Hofu ya Kikwete na visasi na matamanio ya uongozi 2015

Aug 1, 2012
35
27
HOFU YA KIKWETE NA VISASI NA MATAMANIO YA UONGOZI 2015.
Kauli ya Kikwete katika maadhimisho ya miaka hamsini na mbili ya uhuru wa Tanganyika jijini dare s salaam tarehe 9 disemba 2013, akiwataka watu wanaotaka nafasi za uongozi nchini kuiga mfano wa mwasisi wa taifa la afrika kusini hayati Nelson Mandela , akitolea mfano wa kiongozi huyo wa afrika kusini mzee Nelson Mandela kwa kitendo chake cha kutolipiza kisasi kwa makaburu waliowatesa wananchi wa afrika kusini na kumfunga kwa takribani miaka 27 jela lakini baada ya kutoka jela na kupata nafasi ya kuliongoza taifa la afrika kusini bado aliamini kuishi kwa kutombagua mtu yeyote Yule alitenda vitendo viovu kwa wananchi wan chi yake na kwake pia.

Mfano wa Mandela ni mzuri sana kuigwa na viongozi wa kiafrika lakini sio kigezo cha watawala kuhubiri kutolipizwa visasi pindi wanapofanya vitendo viovu kwa jamii zao au wahasimu wao katika harakati ziwe za kutafuta madaraka na vinginevyo,naweza kuwa tofauti kidogo na mitazamo iliyotolewa na wanataaluma mbalimbali juu ya kauli hii lakini napenda kuweka wazi hapa kwa nini tunakuwa waoga wa kulipiziwa visasi? Kwani kisasi ni nini? Kisasi sio kile kitendo kinacholipwa kulingana na vitendo vyako? Bado nikawa sielewi nini tatizo lililopo katika neno kisasi,Kwa nini tusitegemee kulipiziwa mema na ni nani hapendi kulipwa mema?

Maneno mengi ya kutufundisha juu ya utumishi wa kiongozi huyu hayati wa taifa la afrika kusini"Mzee Mandela hana wa kumlinganisha naye, ni kiongozi wa aina yake ametufundisha mengi katika uongozi wake, lakini kubwa zaidi ni kusamehe hata kwa mtu aliyekosea, wengi wetu tuliopo hapa tunajiandaa kulipa kisasi pindi tutakaposhika nafasi za juu za uongozi" mtazamo wangu waweza kubadilika kama tafsiri yangu ipo sahihi, leo hii tunashuhudia nafasi alionayo Jacob Zumma kwa sasa katika taifa lililoasisiwa na kiongozi anaejipatia sifa kuwa duniani kwa kuwa mwema hata kwa maadui zake, tumeona miguno katika jumuiko kubwa la kusherekea utumishi wa Mandela na kumuaga katika safari yake ya kwenda katika pumziko la milele, je pamoja na miguno hiyo ya kuashiria kutokubali utawala huo ni wapi Zumma alilipiza kisasi kwa Mandela, au ni wapi tumeona Mandela katika uatawala wake akitahadharisha wanaotafuta uongozi kuja kulipiza visasi? Kwa historia iliyopo nchini afrika kusini Hata Rais aliemfuatia Mandela Mzee Mbeki hakuwa na kisasi cha kulipiza kwa Mandela zaidi ya kutenda mema na kumuona ni kiongozi ambae alihitaji kuthaminiwa na serikali yake mpaka kufa kwake.

Bado narejea kauli ya Kikwete na hofu yake juu ya visasi"Nawasihi tuache kuwazia mambo ya visasi, wengi tulioko hapa tunamawazo ya nikipata watanikoma, kwa mzee huyu ni tofauti, alipopata madaraka aliwashirikisha makaburu hao hao waliomtesa akiwa na lengo moja tu la kuleta umoja na maendeleo ya nchi,"alisema Rais Kikwete.

Sina haja ya kutofautiana na Rais Kikwete juu ya visasi vyenye hila, ila kwa nini tunayo hiyo hofu ya kulipiziwa visasi? Kwa nini hatuamini tutatendewa mema kama malipo ya mema tuliyotenda katika kipindi chetu? Hofu hii inatoka wapi? Kwani tukitenda mema kisasi kitatoka wapi? Mandela katika uongozi wake alitenda mema na ndio mana hakuwa na hofu ya kulipiziwa visasi kwa hazina ya mema aliyoyatenda kwa wananchi wake.

Ipo mitazamo tofauti juu ya kauli hii ya Rais Kikwete, aidha kuangalia mienendo yake katika uongozi wake na dhamira yake ya kuwataka viongozi wajao kutolipiza visasi, lakini mbali zaidi kuhoji juu ya uadilifu wake katika hayo anayozungumza hususani wakati wa uchaguzi wa urais mwaka 2005, wapo waliokwenda mbali zaidi na kuhoji juu ya yale aliyotendewa Mzee Salimu ikitafsiriwa kama ni visasi vilivyofanywa na Rais Kikwete.

Siwezi tolea ufafanuzi wa hayo lakini msingi wangu hapo ni kujitazama kwanza na kufanya tathmini binafsi, haimaanishi kuficha mafunzo tunayoona hatukuyatenda ila ni kuweka wazi juu ya mienendo yetu ndipo tukatoa wito kwa wengine kwa kuona kwanza nini sisi tumekikosa na nini huenda ikawa ni kikwazo katika kufanikisha majukumu yetu kwa umma kutokana na hicho tunachokitoa kama funzo kwa wengine.

