Wengine hatumpendi Mungu tunajilazimisha tu

mkuu kumbuka wakati Mungu anamuumba mwadamu haikuwa lengo lake mwanadamu kufa ila alimwambia utakapo kula mtu huo ni hakika utakufa.

Na mimi na wewe tunajua kabisa kuwa shetani ndio sababu ya mwanadamu kula lile tunda kwa maana yeye ndie alie washawishi hivyo ni Lucifer anapaswa kulaumiwa juu ya vifo vya wanadamu.
Mkuu soma tena ulichoandika, haikuwa mpango wake? Kama ndio hivyo kwa nini akatuumba kama alijua yatakuwa hivi?

Ikiwa ni hivyo huoni kama his mission is a failure?
 
Leo umeniamulia
Kama nakukwaza nisamehe bure najaribu kukupa ushuhuda wangu binafsi kuhusu Mungu. Hasa ukizingatia mimi kwa asili siyo mtu wa kuamini hear-say. Mke wangu,Baba yangu na Mama yangu na wengineo huwa wananiita "mbishi" kumbe kiuhalisia mimi sio mbishi ila ni mtu wa kuhoji sana lakini kwa nia njema ya kutaka kuujua ukweli ili nisiangamizwe kwa kukosa maarifa. Na huwa siwahoji wanadamu tu hadi Mungu huwa namuhoji tena miswali kibao. Na hakuna swali au hoja ambayo mpaka sasa hajanijibu. Hivyo ndivyo ninavyoishi na Mungu kwa miaka 15 sasa.
 
Kiuchumi, kwa mda mfupi alifanya makubwa, muulize hata mzee Mwinyi. Hakika hatutapata tena mtu caregeous kama huyu.
 
Wengine hatuna tu option kulingana na vitisho tulivyopandizwa tangu utotoni ila huyu Mungu hatumpendi haswa
Imagine wewe ni baba wa watoto kadhaa, alafu unawapenda sana wanao ila kuna mtoto mmoja ambae una mapenzi nae zaidi na upo kusimamia mafanikio yake mpaka afanikiwe, ajabu siku 1 unaskia hadharani akiwatangazia watoto wenzie na watu wengine kwamba "Mimi simpendi baba yangu haswa hata kidogo, basi tu anajipendekeza ili aonekane ananijali ila simtegemei kwa lolote lile katika maisha yangu"

Hivi utajisikiaje hapo baada ya kusikia hivyo kwa masikio yako mawili ukiwa na akili zako zinafanya kazi vizuri...?!

Huo nimetoa mfano tu katika maisha halisi ya kibinaadamu.

Sasa wewe jamaa MUNGU anakupenda sana, Na hii nyongo yako uliyotema hapa kaiona ila atakufanyia surprise ambayo wewe mwenyewe na akili zako timamu utakuja kutoa ushuhuda humu na kukubali Mungu yupo ni mwema na mwenye huruma, vilevile kumbuka tu ya kua Mungu HADHIHAKIWI hivyo anaweza pia kukudhibitishia ukuu wake dhidi ya kauli yako hiyo.
 
Siyo kutishana,ni kweli. Kama huamini kwa kusikia subiri utaamini kwa kuona. Kwa hulka, Mimi siyo mtu wa kuamini mambo kirahisi hadi nijiridhishe pasipo shaka yoyote. Achana na faraja hewa ambazo watu wanafarijiana duniani hapa. Mungu yupo na kila asemacho ni dhahiri na kweli.
japo hili la kuchomwa moto milele wakati ulikufa una miaka kadhaa tu lina ukakasi sana!!!mtu aishi miaka 140 halafu afe ahukumiwe moto milele na wala sio miaka 140 alioiishi!!shida sana aiseh!!!
 
japo hili la kuchomwa moto milele wakati ulikufa una miaka kadhaa tu lina ukakasi sana!!!mtu aishi miaka 140 halafu afe ahukumiwe moto milele na wala sio miaka 140 alioiishi!!shida sana aiseh!!!
Ndio maana Mungu hutumia miaka mingi pia kutushauri na kutuonya hadi wengine wanafikia hatua wanautukana uvumilivu huo wa Mungu. Kifupi ni kwamba sisi ndio tunaojichuja wenyewe hapa hapa duniani. Sioni kosa la Mungu. Twende hivi hivi mwisho hesabu. Mwenye masikio na asikie.
 
Dhamiri zipi wakati wao walikua wanafahamu kuua falme nyingi ni jambo la kishujaa
Ukitaka kufanya jambo lolote baya kuna hali inajitokeza ndani yako kabla. Ya kureflect wewe ukifanyiwa jambo hilo utajisikiaje. Hapo ndipo hukumu ilipo. Amri za Mungu zililetwa ili kuhuisha hali hiyo ambayo tuliumbiwa nayo kabla. UTASHI
 
Mfano enzi hizo za utawala watemi walikua wanafanya mapenzi na mabinti ata zaidi ya 50. Na wao walikua wanachukulia kawaida sasa watahukumiwaje
 
Mkuu soma tena ulichoandika, haikuwa mpango wake? Kama ndio hivyo kwa nini akatuumba kama alijua yatakuwa hivi?

Ikiwa ni hivyo huoni kama his mission is a failure?
kutuumba ilikuwa mpango wake, lakini kifo kwa mwanadamu haikuwa mpango wake.

Kuthibitisha hilo hata baada ya mwanadamu kuwa ameanguka dhambini bado amemtoa mwanae ili kuweza kurudisha hali ile ya mwanadamu iliyopotea ya kutokufa.
Yohana 3:16-17 "16 Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele. 17Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye."

kwa hivyo mkuu kama mimi na wewe tukimpokea ni hakika baada ya haya maisha tutaishi milele. Nipende kukualika tufanye jitihada ili tusiikose nafasi ya pili tuliyopewa ya kuishi milele. Kumbuka aliye mwangusha Adam na mpaka leo kifo kipo bado pia lengo lake ni kutuangusha ili pia tuikose nafasi hii ya upendeleo iliyotolewa tena.
 
Sasa hiyo dhambi inatunusu nn sisi?
Hii dhambi inatuhusu kwa sababu sisi tu watoto wa Adam na kwa kuwa tu watoto wake basi hii tayari imekuwa kwenye asili yetu.

Na hii haikuwa kwa Adam tuu ata sisi leo hii kuna dhambi zetu ambazo tunazitenda na kupelekea kizazi na kizazi kuzirithi. Mfano mtazame Daudi na dhambi yake ya uzinzi hata baada ya kumuomba Mungu msamaha na akasamehewa lakini hata kizazi chake bado kilitembea na hiyo dhambi bado.
 
mkuu kumbuka wakati Mungu anamuumba mwadamu haikuwa lengo lake mwanadamu kufa ila alimwambia utakapo kula mtu huo ni hakika utakufa.

Na mimi na wewe tunajua kabisa kuwa shetani ndio sababu ya mwanadamu kula lile tunda kwa maana yeye ndie alie washawishi hivyo ni Lucifer anapaswa kulaumiwa juu ya vifo vya wanadamu.
Hizi nadharia hazitafsiriki.
Kwann Mungu alimtupa shetani duniani badala ya motoni
 
Back
Top Bottom