Kuna wakati ilinibidi niwe mbali na familia kwa sababu ya shule. Kule nilipokuwepo nilionekana mama mbaya sana kwa sababu niliacha watoto wadogo, nikaenda kutafuta shule. Lakini mimi wakati nafanya hivyo, nilikuwa nafanya kwa ajili ya familia!
Japo umesema kazi, lakini naona inaendana pia hata mambo ya shule, kwa sababu tunaongeza elimu ili pia kipato kiongezeke, japo sio siku zote! Sijaweza kujibu swali kwa sababu vyote muhimu kwangu!
....Keren_Happuch wala hujakosea, ndio maana nikajisemea niwaulize nyie wenzangu kwa experiences zenu ila,
issue hii kidogo ni tofauti na 'shule' iwe ni college, au university ambayo ni short term, iwe ni 6mths, 1yr au 3yrs...
...kazi kidogo ni tofauti, kwani inaweza ikawa ni 5yrs- 10yrs contract, ....au kama ndio 'maboksi,' miaka 15 sasa kuna watu hawajarudi makwao, ...wazee, ndugu jamaa na marafiki, wanaoa, wanaugua na wanaokufa wao wanatuma pesa tu za shughuli...!
Naona kwenye mabano hapo umenieahi....lol...
Well kwa mtazamo wangu what determines kipi kuchukue nguvu zaidi (i.e familia vs kazi) ni hali halisi ya maisha ya hio familia hasa upande wa kipato. Kuna vipato vimetofautiana jinsi na wapi pa kuvipata.... Hii inasumbua saana kwa upande wa wale ambao source za vipato zao ni Career ambayo mara nyingi hua nurtured for a long time na there is no turning back hasa kwenye ma firms na companies...
Mie hapa nimeshindwa kabisa kusema nini bora zaidi... Logically speaking familiy comes first no matter what.... Na family coming first does not neccessarily mean kua wakati woote utakua nao karibu; for saa ingine unakaa nao mbali sababu tu ya kuhakikisha they are getting the best in this world ambayo kila kitu kinauzwa.... na the more expensive services... the best of it.
Realistically speaking aisee.... you have to have money to support your family.... Ndio maana nilisema option ya tatu iwe both...lol
unakaa nao mbali sababu tu ya kuhakikisha they are getting the best in this world
kipato na familia vyote vinategemeana, ila kipato ni muhimu zaidi manake kitaiwezesha familia kuwa bora, kuwa mbali na familia haimaanishi kuwa umeacha kuijali, makubaliano ndicho kitu cha muhimu hapa.
Mhhh...sasa hapo kwa muda mrefu kiasi hicho, basi inakuwa ngumu kweli! Mimi nafikiri pia cha muhimu, familia ina mipango gani? Sasa kweli MBU...15 yrs away from your family???!!! Hapana jamani...sasa hapo si ndo unakaribisha majaribu mengine, halfu unamsingizia shetani! Lakini iwepo mipango ya familia!
Mzee mosquito hiyo kazi ni kwa ajili ya welfare ya familia yako as well
I had a relative alikuwa na dilema of ur sort yeye alipiga mgodini but as soon as alipomaliza mjengo wake pale A town aliquit job na kurejea home kwa familia yake na sasa they are happy kwa sanaa tu. Hapo u must strike a fine ballance ili familiymembers waone faida ya wewe kuwa mbali nao.....comparative advantage......
Set the target and hit the bull.......kabhaaaang u get up and slowly u re-join ur family........sio ukae wee mbali na ukija huko ni story tu na kuchukua tena na kidogo ulichokuta hapo home unatokomea tena
Pole kaka mzani huo ballancing point yake ni ngumu ila inatafutika.....no formula though
...nisaidieni mawazo wanandugu.
Baina ya kipato na familia kwa mtazamo wako, kipi unakipa uzito mkubwa kuliko kingine?...
...kabla wenye muono 'tofauti' hamjanitoa jicho, kipato namaanisha
kazi yenye kipato kikubwa inayonilazimu nikae mbali na familia kiasi cha
kuonana nao wakati wa likizo ya mwezi mmoja, kila baada ya miezi sita au nane.
