwa battery za Samsung ni imara
 
They have to feel the pinch, haraka ya nini? wenzio wanafanya research ya kutosha kabla ya kutoa toleo jipya. hii itawagharimu sana. samsung note 5 yangu ndio simu yangu ya mwisho ya samsung kuimiliki.
 
View attachment 415831

Simu ya Samsung Note 7 ilishika moto ikifanyiwa uchunguzi maabarani Singapore

Samsung imetoa wito kwa watu wenye simu aina ya Galaxy Note 7 kuzizima mara moja huku ikifanya uchunguzi kubaini ni kwa nini simu hizo, hata zile ambazo kampuni hiyo ilikuwa imethibitisha kwamba ni salama, zinawaka moto.

Kampuni hiyo ya Korea Kusini imesema itasitisha uuzaji wote wa simu hizo.

Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.Walipewa simu mpya ambazo zilidaiwa kuwa salama.

Kwa nini betri za Lithium hulipuka?
Lakini sasa taarifa zimetokea kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto.
Mwanamume mmoja jimbo la Kentucky, Marekani anasema aliamka na kupata chumba chake cha kulala kimejaa moshi uliotokana na simu mpya ya Note 7 aliyokuwa ameipata baada ya kurejesha ya awali.
Siku chache awali, abiria kwenye ndege moja Marekani walitakiwa kuondoka kwa dharura ndegeni baada ya simu ya Note 7 kuanza kutoa moshi.

Samsung imesitisha mauzo ya Galaxy Note 7
"Kwa sababu usalama wa wateja ni jambo tunalotilia maanani zaidi, Samsung itawataka wasambazaji wote na wauzaji wake kote duniani kusitisha uuzaji na pia ubadilishaji wa simu za Galaxy Note 7 uchunguzi unapoendelea," kampuni hiyo imesema.

"Wateja walio na simu asili za Galaxy Note 7 au simu za Galaxy Note 7 za kubadilisha, wanafaa kuzizima na kuacha kuzitumia na badala yake kutumia njia nyingine (kuendelea na shughuli zao)," kampuni hiyo imeongeza.

Ni watu wangapi wameathirika?
Samsung inasema simu zilizoathirika ni takriban 2.5 milioni. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, simu 45,000 za Note 7 zimeuzwa Ulaya, na sana Uingereza. Zaidi ya asilimia 75 zilikuwa zimebadilishwa na wamiliki wake wakapewa simu nyingine za Note 7 au mitambo mingine ya Samsung.

Samsung sasa itashindwa na Apple?
Galaxy Note 7 ilitarajiwa na Samsung kuisaidia kushindana na simu ya Apple iPhone 7. Lakini baada ya matatizo hayo, Samsung imeathirika pakubwa na hisa zake kushuka. Hisa za Apple upande mwingine zimepanda sana thamani. Aidha, nembo ya Samsung kama kampuni ya kuaminika imeathirika pakubwa.

Wakala wa kulinda wateja Marekani amewahimiza watu kutotumia simu za Samsung ambazo wamebadilishiwa.
Mwenyekiti wa usalama katika tume hiyo ya Elliot Kaye amesema uamuzi wa Samsung wa kuacha kuuza simu hizo ni wa busara.
Chanzo: BBC Swahili.
No doubt, system hackeb by rivals
 
Hapa tecno tu,ninyi endeleeni na simu zenu za kitajiri za Samsung
 
Siwaliambiwa wazirudishe sasa maswara ya kuzma yanatoka wp au ni hile kiendacho kwa mganga hakirudi
 
Sijawai ziamini simu zao ingawa watu wanazipenda ......

Nokia ilipopitwa na wakati ....

Nikaamina kwa Techno mobile....
 
ingekuwa tecno zetu ungesikia mijimaneno hapaaaaa,simu zao zimepatwa na majanga kimiyaaaaaaaaaa,anyway,poleni mlionunua vimeo vya bei kubwa halafu vinawapasua kichwa
 
Mi nina samsung galaxy note 8 ila made in vietnam....ila imejizima ghafla juzi.
 
HEHEHEHHEEH naona watu wa Tecno wamepata mahali pa kujificha ili kujustify umiliki wao wa tecno. hehehhee ni sawa na kusema ''mi ndomana sipendagi kabisa ferrari,bora nibaki na hii kirikuu yangu.'' anyway mi nina nokia ya tochi kabisa yani.
 
Back
Top Bottom