Wenye kutakiwa kuogopwa kama ukoma bado wapo na malengo yao ya siri hayawezi kufa upesi.

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,487
13,612
Maneno yaliyosemwa miaka 22 iliyopita kule Mbeya bado yanaishi. Siku ya Mei Mosi ambapo Taifa lilipewa onyo la kuepuka kununuliwa na fedha ambazo vyanzo vyake havijulikani.

Onyo la siku ile linakihusu mpaka kizazi cha Tanzania ya kesho. Onyo lile linaendelea kutufundisha maana ya kuishi ndani ya mipaka ya fedha halali.

Ni onyo ambalo halitaweza kupoteza maana iliyokusudiwa, maadam mwanadamu anayelisikiliza, anayo akili ya kulielewa na kujifunza namna linavyoweza kuyafaa maisha yake.

Siku zote mtu huacha kumbukizi (legacy) kwa namna ambavyo anagusa hisia za watu. Na kuweza kuzigusa hisia za watu ni lazima mtu afanane na anachokiongea.

Mwaka 1995 Watanzania tulionywa juu ya madhara ya kutonunulika kwa sababu ya tamaa za maisha haya mafupi. Aliyetuonya alifariki mwaka 1999, lakini mwaka 2015 na kabla ya hapo tukawa mashahidi wa namna ambavyo tamaa zetu zinavyoweza kutuingiza mkenge.

Wale ambao tulionywa kuwa tuwaepuke kadri tuwezavyo bado wapo, fedha zao bado zipo. Sababu zenye kuweza kuhalalisha malengo yao yaliyojificha, bado zipi na tunayo masikio ya kuweza kuzisikia.

Ole wetu basi, tukiamua kwenda kinyume na mafunzo tuliyopewa katika hali ya upendo mkubwa wa kibinadamu.

Tunaweza kubadilisha katiba na vifungu vyake, tunaweza kubadilisha mfumo wa upatikanaji wa tume ya uchaguzi.

Lakini hatuwezi hata siku moja kulibadilisha lengo la mtumiaji fedha kila sehemu kwa nia tu ya kuwa kiongozi, mpaka likawa ni jema kwetu.

Na haina maana kwamba haya yanayopigiwa kelele yakishaweza kuwa yametimizwa, basi na lengo ovu lenye kujificha ndani ya tabasamu la wanasiasa, linaweza kubadilika ghafla na likawa jema kwa kila Mtanzania.

Ubinafsi ndio chanzo cha maovu mengi, hata kama mbinafsi anao watu wenye ufundi mkubwa wa kumfanya aonekane ni mnyenyekevu wa kiwango cha kimataifa.

Tunapoimba wimbo wa Taifa, tumuombe Mungu pia atuepishe na udhaifu wa kuweza kutekwa na mvuto wa fedha, ambazo hatuna uhakika kama sio sumu kwetu.
 
Back
Top Bottom