Wenye haraka

BABA JUICE

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
426
225
Jamaa watatu walikufa wakaenda mbinguni walipofika geti la mbinguni wakakuta foleni kama ya dar,malaika akasema leo tunapokea wenye haraka na waliokufa kifo cha kutisha na cha huzuni kwahiyo nasikiliza story zenu,wakwanza akaja nakuanza kuadithia alivyokufa....mimi nina mke mzuri sana,nilihisi kwamba anatembea na mwanaume mwingine nikienda kazini basi nikaamua kumzuga naenda kazini,nilichukua kama masaa matatu na kurudi ikabidi nipande ngazi kwani tulikuwa tunaishi gorofa ya nane,nipofika ndani nikaisi kuna harufu ya manukato ya kiume..nikamuuliza mke wangu yukuapi huyo mwanaume...nikatafuta ndani kote lakini sikumuona mtu kwasababu ya hasira ikabidi nitoke kwenye kibaraza cha gorofa kupunga upepo....nipotoka nikamuona mwanaume amevaa kaptulaa ananinginia nikamponda vidole hadi akaanguka..bahati mbaya akaangukia kwenye mti..kwahasira nikaenda ndani nikaschukua friza nikamtupia akaanguka nalo hadi chini akafa..na mimi presha ikapanda hapo hapo nikafa...hiyo ndio hadithi ya kifo changu..malaika akampa pole akamuita mwingine.Wapili akaja nakuanza...mimi ni mpishi huwa naingia kazini mchana,siku ya kifo changu nikuwa nafanya mazoezi katika kibaraza ya gorofa ya saba huku nashikilia gorofa ya nane..alikuja mtu na kuanza kuniponda vidole vyangu kwa bahati mzuri niliangukia mti..muda si muda akaja na friza akanibonda nalo nikaanguka hadi chini na kufa na sasa nipo hapa...malaika akampa pole...akaita mwingine watatu...mmi sina kazi nilikuwa natembea na mke wa mtu mume wake akaja nikaingia kwenye friza ndio nipo hapa sijui nimefikaje!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom