Wengi humu JF wanaojiita introverts si introverts

Wengi humu JF wanaojiita introverts si introverts

Hata mimi nasoma avatars
1649712606588.png

Extroivert nasoma comments
 
Mkuu kama kitu hujui kubali, then acha uelekezwe. Unaposema ni ujinga unakosea mno.

Kila mtu ni bora kwa nafasi yake. Watu wengi kuwaona intros bora kulichangiwa na watu wengi mashuhuri na wavumbuzi wa vitu vikubwa kutoka kundi hili.

Mifano nafikiri unaijua! Kuna extroverts pia walifanya na hufanya makubwa sana, ila intros wameonekana kuwa more than the extros katika hili.
Nadhan wee umeangalia ktk mazuri TU.

Ila umesahau introverts wanamadhaifu Sana kuishi nao ktk jamii.

Wana kiburi flani hivi Cha ubinafs na kutokujali hisia za wengine, Ambacho Bila shaka Ndo kimekufanya Umeandika Uzi huu[emoji4]
 
Kwema ndugu zangu? Nimelazimika kufungua uzi huu,baada ya kuona watu wengi wa humu wanachanganya sana haya mambo.

Nimepitia nyuzi nyingi humu nimejionea asilimia kubwa ya watu wakijiita introverts ilhali sifa wanazosema wanazo haziendani kabisa na introversion.

Humu wengi wanaojiita introverts ni[emoji116][emoji116]

Watu wenye dharau na wanaoringa; hakuna sehemu ambayo wamesema kuwa introvert eti ndio uwe na dharau kwa wenzio no.

Wewe unadharau simu za wenzio wewe si introvert na acha mara moja kujiita introvert. Unadharau texts za wenzako ilhali hazina sababu za kudharauliwa, wewe sio introvert.

Huitikii ukisalimiwa na watu ilhali unasikia vizuri wewe una kibri na unaringa, si introvert. Acha mara moja kujiita introvert.

Kuogopa kwako discussion chuo kusikufanye kujiita introvert. Wewe ni mpole na hujiamini na si introvert. Introvers WANAJIAMINI, hawapendi kuongea hovyo haimaanisha hawawezi kuongea wala kujieleza.

Newton, Einstein, JESUS etc, hawa hawakupenda kuongea hovyo na walikuwa introverts. Ila walijua kuongea pale WALIPOTAKA na waliweza kupangilia hoja na kujieleza vizuri kiasi cha kuwashinda na kuwashangaza extroverts wengi sana.


Wewe ni domo zege sio introvert! Introvert humtongoza binti yeyote atakayemtaka, na kwa wakati atakaotaka yeye. Acheni kujificha kwenye calibre za watu.

Huenda wengine humu wakawa wagonjwa wa akili tu na wako stressed na mambo yao, ila wanajificha kwenye kivuli cha introversion.

Ukijijua una dalili tajwa hapo juu, TAFADHALI! KAKA, DADA, MJOMBA, BABA, MAMA, BIBI:

Haraka sana kamuone daktari, acha kulilea lea tatizo uepuke makubwa huko mbeleni.


Kuna vijitabia vingi tu vya kipuuzi sijavitaja ila watu wengi waliojificha kwenye muamvuli wa 'mimi ni introvert' wanavyo.

Halafu mwisho ni kuwa, kama huna confidence ya kuongea mbele za watu iwe chuoni, au sehemu nyingine yoyote, wewe si introvert.

Introvert anajiamini na haogopi umati wa watu kuongea atakachotaka, kamuone Dr! Anajiamini na anamudu hoja kinzani dhidi yake.

*Najazia nyama

Introvert hana majivuno, hana dharau, si kiburi, si mjinga, si domo zege, anashirikiana na watu kwa sababu maalumu, na sio kwamba hawezi ku socialize..

Ni kweli hana kabisa au ana marafiki wasiozidi 2. Hii ni kwa 7%. Mara nyingi hawana marafiki kabisa.

Huwezi kukuta introvert ni tapeli au mwongo mwongo, never. Humu unakuta mtu anajiita intro unamkuta kwenye uzi mwingine anasimulia mambo ya ajabu tofauti kabisa na intro.

Introvert anaongea pale inapobidi, na sio kwamba anaogopa kuongea.

