Wengi humu JF wanaojiita introverts si introverts

Zee Korofi

JF-Expert Member
Oct 5, 2021
1,612
1,410
Kwema ndugu zangu? Nimelazimika kufungua uzi huu,baada ya kuona watu wengi wa humu wanachanganya sana haya mambo.

Nimepitia nyuzi nyingi humu nimejionea asilimia kubwa ya watu wakijiita introverts ilhali sifa wanazosema wanazo haziendani kabisa na introversion.

Humu wengi wanaojiita introverts ni

Watu wenye dharau na wanaoringa; hakuna sehemu ambayo wamesema kuwa introvert eti ndio uwe na dharau kwa wenzio no.

Wewe unadharau simu za wenzio wewe si introvert na acha mara moja kujiita introvert. Unadharau texts za wenzako ilhali hazina sababu za kudharauliwa, wewe sio introvert.

Huitikii ukisalimiwa na watu ilhali unasikia vizuri wewe una kibri na unaringa, si introvert. Acha mara moja kujiita introvert.

Kuogopa kwako discussion chuo kusikufanye kujiita introvert. Wewe ni mpole na hujiamini na si introvert. Introvers WANAJIAMINI, hawapendi kuongea hovyo haimaanisha hawawezi kuongea wala kujieleza.

Newton, Einstein, JESUS etc, hawa hawakupenda kuongea hovyo na walikuwa introverts. Ila walijua kuongea pale WALIPOTAKA na waliweza kupangilia hoja na kujieleza vizuri kiasi cha kuwashinda na kuwashangaza extroverts wengi sana.


Wewe ni domo zege sio introvert! Introvert humtongoza binti yeyote atakayemtaka, na kwa wakati atakaotaka yeye. Acheni kujificha kwenye calibre za watu.

Huenda wengine humu wakawa wagonjwa wa akili tu na wako stressed na mambo yao, ila wanajificha kwenye kivuli cha introversion.

Ukijijua una dalili tajwa hapo juu, TAFADHALI! KAKA, DADA, MJOMBA, BABA, MAMA, BIBI:

Haraka sana kamuone daktari, acha kulilea lea tatizo uepuke makubwa huko mbeleni.


Kuna vijitabia vingi tu vya kipuuzi sijavitaja ila watu wengi waliojificha kwenye muamvuli wa 'mimi ni introvert' wanavyo.

Halafu mwisho ni kuwa, kama huna confidence ya kuongea mbele za watu iwe chuoni, au sehemu nyingine yoyote, wewe si introvert.

Introvert anajiamini na haogopi umati wa watu kuongea atakachotaka, kamuone Dr! Anajiamini na anamudu hoja kinzani dhidi yake.

*Najazia nyama

Introvert hana majivuno, hana dharau, si kiburi, si mjinga, si domo zege, anashirikiana na watu kwa sababu maalumu, na sio kwamba hawezi ku socialize..

Ni kweli hana kabisa au ana marafiki wasiozidi 2. Hii ni kwa 7%. Mara nyingi hawana marafiki kabisa.

Huwezi kukuta introvert ni tapeli au mwongo mwongo, never. Humu unakuta mtu anajiita intro unamkuta kwenye uzi mwingine anasimulia mambo ya ajabu tofauti kabisa na intro.

Introvert anaongea pale inapobidi, na sio kwamba anaogopa kuongea.

Tena vyuoni watu wa namna hii ndio hutoa hotuba zenye hisia na za kuteka watu wengi sana.

Humu watu wengi kwa ushahidi wa wazi kabisa, si intros. Wengine wana stress za mapenzi, wengine wapole tu, wengine viburi n.k, intros ni wachache sana humu.

Wengi ni matapeli na wanavamia calibres za watu.

Suala la intros kutopenda mikusanyiko ni kweli, ila hawaogopi mikusanyiko.

Wewe unapochukia mikusanyiko kwa sababu ya udhaifu ulionao unaokufanya usijiamini acha kujiita intro. Mwingine ana sura isiyovutia, anachekwa sana na anapoteza kujiamini mbele za watu. Huyu si introvert na anatakiwa apate Mwanasaikolojia haraka.

Mtu wa namna hii anaweza hata kujiua.

Hope nimeeleweka, sio uadui jamani tunawekana sawa tu. Amani!!!

Nimejazia nyama baada ya maombi ya baadhi ya wadau!
 
Back
Top Bottom