Wenye nguvu ni wananchi. Hakuna jeshi la kiongozi, wenye jeshi ni wananchi

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
KUTOKA SUDAN; DUNIA HAINA RAIS MWENYE NGUVU, INA RAIS MAARUFU!

WATAFITI kwa majibu yao, utasikia Donald Trump, Vladimir Putin na Xi Jinping kuwa ni viongozi wenye msuli mkubwa duniani. Ngoja nikwambie; dunia haijawahi kuwa na kiongozi mwenye nguvu. Sema kiongozi huongoza taifa lenye nguvu.

Baada ya Omar al-Bashir kuangukia pua Sudan jana, huu ni uthibitisho mwingine; Hakuna kiongozi mwenye nguvu. Kuna kiongozi maarufu. Al-Bashir alikuwa kiongozi maarufu. Dunia, hasa Afrika aliogopwa. Aliaminika ni kiongozi mwenye nguvu. Kumbe hakuwa na lolote. Jeuri yake ilikuwa ni wananchi.

Inabidi unielewe; hakuna powerful leader (kiongozi mwenye nguvu). Wala hakuna strong leader (kiongozi imara). Kuna popular leader (kiongozi anayependwa) na unpopular leader (kiongozi asiyependwa). Vilevile kuna famous leader (kiongozi maarufu) na infamous leader (kiongozi muovu au kiongozi kituko). Ipate hii uzuri.

Akina Muammar Gaddafi, Robert Mugabe, Hosni Mubarak na wengine wengine, walionekana viongozi wenye nguvu na imara, lakini wananchi walipoamua, waling'oka kiurahisi. Jeuri ya kiongozi ni utulivu wa wananchi. Hajawahi kutokea kiongozi mwenye nguvu kuzidi wananchi waliomkataa.

Al-Bashir alitakiwa muda mrefu The Hague ili ajibu mashitaka ya mauaji ya kimbari Darfur, lakini hawakumpata. Alioneka ni imara sana. Wananchi walipoamua, miezi miwili kang'oka. Umma unapoamua, kiongozi ambaye hudhaniwa ni mwenye nguvu, hugeuka mwepesi kuliko unyoya!

Kuna viongozi hudhani wao wana nguvu. Kumbe nguvu zao ni wananchi. Kiongozi ukipendwa na wananchi wewe ni salama. Ukichukiwa, haupo salama. Kiongozi mwenye akili huwekeza upendo kwa watu ili awe salama. Kiongozi mjinga huwekeza nguvu kwenye jeshi, eti wamlinde. Jeshi halijawahi kumtii kiongozi dhidi ya wananchi wanaoamua.

Nchi ni jeshi. Na jeshi ni wananchi. Muda ambao wananchi hubadilika, ndio hapo jeshi humgeuka kiongozi ili matakwa ya wananchi yatimie. Jeshi limemgeuka Al-Bashir kama lilivyowageuka akina Mugabe, Mubarak, Ben Ali, Bouteflika na wengineo.

Kanuni ni hii; hakuna kiongozi mwenye nguvu, wenye nguvu ni wananchi. Hakuna jeshi la kiongozi, wenye jeshi ni wananchi.

Ndimi Luqman MALOTO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajeshi au Mapolisi wametoka kwa wananchi...wana Dada zao, Kaka zao, Baba Zao, shangazi zao, wajomba zao, mama mkwe, baba mkwe, shemeji etc

Upofu wa watawala ndio hujidanganya kuwa unaweza kutumia Polisi kupiga shangazi zao, au kipigo cha mbwa koko, au kupigwa hadi kuchakaa..au kulazimisha gesi itoke mtwara JWTZ - Ni vitendo vya muda mfupi tuu

Iko siku polisi/mwanajeshi atasikia ndugu yake au mama yake kanyanyaswa na Jeshi au polisi....eee maeneo fulani na yeye yko mkoa fulani, nae anapewa amri apige, ua....Formula itagoma.

Maandamano yanayogusa Taifa zima, maana yake jamii nzima inaguswa..hata ndugu za wanajeshi/Polisi watamwagiwa maji ya kuwasha...Je wataendelea kutii?

Kinachoshindikana Tanzania ni kuwa maandamano yanakuwa ni ya mkoa mmoja tu, au mji mmoja...na Wananchi kukosa elimu/muamko wa kujua sababu ya maandamano...Kwa Tanzania bado, hasa itokee Uchumi mbaya....

Watch out..Uchumi wa tanzania umeshuka hadi % we not far from there...
 
Back
Top Bottom