Wenje atishia kwa bastola kikaoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wenje atishia kwa bastola kikaoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FIDIVIN, Mar 21, 2012.

 1. FIDIVIN

  FIDIVIN Senior Member

  #1
  Mar 21, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni ktk kikao cha CDM Mwanza chini ya uenyekiti wa Dr Slaa.

  Source: Habari
  MBUNGE wa Nyamagana, Ezekia Wenje (Chadema), ameingia matatani baada ya kudaiwa kumtishia mtu kwa bastola katika kikao cha ndani cha chama hicho.

  Wenje, ambaye amekanusha madai hayo, anadaiwa kufanya kitendo hicho katika mkutano wa Kamati ya Utendaji ya wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela, Jumamosi, Mwanza chini ya uenyekiti wa Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.

  Hata hivyo, alikiri jana kuwa na bastola kwenye mkutano huo akidai muda wote aliiweka kiunoni.

  Wenje anadaiwa kufanya kitendo hicho kwa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Ilemela, Robert Gwanchele baada ya kushindwa kuelewana kikaoni.

  “Katika purukushani hizo, Mbunge wa Viti Maalumu, ndiye aliyenusuru hali baada ya kuipiga kumbo silaha hiyo na kusababisha Wenje adondoke chini na kupata maumivu usoni, na mlengwa wa silaha hiyo kupata upenyo na kuchoropoka,” kilidai chanzo cha habari.

  Wenje alipoulizwa kwa njia ya simu kuhusu tuhuma hizo jana, alikana kumtishia mtu kwa bastola kwenye mkutano huo na kuhusisha madai hayo na masuala ya migogoro ya kisiasa ndani ya chama hicho.

  “Kwanza sikuwa na sababu yoyote ya kutishia mtu bastola ingawa kweli inawezekana ni peke yangu niliyekuwa na silaha hiyo kwenye mkutano huo … hakubishana nami sasa ningeanzia wapi? Yeye alibishana na Dk Slaa,” alidai Wenje.

  Akisimulia tukio lilivyokuwa, Wenje alisema: “Ilikuwa Jumamosi kwenye kikao cha ndani cha chama kilichoongozwa na Dk Slaa, kabla hatujaanza, vijana wawili si wajumbe wa kikao waliingia, Dk Slaa akaamuru watoke, wa kwanza akatoka na wa pili akagoma.

  “Aliyetoka kwanza ni Deus Litaragula wa Nyamagana na wa pili nilimtambua kwa jina moja la Gwanchere kutoka Ilemela, huyu aligoma kutoka, mimi nilikuwa nimekaa kwa mbele, watu wa nyuma alikokuwa huyu kijana wakaanza kumtoa kwa nguvu, ikazuka purukushani na kusukumana,” alisema Wenje.

  Alidai kuwa alinyanyuka kwenda kusaidia kumtoa kijana huyo ili mkutano uendelee na kwa kuwa ilikuwa usiku, mtu wa kwanza kumtambua katika purukushani ya kumtoa nje kijana huyo ni Naibu Meya wa Mwanza, Charles Chibela.

  Kwa mujibu wa Wenje, Litaragula kabla ya kupoteza sifa za kuhudhuria kikao cha Kamati ya Utendaji ya wilaya hizo mbili, alikuwa Katibu Mwenezi wa Chadema wa Wilaya ya Nyamagana, lakini hakujua nafasi ya Gwanchere.

  “Kwa hali ya kawaida nisingeweza kutishia mtu ambaye sikubishana naye tangu awali, nilikwenda kusaidia kumtoa, hizo nyingine ni siasa, maana ni kikao kilichogusa migogoro ya kisiasa ndani ya chama na baadhi ya watuhumiwa ni hao waliotolewa, ndiyo maana nasema ni siasa,” alidai Wenje.