Mazingira ya kazi hayaruhusu kuishi pamoja na familia.
Vyote ni muhimu, unaweza kujikuta unakimbiza kipato ukapoteza familia uliyokua unadai ndio unayoisumbukia, unaweza ukakumbatia familia huku mkiwa na matatizo mengi ambayo yangetatulika iwapo ungekimbizana na kipato.
Kwahiyo ningeshauri utafute balance, usikipe kipato 70% na familia 30% kwasababu waweza jikuta umetupwa nje ya mzani. Angalia huko unakofuata hicho kipato, angalia je hicho kipato/muda/umbali vitaruhusu wewe kuwa karibu na familia kiasi cha kutosha? Jiulize, je familia yako inaweza ikasurvive kwa kupata pesa nyingi bila baba around? Je mnaweza mkasurvive bila hizo pesa huku baba akiwepo karibu? . . .
...sweetlady karibu na asante kwa mchango wako, umegusia makubaliano... nadhani hii inahusisha zaidi baina ya mke na mume. Je? nini athari za makubaliano haya kwa mtoto au watoto ambao kwa kipindi kirefu wataishi bila baba/mama? ...ushawahi lifikiria hilo?
...."the precious time lost, is lost forever!"
Bless you Lizzy,....woww!
...umenifunga tena kwenye jibu,....hapo una maanisha familia kwanza kabla ya kipato, si ndio?
Asante, ni maamuzi magumu yanayohitaji hekima.
Tukija kwenye swala la watoto hapo sasa tunahama kwenye kipengele cha makubaliano na kuhamia kwenye kipengele kingine cha malengo. Ni vizuri sana watoto wakapata malezi ya baba na mama, hiyo ni haki yao ya msingi kabisa....ndio mana hapo nimesema inabidi kuwa na malengo madhubuti, manake mke na mume mnaweza kufanya makubaliano lakini wakati huo huo yakawa na madhara kwa watoto japo pia yanaweza yasionekane kwa wakati huo... Mbu kila kitu kwenye haya maisha ni kwa mipango na malengo... Lazima ujipange na kuhakikisha kuwa huegemei upande mmoja sana( kazi iwe 50% na familia iwe 50%)...familia hata ikiwa na kipato kiasi gani amini usiamini kama haiko pamoja( baba, mama, na watoto) haitakuwa na furaha...japo kwa nje inaweza kuonekana yenye furaha... Mada yako ngumu bana, naungana na AshaDii kudai kipengele cha both...
Ahsante Mbu. . . nawe pia.
Hopefully umekaribia kupata muafaka.
...hahahaha, sasa hapo kwenye wekundu nawe umenifunga, maana umeanza vizuri tu kuwa malezi ya watoto yanahitaji presence ya wazazi wawili....sasa ugumu upo wapi namai nachotaka ni uamuzi kipi bora kati ya kipato kikubwa au familia?
...unajua kama ni mtumbwi, wangu ulikuwa anaingiza maji. Angalau umenitupa kifuniko cha X-pel kunisaidia
kuyapunguza...
kiukweli,...kuna kitu umegusia kuhusu balancing hapo...yaani umenipa mwanga wa ku sacrifice kipato kinachokidhi 95% ya mahitaji ya familia, ili kuweza kupunguza hilo gap la umbali....
...au nimekuelewa vibaya? wengine mnasemaje! :A S-coffee:
Umenipata sawia Mbu, usishikiliee sana kimoja na kusahau kingine maana mwisho wa siku unaweza ukapoteza familia ukashindwa kuelewa hata ulichokua unahangaikia. Chukua karatasi na kalamu, piga hesabu ya umbali, piga hesabu ya mshahara (utatosha kuwaweka karibu, au ni chakula/malazi na mavazi tu), piga hesabu ya muda mtakaokua apart (is it reasonable? Sio unakua mbalia kiasi kwamba ukirudi unakuta watoto walishaota ndevu wakati uliwaacha bado wanaendesha baiskeli za mbao).
Unaweza ukaandika list mbili. . . KAZI (faida na hasara), FAMILIA (faida na hasara) alafu upime uzito.