Wenye nyumba wameanza makeke !

Wenye nyumba wameanza makeke !

SUPER BRAND

Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
8
Reaction score
0
Salaam wana jf,

Mwaka 2015 iwe isiwe lazima na mimi nipate kibanda changu cha kujisitiri na familia yangu maana tusio na nyumba sometimes naona kama tunyanyasika!!

Hivi juzi juzi jobmate mwenzangu alipoteza mke na mtoto katika ajali ya bus huko Musoma,na mmoja ya waliokuwepo kwenye msiba huo ni baba mwenye nyumba anapoishi.

Jamaa alienda kumzika mkewe upareni na alirudi jana na leo amekuja job.Wakati tunaendelea kumpa pole za hapa na pale!! .Simu yake iliita na alikwenda kuongelea pembeni.Aliporudi alitueleza mzee mwenye nyumba anataka kodi yake siku ya tarehe 01 saa mbili sharp bila kukosa na awali alikuwa alikuwa analipa kwa miezi sita sita but mzee kamwambia kwa tarehe hiyo alipe ya mwaka na kama hataweza tarehe 2 January ahame!

My take: sikatai jamaa kulipa kodi kwa kipindi hicho but ni vema wenye nyumba mkawa na busara ya kumvumilia kidogo mtu hata apumzike kidogo then ndo umweleze.Kufiwa na mke na mtoto mara moja si jambo dogo na pia kitendo cha kupandisha miezi ya kulipia bila taarifa ya miezi mitatu pia si ustaarabu.

Tiririkeni waungwana.
 
Daah...we acha tu. Wenyu nyumba wengine ni kero wana 'joto' kushinda Jahannam
 
Taarifa Za Mabadiriko Zitolewe Miezi Mitatu Kabla
Mpangaji Kama Hajaridhia Ana Haki Ya Kutoingia Mkataba Mpya

suala La Mwenye Nyumba Kudai Chake Ingawa Mpangaji Ana Huzuni Ya Kufiwa....Huo Ni Uamuzi Wake Binafsi Yeye Mwenye Nyumba
Kama Anafata Mkataba, Mwenye Nyumba Haimfungi Kwa Lolote
Hauna Haja Ya Kumpangia Mda Wa Kudai Pesa Yake
suala La Msiba Haliingiliani Na Utaratibu Wa Malipo
Ahsante Jigo
 
sasa kilichompeleka msibani ni nini kama si kutaka kuonekana tu machoni mwa watu wakati moyoni hana hata chembe ya ubinadamu
 
Unaweza ukawa unaishi na mchawi ila ukachukua muda sana kujua hilo.

Huyo mzee ni mchawi.

Kwa Nini Umtuhum Uchawi Wakati Anadai Chake
Si Vizuri Hivyo, Acheni Lawama Zisizo Na Mantiki
Kama Anafata Mkataba, Alipwe Pesa Yake.....Nasema Alipwe Chake
Ahsante Jigo
 
Serikali ifanye haraka kuleta sheria ya kuwatoza kodi wenye nyumba za kupangisha. Tra na mwigulu mpo?. Kakusanyeni kodi kwenye nymba hizo kwani kodi ya chumba ni sh.50000 hadi 60000/= kwa chumba cha hadhi ya chini.
 
Serikali ifanye haraka kuleta sheria ya kuwatoza kodi wenye nyumba za kupangisha. Tra na mwigulu mpo?. Kakusanyeni kodi kwenye nymba hizo kwani kodi ya chumba ni sh.50000 hadi 60000/= kwa chumba cha hadhi ya chini.

serikali ipi?
kama ni Tanzania je sheria zipo?
 
Kwa Nini Umtuhum Uchawi Wakati Anadai Chake
Si Vizuri Hivyo, Acheni Lawama Zisizo Na Mantiki
Kama Anafata Mkataba, Alipwe Pesa Yake.....Nasema Alipwe Chake
Ahsante Jigo



Mchawi ni mtu yeyote asiye na utu nafsini mwake.

Hivi mfano-una kijana wako umempa piki piki awe anakuletea elfu kumi kila siku,ikatokea bahati mbaya akafiwa na mwanae.utakomaa siku hizo zote za msiba akupe pesa yako!!!!

Bila shaka inawezekana sababu-
*piki piki ni yako.
*kafiwa yeye wewe haikuhusu.
*unachotaka wewe ni kutimiza ndoto zako na si kingine.

Faza hauzi,ana mamlaka yooooooooote ya kudai hela yake,nyumba si yake bwana,na asishtakiwe popote.

Ila sababu matatizo hayana mwenyewe,tunahimizana katika kutendeana utu.

Imagine,kaomba hela hiyo alafu akapewa yote,siku akipata tatizo si watu watamuangalia tu!!.
 
