Wenye mafuta wagoma tena

Wenye mafuta wagoma tena

rushanju

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
3,327
Reaction score
5,599
Kwa wenye mikweche kama mimi wenye kuweka lita mojamoja nawashauri mtakapoona mafuta kwenye petrol station popote tafadhali weka mafuta ya kutosha maana vituo vyote tayari wameishaanza kugomea kuuza mafuta. Nimekwenda kununu mafta kwenye petrol station moja wamesema kwamba haiwezekani kununua zaidi ya lita kumi. Na vituo vingi wamekataa au wamegoma kabisa kuuza mafuta kwamba mafta yameisha.
 
Pumbavu zao, tatizo wenye vituo vya mafuta wameiweka EWURA mfukoni
 
Wanatest ili kuona kama serikali watakuwa wapole kama walivyofanya last time. This time hakuna udhaifu tutafungia vituo vyote chezea JK..
 
sio ewura tu imewekwa mifukoni mwa wauza mafuta bali serikali nzima na watanzania wote
 
Pumbavu zao, tatizo wenye vituo vya mafuta wameiweka EWURA mfukoni

Mnajua nchi ina mafuta kiasi gani mpaka kuanza kutukana hivyo? Jamani hakuna mafuta kabisa na sio kwamba makampuni ya mafuta yamegoma. Muulize Bulk Procurement Coordination Company imekuwaje mafuta yanayoagizwa na makampuni yauzayo mafuta hayaletwi nchini na sio kutukana bila kuwa na data.
 
sasa yule bwana msemaji wa EWURA alikua anaongea nini siku ile???asee ngoja nikacheki ndo nitaamini hii nchi kiboko
 
Kwa wenye mikweche kama mimi wenye kuweka lita mojamoja nawashauri mtakapoona mafuta kwenye petrol station popote tafadhali weka mafuta ya kutosha maana vituo vyote tayari wameishaanza kugomea kuuza mafuta. Nimekwenda kununu mafta kwenye petrol station moja wamesema kwamba haiwezekani kununua zaidi ya lita kumi. Na vituo vingi wamekataa au wamegoma kabisa kuuza mafuta kwamba mafta yameisha.

Nchii hii bana.. hata hapa morogoro stores (iliyokuwa BP filling station) wamegoma. Ndo tatizo la akili ndogo kuongoza akili kubwa. Ilitakiwa mamlaka husika kutoa adhabu kali ili iwe mfano na mambo ya migomo ya wauza mafuta iwe historia...Kuleana na kuchekeana kwingi nchi hii..
 
Mnajua nchi ina mafuta kiasi gani mpaka kuanza kutukana hivyo? Jamani hakuna mafuta kabisa na sio kwamba makampuni ya mafuta yamegoma. Muulize Bulk Procurement Coordination Company imekuwaje mafuta yanayoagizwa na makampuni yauzayo mafuta hayaletwi nchini na sio kutukana bila kuwa na data.

Na wewe mwenye data badala ya kuziweka hapa watu wakaelewa unaishia kulalamika na kulaumu...hili Taifa lina matatizo gani? Mlalamikaji anajibiwa kwa kulalamikiwa...
 
Wanatest ili kuona kama serikali watakuwa wapole kama walivyofanya last time. This time hakuna udhaifu tutafungia vituo vyote chezea JK..

Unaamanisha JK huyu huyu presidaa? Amebadilika lini na kuanza kuchukua hatua?
Halafu umeongea kama wewe ndiyo msemaji wa hii serikali dhaifu ya JK.
 
Na wewe mwenye data badala ya kuziweka hapa watu wakaelewa unaishia kulalamika na kulaumu...hili Taifa lina matatizo gani? Mlalamikaji anajibiwa kwa kulalamikiwa...

Hakuna mgomo wa mafuta....mafuta yaliyopo hayatoshi kwa mahitaji ya soko la ndani sababu uagizaji wa mafuta hauendani na matumizi. Mafuta yaliyoagizwa miezi kadhaa nyuma ndio yameshushwa wiki iliyopita I think...na mengine yatakuja next month if am not mistaken. Hilo sio tatizo la wauza mafuta maana utaratibu wa sasa, muagizaji wa mafuta ni ile kampuni iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria kuwezesha bulk procurement.
 
Wakigoma tunatia kiberiti vituo vyao tukose wote
 
jana nimepita vituo viwili kimoja karibu na jengo la tcra na kingine ubungo.
Vyote havina mafuta, nimeenda kupata kituo cha puma maeneo ya kimara.
Nilihisi tu kutakuwa na tatizo.
Jamaa wanataka bei ipandishwe ndo wauze.
 
Mi nilijua tu kwa hii bei hatuwezi kudumu nayo hata wiki 2. maana ingekuwa juu hata miezi miwili fresh tu kwa EWURA NA WEZI WENZIWE.
 
Back
Top Bottom