Wema Sepetu: Wasanii tunakidai Chama madeni ya uchaguzi 2015, Tunaambiwa nendeni mkamdai Kikwete

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,591
36,004
"Nendeni mkamdai Kikwete"
Hii ni kauli ambayo msanii Wema Sepetu ameitoa na kwa kweli imeusononesha sana moyo wangu. Sii kauli ya kiungwana kujibiwa watu wale waliomsaidia Rais Magufuli kuingia ikulu. Ole kwa yule aliyetoa majibu hayo!

Nadhani kauli hii itaweza kuusononesha sana moyo wa rais mstaafu ndugu Jakaya Kikwete ambaye alifanya kila liwezekanalo "liwe la kifedhuli au la haki" kuhakikisha Magufuli anashinda hasa kutokana na ule ushindani mkali uliokuwepo.

Ni kauli inayoendeleza udhihirisho wa kiburi na ulevi wa madaraka vilivyoujaa utawala huu wa awamu ya tano! Si kauli nzuri hata kidogo.

Majibu ya hovyo yanayotolewa na baadhi ya watendaji kwenye huu utawala kama haya yanadhihirisha kuwa watanzania bado tunajithibitishia wenyewe jinsi tulivyopotea njia.

Aidha kusukumiwa mzigo huu wa wadai wa CCM kwa Kikwete kunaendelea kudhihirisha utu wake na uungwana ambao mimi ni miongoni mwa wadau tunaolia machozi makuu kuukosa na kujikuta tukitumbukia tusikokujua. Kwa haya siamini kama mdai mwingine Shigongo yu salama na ahadi aliyopewa hivi karibuni.

Angesema alijibiwa na nani, ameongea atafute pa kuokea kwa kudanganya. Eti hadi leo hakulipwa na alikaa kimya mmmmmh

Naongezea
Je ameandija barua ya kudai pesa hizo? Na walipewa contract ya kazi na malipo au ni yale yale ya maziea kupeana kwa kujuana chini ya roof? Also inabidi sasa aweke makaratasi yasomwe ya ahadi na kukubaliana malipo. Alifikiri chama kitakuwa na pesa za kupoteza kuwapa zaidi ya walichopewa, hiyo ni hakuna tena. Mchezo wa chini ya carpet umekufa.
 
Nikisikia watu wanavyomlilia Jakaya Kikwete namkumbuka sana Faiza Fox alisema mara nyingi kua tutamkumbuka kwa mema mengi mzee Kikwete naona recently bila kujali tofauti zetu za ki-itikadi za chama au dini wote tumeungana kumkumbuka Jakaya nahisi pia tutamkumbuka sana maana safari bado ni ndefu.
 
G Sam Ndugu Yangu Ngoja nikwambie Kitu

Sio Shingongo Pekee Aliye dhulumiwa Na ccm Wapo Wengi Sana

Ila waliothubutu Ni wachache Na kusema waziwazi

Kuna siku niliweka wazi Sakata la Madawa ya kulevya na Nshu Ya manji Ila Mod waliutoa Uzi Ule haraka sana

Manji Ni Mmoja wa watu waliojitolea Pesa Kipind cha Kampen

Ila baada ya kilanja kupewa Madaraka Akawakana Hawa Watu

Haya ndio matokeo yake kuona Kira siku kuna vitu vinaibuka

Na Bado Vingi Sana vitaibuka

Natamani kusema mengi sema Mod wanaweza Nipiga Bun au Kufata nyuz
 
Katika situation ka ile, mtu anaweza kutunga sentesi yoyote ili kupata sympath wananchi na kuhalalisha kuondoka kwake ka wewe ulivyoingia king.

kwa iyo usiamini kila kauli.
Mfano leo angesema "RC aliniita ofisini kwake, akaanza kunitongoza na kunishika shika, nikapata mwanya nikakimbia nje, akahaidi kunifanyizia" je kuna ambaye angebisha?
 
S
"Nendeni mkamdai Kikwete"
Hii ni kauli ambayo msanii Wema Sepetu ameitoa na kwa kweli imeusononesha sana moyo wangu. Sii kauli ya kiungwana kujibiwa watu wale waliomsaidia Rais Magufuli kuingia ikulu. Ole kwa yule aliyetoa majibu hayo!

Nadhani kauli hii itaweza kuusononesha sana moyo wa rais mstaafu ndugu Jakaya Kikwete ambaye alifanya kila liwezekanalo "liwe la kifedhuli au la haki" kuhakikisha Magufuli anashinda hasa kutokana na ule ushindani mkali uliokuwepo.

Ni kauli inayoendeleza udhihirisho wa kiburi na ulevi wa madaraka vilivyoujaa utawala huu wa awamu ya tano! Si kauli nzuri hata kidogo.

Majibu ya hovyo yanayotolewa na baadhi ya watendaji kwenye huu utawala kama haya yanadhihirisha kuwa watanzania bado tunajithibitishia wenyewe jinsi tulivyopotea njia.

Aidha kusukumiwa mzigo huu wa wadai wa CCM kwa Kikwete kunaendelea kudhihirisha utu wake na uungwana ambao mimi ni miongoni mwa wadau tunaolia machozi makuu kuukosa na kujikuta tukitumbukia tusikokujua. Kwa haya siamini kama mdai mwingine Shigongo yu salama na ahadi aliyopewa hivi karibuni.

Bila kuathiri mada yoyote ningeomba sana mods wauache ujumbe huu ujadiliwe na wadau.
Sijaelewa alikuwa kada au mfanyabiashara?
 
Back
Top Bottom