Pole sana kaka kwa huo msiba mzito ..daaah!!! hakyanani.., yaan pole tu.., Mungu amekuandalia vinono hapo mbeleni...
 
Salaam wana jf.mwaka 2015 iwe isiwe lazima na mimi nipate kibanda changu cha kujisitiri na familia yangu!! maana tusio na nyumba sometimes naona kama tunyanyasika!! hivi juzi juzi jobmate mwenzangu alipoteza mke na mtoto katika ajali ya bus huko musoma,na mmoja ya waliokuwepo kwenye msiba huo ni baba mwenye nyumba anapoishi,jamaa alienda kumzika mkewe upareni na alirudi jana na leo amekuja job.wakati tunaendelea kumpa pole za hapa na pale!! .Simu yake iliita na alikwenda kuongelea pembeni.aliporudi alitueleza mzee mwenye nyumba anataka kodi yake siku ya tarehe 01 saa mbili sharp bila kukosa na awali alikuwa alikuwa analipa kwa miezi sita sita but mzee kamwambia kwa tarehe hiyo alipe ya mwaka na kama hataweza tarehe 2 january ahame!!!

Nb.my take .sikatai jamaa kulipa kodi kwa kipindi hicho but ni vema wenye nyumba mkawa na busara ya kumvumilia kidogo mtu hata apumzike kidogo then ndo umweleze.kufiwa na mke na mtoto mara moja si jambo dogo.na pia kitendo cha kupandisha miezi ya kulipia bila taarifa ya miezi mitatu pia si ustaarabu.tiririkeni waungwana

Hongera kwa nia uliyotia ya kuhamia kwako.

Mwanaume ni Nyumba na sio magari. Vijana tulio wengi tuwaoga sana wakujenga nyumba na tunakimbilia sana vitu vya anasa wakati uwezo wetu bado uko chini.

kijana kapata kazi anachukua mkopo benk ananunua gari cc2000 anakokaa hadi anakofanyia kazi daily mafuta ya 15(15x30=450000/=) halafu kila jambo la anasa hataki kubaki nyuma. kijana wa sampuli hii hawezi kujenga ataishia kuhama hama.

Na wenye shida sana na sie tuliotokea familia masikini tukisha pata kazi huwa hatujikubali kama tumetoka familia masikini tunaanza kuishi kama nasie ni watoto wa bakhresa
 
Ilitakiwa mwenye nyumba atoe taarifa miezi 3 mbele kwamba next mtataba itakuwa mwaka na Si ghafra Kama alivyofanya,suala la msiba na ulipaji kodi havina uhusiano..mpe pole jamaa yetu,ndiyo changamoto hizo ajipange ajenge yake...
 
Duuuh pole sanaaaa aiseee nyumba za kupanga ni shida kuna mkuu wangu alihamia nyumba yake ikiwa bado haija isha kutokana na kero za mama mwenye nyumba ila alifanikiwa kumaliza aiseee wana jf tupambane sana tuwe na makazi yetu pia.kupanga ni kero kubwa sanaaaa
 
Itabidi nitafute kazi ya ulinzi maana hizi kodi sasa tunakomoana........mzee asubuhi naamkia mzigoni na naelekea mzigoni baada miaka kumi nitakuwa nimeshajenga ya kwangu hata kama kibada poa tu.....
 
Na je, ni haki mwenye nyumba kuongeza kodi ya sh. 10000 kila mwaka wakati hakuna kilichokarabatiwa kwenye chumba hicho kwa miaka minne iliyopita?. Na kama si haki, ni hatua gani zinastahili kuchukuliwa?. Usiniambie nihame.
 
Daah...we acha tu. Wenyu nyumba wengine ni kero wana 'joto' kushinda Jahannam

Tatizo linakuja pale mwenye nyumba aliishi kwenye mbavu za mmbwa enzi hizo halafu aje jenga kibanda mjini basi ataona ndio mwisho bila yeye mjini hukai maneno mbofumbofu kibao halafu wana kale kamtindo kabovu ka kila mwaka wanakupa notes kodi imepanda kutokana na gharama za uendeshaji hapo ndio napochokaga kabisaa wakati nyumba ya mwaka wa sabini rangi haieleweki ukija kwenye swala la choo hapo ndio majanga mimi naona bora nao walipe kodi manake wanafanya biashara nyumba zenyewe mbovuuu.
 
Wamenifurahisha wenye nyumba ninayokaa. Walidai kodi kwa msisitizo na kuomba kabla sijamaliza mkataba, nimewapa pesa haoo wakaenda kuchezea ngoma. Actually kodi yetu haiwasaidii zaidi ya mwezi mmoja, baada ya hapo wanarudia shida zao
 
Back
Top Bottom