  Kuhusu bastola Wenje alisema: “Kweli bastola nilikuwa nayo lakini sikumtishia nayo mtu yeyote, kwanza purukushani hiyo haikuhitaji hata kutumia rungu, sembuse bastola, nilikuwa nimevaa shati bila koti na nimekunja mikono labda katika harakati ilionekana na kudhaniwa natishia”.

  Alidai wapo wanaoweza kusema, kwa kuwa aliyekuwa karibu ni Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia na meza kuu mbali ya Dk Slaa alikuwepo pia Katibu wa Mkoa wa Mwanza, Wilson Mushumbusi na Meya wa Jiji la Mwanza, Josephat Manyerere.

  Dk. Slaa alipotafutwa na gazeti hili kuzungumzia tukio hilo alikataa kulizungumzia akidai kuwa analenga uchaguzi wa Arumeru Mashariki zaidi na kisha kukata simu.

  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alikiri kupata taarifa za suala hilo kwa njia ya mtandao na kueleza kuwa hatima yake itajulikana baada ya uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki na uchaguzi mdogo wa udiwani Kirumba, Mwanza.

  “Ni kweli, tumelisikia hilo lakini akili na mawazo yetu yote sasa hivi tumeelekeza kwenye kampeni Arumeru na udiwani Mwanza, tukimaliza huko tutalishughulikia hilo. Lazima kusikiliza pande zote mbili na kuchunguza kila madai, kila kitu kina chanzo na huenda hata tukio lenyewe halipo jinsi linavyodaiwa,” alisema Mbowe.

  Mbowe alifafanua, kuwa utaratibu wa chama hicho ni kutumia vikao na taarifa rasmi kuhusu tukio lolote na wakipata taarifa ya kilichotokea, watakaa na pande hizo mbili kulimaliza na ikibainika ukweli upo, watachukua hatua kwa mujibu wa utaratibu wao.

  Alipoulizwa kwa taratibu zao endapo Wenje atakutwa na hatia watachukua hatua gani, Mbowe alisema: “Tusizungumzie kuvuka mto wakati bado hatujaona mto wenyewe, tuvute subira tutawaeleza kitakachojiri”.

  Kutoka Mwanza, Grace Chilongola anaripoti kuwa Katibu wa Chadema wa Mkoa, Mushumbusi alisema tukio hilo halina ukweli bali ni uvumi ulioenezwa na mjumbe aliyeondolewa kwenye kikao hicho, baada ya kusimamishwa ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Mkoa mwaka jana.

  Kwa mujibu wa Mushumbusi, waliotolewa ni Litaragula, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Wilaya ya Nyamagana na Robert Gwanchere aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ilemela, ambaye anadaiwa kueneza uvumi huo.

  Katika hatua nyingine, Mbowe alipotakiwa kushauri kuhusu wimbi la matumizi holela ya silaha nchini, aliiomba Serikali kupitia Jeshi la Polisi kuzuia utoaji silaha holela kwa kuwa unahatarisha maisha ya watu badala yake vikosi vya ulinzi na usalama viimarishwe.

  “Hatuwezi kuwa nchi ya watu wanaogawa silaha kama manati, mtu akipata umaarufu kidogo na vihela kidogo, anataka kumiliki silaha, ifike mahali tuelezwe ni Watanzania wangapi wanamiliki silaha na vigezo gani vinatumika kupewa hizo silaha, pia yapo mahitaji ya mafunzo ya matumizi ya silaha,” alisema Mbowe.

  Alishauri wamiliki wa silaha kufuatiliwa kila wakati na kujua kama wanakumbuka matumizi ya silaha na kupunguza kutoa silaha kwa watu hata kama ni mamlaka iliyowekwa kisheria.

  Wenje ni Mbunge wa pili kukumbwa na kadhia hiyo ya silaha baada ya Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM) kupanda jukwaani akiwa na bastola kiunoni kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni katika Jimbo la Igunga mwaka jana. Pia Dk. Slaa alipata kukutwa na silaha mkoani Arusha baada ya kupekuliwa katika gari alimokuwa.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 21, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Hizi bastola wanazinunua wapi?
   