Tena vyuoni watu wa namna hii ndio hutoa hotuba zenye hisia na za kuteka watu wengi sana.

Humu watu wengi kwa ushahidi wa wazi kabisa, si intros. Wengine wana stress za mapenzi, wengine wapole tu, wengine viburi n.k, intros ni wachache sana humu.

Wengi ni matapeli na wanavamia calibres za watu.

Suala la intros kutopenda mikusanyiko ni kweli, ila hawaogopi mikusanyiko.

Wewe unapochukia mikusanyiko kwa sababu ya udhaifu ulionao unaokufanya usijiamini acha kujiita intro. Mwingine ana sura isiyovutia, anachekwa sana na anapoteza kujiamini mbele za watu. Huyu si introvert na anatakiwa apate Mwanasaikolojia haraka.

Mtu wa namna hii anaweza hata kujiua.

Hope nimeeleweka, sio uadui jamani tunawekana sawa tu. Amani!!!

[emoji115][emoji115]Nimejazia nyama baada ya maombi ya baadhi ya wadau!
Wewe umeawajuaje wakati huwafahamu? Keyboard warriors humu ndio wengi
 
Ni wao, nawe ikikupendeza jiite extrovert au vyovyote. Acha kuonesha viashiria vya wivu mkuu.
Mkuu,
Mbona Inaonekana wee ndo unaeteseka Sana mtu kujiita introvert humu jf[emoji28]

Ungekua uteseki sidhan Kama ungeanzisha Uzi wa namna Hii na shutuma nzito Kama hizi[emoji4]
 
Wewe umeawajuaje wakati huwafahamu? Keyboard warriors humu ndio wengi
Mtoa mada hawafahamu ktk madhaifu Yao, amekalili mazuri Yao.

Anapokutana na madhaifu Yao anahisi wanajiskia, wanadharau n.k
Wakati hayo ndo madhaifu Yao kiuhalisia[emoji4]
 
Mkuu kama kitu hujui kubali, then acha uelekezwe. Unaposema ni ujinga unakosea mno.

Kila mtu ni bora kwa nafasi yake. Watu wengi kuwaona intros bora kulichangiwa na watu wengi mashuhuri na wavumbuzi wa vitu vikubwa kutoka kundi hili.

Mifano nafikiri unaijua! Kuna extroverts pia walifanya na hufanya makubwa sana, ila intros wameonekana kuwa more than the extros katika hili.
Hivi Huu Ujinga wa kuamini introvert Ni Bora kuliko extrovert Ndo unaokuumiza KICHWA mpk ukaamua kuja kuanzisha uzi Kama huu?

Hivi tukisema wewe ndio unawaonea wivu wanojiita introvert tutakua tunakosea?

Aya twambie Sasa,
wewe Ni introvert au extrovert?

Inavoonekana wee ukiitwa extrovert unajihisi Kama umetukanwa Sana eeh?[emoji4]
 
Nadhan wee umeangalia ktk mazuri TU.

Ila umesahau introverts wanamadhaifu Sana kuishi nao ktk jamii.

Wana kiburi flani hivi Cha ubinafs na kutokujali hisia za wengine, Ambacho Bila shaka Ndo kimekufanya Umeandika Uzi huu[emoji4]
Ni kweli mkuu! Kongole kwa kuangazia hilo.
 
Mkuu,
Mbona Inaonekana wee ndo unaeteseka Sana mtu kujiita introvert humu jf[emoji28]

Ungekua uteseki sidhan Kama ungeanzisha Uzi wa namna Hii na shutuma nzito Kama hizi[emoji4]
Nateseka.! Hasa kuudhihaki upande mwingine. Mtu akiwasema exro naumia pia. Haya makundi yote mawili ni muhimu.
 
Hivi Huu Ujinga wa kuamini introvert Ni Bora kuliko extrovert Ndo unaokuumiza KICHWA mpk ukaamua kuja kuanzisha uzi Kama huu?

Hivi tukisema wewe ndio unawaonea wivu wanojiita introvert tutakua tunakosea?

Aya twambie Sasa,
wewe Ni introvert au extrovert?

Inavoonekana wee ukiitwa extrovert unajihisi Kama umetukanwa Sana eeh?[emoji4]
Hahah mimi ni bonge la ambient. Nipo kote kote mkuu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom