Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
maandiko matakatifu yanasema ukweli hukuweka huru na mimi leo hii nimeamua kuongea ukweli ambao nahisi utaniweka huru.
ukweli huu uko wazi kwa baadhi ya watu wanaoifuatilia na kuitakia mema arsenal.
natanguliza maneno haya kwa baadhi ya watu kwa ajili ya kujihami "naomba nisionekane adui kwa kusema ukweli".
ni wazi kocha wa arsenal mfaransa mchumi arsene wenger ameshindwa kutupatia mafanikio tunayoyahitaji katika klabu yetu.
sera zake na mbinu zake zimeonekana kushindwa kumudu ushindani wa kubeba vikombe nchini uingereza na hata barani ulaya.
sera yake ya kuamini sana vijana na ubahiri uliokomaa na kuota mizizi pia vimechangia kuzorota kwa arsenal kwa siku za karibuni.
SERA YA MIAKA 30...
sera hii amekuwa akiitumia kwa miaka ya hivi karibuni kwa kuwauza wachezaji wenye umri wa miaka 30 na zaidi au kuwa anawapa mkataba wa msimu mmoja kitu ambacho kinachukiwa na wachezaji wa kulipwa barani ulaya.
sera hii pia imepelekea kuondoka kwa wachezaji wengi ambao kwa namna moja au nyingine wangeweza kutumia uzoefu wao kuhakikisha mafanikio yanapatikana klabuni.
SERA YA KUKUZA VIPAJI...
moja kati ya sera anayojivunia mfaransa huyu ni kukuza vipaji vya wachezaji.
lakini hii haileti maana kwa sababu wachezaji anaowakuza mwisho wa yote huwa hawatumii na huwauza kwa timu nyingine.
tumeona mifano mingi kama fabrice muamba, sebastian larson, jermain penant, mathew upson, jermain aliadiere, david bentley na wengine wengi wakiunguruma na kung'ra katika klabu zao.
CAPTAIN...
katika vitu vilivyoniuma msimu huu ni kumnyang'anya wadhifa wa captain mpiganaji Gilberto Silva ambaye kwa kweli hujituma kwa moyo wake wote awapo uwanjani ili kuhakikisha arsenal wanapata ushindi.
girberto alipokwa wadhifa huo pasipo kupewa hata taarifa na kupoteza namba yake uwanjani, namba ambayo ilikabidhiwa kwa mfaransa mwenzie wenger bwana mathew flamini ambaye siwezi kumuelezea kwa jinsi alivyotutenda na kuhamia AC milan.
lakini baadae wenger alipohojiwa alisema kuwa ameamua kumpa gallas wadhifa huo kwa sababu gallas yupo nyuma hivyo anaiona timu nzima na hivyo ataweza kutoa maelekezo kwa wachezaji woote.
lakini waandishi wakamuhoji je kwa nini hukumpa lehman ambaye ndio mtu wa mwisho na anaiona timu nzima pamoja na huyo gallas? kisha wakamtwanga na swali jingine je mbona ulishawahi kumteua thiery henry ambaye ni mshambuliaji kuwa captain je hapo ilikuwaje?
mzee wenger alikosa jibu.
gilberto aliingia kwenye kumbukumbu ya vitabu vya arsenal siku alipoifungia gunners goli la pekee katika mechi yake ya kwanza kuichezea arsenal, pale alipofunga goli dhidi ya liverpool katika mchezo wa ngao ya hisani akiingia mwanzo wa kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mbrazil mwenzie Edu aliyetoka kutokana na majeraha ya paja. hivyo ni wazi kuwa wenger hakumtendea haki gilberto kwa maamuzi hayo ya kumnyang'anya wadhifa wa captain.
KUIAMINI TIMU MOJA...
wenger amejenga timu ambayo nikilala nikiamka najua ni wachezaji gani watakaoanza katika mechi, pia wenger ameshindwa kufanya mzunguko ambao matokeo yake sasa yamekuja kuonekana kuwa kuna baadhi ya wachezaji wamebweteka wakijua kuwa wana namba za kudumu na hakuna swala la kugombea namba wala kuwa na ushindani.
ARSENAL WANASHINDWA KUMALIZIA LIGI WAKIWA KILELENI...
kwa mara nyingine tena arsenal tunashindwa kumalizia ligi tulioianza vizuri na matokeo yake tunakuja kuiachia nafasi ya kwanza tulioishikilia kwa muda mrefu na kumaliza ligi tukiwa katika nafasi ya tatu.
hii inatokana na ubishi wa mzee wenger kwani wachunguzi wa maswala ya soka walimwambia anunue wachezaji katika kipindi cha dirisha dogo la usajili la january, lakini mzee huyu alijibu siwezi kununua mchezaji kwani Robin Van Persie akipona atakuja kutuongezea nguvu hivyo itakuwa ni kama mchezaji mpya kwetu, lakini haikuwa hivyo kwani baada ya usajili kufungwa Eduardo aliumia vibaya mguu na kutakiwa kukaa nje kwa kipindi kirefu sana hivyo Van Persie alilazimishwa kucheza ili kuja kuziba pengo la Eduardo.
UCANT TAKE PREMIERSHIP WITH TEENAGER...
maneno haya alianza kuambiwa na sir bobby robinson, pia maneno haya aliyarudia captain wa heshima wa arsenal Tony Adams na hivi majuzi maneno haya kaambiwa tena na Jose' Mourinho wakiwa na maana kuwa huwezi kuchukua ligi kuu ya uingereza ukiwa na wachezaji vijana.
na hapa ndo ninawakumbuka kina Fleddie Ljungberg, Robert Pires, Sol Campbell, Patrick Vieira, Edu, Thiery Henry, Lauren na wengine wengi ambao wangeweza kutumia uzoefu wao kuhakikisha arsenal tunapata mafanikio, leo hii watoto wameshindwa kumalizia mkia kwa kukosa uzoefu.
ADEBAYOL...
kama utazungumzia uozo wa arsenal basi huwezi kuacha kumtaja jamaa huyu.
yeye msimu huu ndie amekuwa kielelezo cha uozo wa klabu kwa kukosa nafasi nyingi za kufunga, kupoteza mipira mingi uwanjani, kushindwa kujipanga katika mitego ya offside awapo uwanjani, kutoitumikia timu kwa juhudi zake binafsi, na pia ameshindwa kuyamudu majukumu aliyopewa na kuaminiwa na arsenal.
ni kweli adebayol ametufungia magoli mengi msimu huu lakini ni wazi kuwa magoli hayo ni magoli ya utamaduni wa arsenal kwani ni magoli ambayo yeye binafsi anatakiwa kumalizia kwa kufunga kitu ambacho kama angekuwa makini na jukumu hilo alilopewa basi angekuwa na magoli mengi zaidi ya haya ya sasa.
ni wazi kuwa adebayol si mshambuliaji wa hadhi ya klabu kama arsenal, na hapa ndipo tunakuwa na wasiwasi na uwezo wa arsenal.
USHINDANI WA VILABU VIKUBWA BARANI ULAYA...
wachunguzi wa maswala ya soka walihoji kwa nini wenger huwa hajitosi kwenye vinyang'anyiro vya kugombea kununua wachezaji wenye majina na uwezo mkubwa? ukizingatia kuwa soka la ulaya kwa sasa limekumbwa na ushindani mkubwa kutokana na timu nyingi kumilikiwa na matajiri ambao wanatumia hela kununua wachezaji ili wapate mafanikio, je wenger na watoto wake wataweza kumudu ushindani huu? au ndo tutakuwa tunawaachia usukani wenzetu zikiwa zimesalia mechi saba ligi kuisha?
hivyo mifumo na imani zilizopitwa na wakati za wenger ndizo zilizotufanya kukosa raha msimu huu na kusemwa vibaya kila tutakapopita, ni wazi kuwa kwa mifumo hiyo ya wenger haiwezi kutusaidia kupata kikombe chochote kwa sasa, hivyo wakati umefika kwa mfaransa huyu kuachia timu na kutafuta changamoto kwingine...