 3. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #3
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  bora umeuliza naona imeshakuwa fasheni kila mtu kuwa na bastola.
   
 4. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #4
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  sidhani kama ni kweli madai ya malalamikaji yana ukweli! Kwa mazingira ya fujo za wanachama wa CCM nashauri kila Mb wa CHADEMA awe na bastola yake ya kujilinda haswa kipindi cha kampeni za uchaguzi maana tunaona jinsi siasa za ugomvi zinavyokuwa ni utamaduni wa Magamba!
   
 5. I

  IFRS 9 Senior Member

  #5
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanganyika arms
   
 6. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #6
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Bila shaka ndio wanaouza hivi vitendea kazi. Wanapatikana wapi?
   
 7. KIMBWANGAI

  KIMBWANGAI Member

  #7
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  itabidi hili liangaliwe kwa jicho la tatu coz kamekua ni kamchezo sasa
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kila mkoa una ofisi yake kwa hapa Moshi iko pembeni ya Tanesco na opposite ya Malindi night club, ukitaka za magumashi zipo pia
   
 9. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #9
  Mar 21, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Wewe Angela na wewe unayo nini hiyo kitu?
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Thanks for the source.......untrustworthy as it is
   
 11. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #11
  Mar 21, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  ukiwa na nyumba 2,gari 3 na viofisi vi 2 unapatiwa
   
 12. u

  ulimbaga mwamsiku New Member

  #12
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kumiliki bastola sio tatizo cha msinhgi matumizi yake tu,yaani ni wakati gani itumike,sio kama matumizi aaliyotumia Dito!!!!
   
 13. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #13
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu huo ndio ukweli. Issue ni matumizi na si umilki. Inaonekana viongozi wetu ndio wanazitumia vibaya
   
 14. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #14
  Mar 21, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sasa bastola ya nini mkutanoni?

  Chadema inabidi wawe makini na haya mambo, sehemu kama hiyo watu wasiingie na silaha huwezi jua jazba itapanda wakati gani.
   
 15. escober

  escober JF-Expert Member

  #15
  Mar 21, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 391
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wakuu hii habari ya lini mbona Dr. slaa ameisha ondoka mwanza siku nyingi and the last time i checked alikuwa kwenye kampeni arumeru au amerudi tena huko?
   
 16. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #16
  Mar 21, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,897
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  ndio maana malima ameamua kumiliki na smg maana kila mtu ana bastola..nina wasiwasi lowassa anatembea na bastola,smg,AK 47,rocket propelled grenades na mapanga.
   
 17. CPA

  CPA JF-Expert Member

  #17
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 737
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  mhh! Huo sio utetezi, magazeti 3 yametoa hiyo habar. Kubar tu hizi siraha cku wanashika watu wasio staili
   
 18. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #18
  Mar 21, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Upanga(Mzinga) makao makuu ya jeshi ndiyo zinapatikana kwa bei rahisi, ziko hata za laki tatu....
   
 19. k

  kamakak Member

  #19
  Mar 21, 2012
  Joined: Sep 22, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Huyu wenje kwanza sio mtanzania.Mmeona nyie CHADEMA kutuletea wakenya kwenye siasa za Tanzania sasa anataka kuwaua.Huyu aliletwa na shule moja ya kiislam pale mwanza kutokea kenya kama mwalim.Akawa na mchezo wa kufanya mchezo mchafu na watoto wa kike akafukuzwa.Si mnakumbuka aliwekewa pingamizi na Masha wakati wa uchaguzi.Yaani ni ugomvi wa Masha na Mengi ndiyo ulimsaidia maana mengi alifanya chini juu rufaa yake inashinda tume ya uchanguzi.
   
 20. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #20
  Mar 21, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  1. Uhuru
  2. Jambo leo
  3. Habari LEO
  4. Daily news
   
Loading...