Ni imani yangu kuwa Rais Kikwete aliona mapungufu yake katika swala la visasi kwanza, lakini hakuweza kuwa muwazi kwa nafasi yake kuwaambia watanzania kuwa ni muumini wa visasi hivyo, na kuona ni muhimu kwa sasa kuzungumzia swala hilo kwa kuwa anatambua madhara yake endapo tutaishi kutafuta uongozi wa kulipiza visasi, Binafsi siamini katika visasi na ni imani yengu hatuhitaji kufundishana kutokufanya vitu mana hatuwezi kuwa na mazoezi ya kutokufanya, tunahitaji kufundishana kufanya vile tunavyoweza kuvifanyia mazoezi, matokeo ya visasi ni vitendo viovu lakini matokeo ya kutolipizwa kisasi ni kutenda mema daima, Nafikiri kama sisi ni wema tufundishane ni kwa nini hayati Mandela hadi kufa kwake hakuna aliefikiri kumlipizia kisasi? Ni kwa nini leo Kikwete anatahadharisha viongozi wajao juu ya visasi? Majibu ni mepesi sana kuna WEMA uliofanywa na Hayati Mandela ndio mana hakuna VISASI ila kuna MEMA, lakini kuna UOVU ambapo matokeo yake ni VISASI hivyo sina kwa wenye utashi inafahamika nyuma ya pazia la onyo kwa viongozi wajao kwa sasa kuna UOVU unaojengewa hoja ya utetezi mbeleni.

Kati ya hazina kubwa za fikra ambazo Watanzania wanayo katika ujenzi wa taifa lao ni fikra za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo ni pamoja na kuelewa nadharia na falsafa zake kuhusu maendeleo, uongozi, na suala zima la ujenzi wa taifa jipya. Kwa kiasi fulani (wengine wanaweza kusema kiasi kikubwa) kipo kizazi cha Watanzania ambacho kinajaribu kufuta, kudharau, na hata kusahau hazina hii ya fikra, binafsi ni muumini wa fikra hizi nab ado naamini tunayo mengi ya kujifunza kutoka katika maandiko yake yenye fikra.

Bado naamini maadili haya tuliyoachiwa na mwalimu hayatuelekezi huku tunakokwenda sasa tunahitaji kujenga taifa lenye umoja na mshikamano, haya yanakuja kwa kuwa na agenda yenye kutuweka katika kapu moja, MwalimuNyerere alipokuwa kiandika kitabu cha UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA Lijaribu kuangalia mambo muhimu kwa taifa na kukosoab moja ya mambo ambayo yaliekea kulimega taifa, Naomba pia kutahadharisha juu ya hofu ya kikwete, kwa kuwa mimi si muumini wa visasi na siamini katika hilo, nitoe wito kwa watawala kutotengeneza mazingira ya visasi na kufanya kuwa ndio msukumo wa wale wanaotafuta kuliongoza taifa hili, watawala wanayo nafasi ya kurekebisha hilo na kuweka mazingia ya kutafakari changamoto za nchi ndio iwe agenga ya kutafuta uongozi na sio visasi.

Emmanuel Masonga,
masongae@gmail.com
+255 753 170 161.
 
Kikwete anajua watu safi wakiingia ikulu lazima watamsafisha kwa mambo yaliyoicost nchi hii anajua watamkausha.... sasa ndio anaanza kuweweseka... mbona kashindwa kumsamehe Babu seya...
 
Na ule ugaidi uliofanyika kule Arusha je? Nao tuufumbie macho? Huyu gaidi ahurumiwe?

1013165_548810871844995_387610025_n.jpg
 
jamaa ana kisasi ndio maana ana kiua chama chake ili Lowasa asiingie ikulu akalipa kisasi, coz alimtosa kwenye kashfa ya richmond ,
 
Kisasi hakitakiwi lakini utawala wa sheria lazima uchukue mkondo wake.

Hata Mandela hakuwaacha watu hivi hivi walilazimishwa kuja mbele ya tume ya ukweli na maridhiano kukiri makosa yao! Waliwajibishwa! Unadhani yule "bwana jela" alifurahia kuletwa mbele za watu kushuhudia mfungwa wake akiapishwa kuwa raisi? Aliwajibishwa vya kutosha siku ile...(unaweza kusema natania).

Hakuna aliyeko juu ya sheria! Alafu si utu kutenda mambo yasiyostahili kwa kisingizio cha kubebwa na mfumo. Eti uwaibie wananchi ukifuatiliwa basi mtu uone ni kisasi?!

Kama ambavyo utaratibu wa kisheria upo kwa wananchi wa kawaida; viongozi nao wafuatiliwe; wawajibishe kwa makosa yao. Kumfuata Mandela ni kuweka mfumo wa kuwajibishana bila kuangalia sura ya mtu wala ukwasi wake!

Muktadha wa Mandela wala hauna uhusiano mkubwa sana hapa! Mandela alijua nchi yake itayumba bila wale jamaa! Ila ukweli ni kuwa makaburu waliwaona waafrika kama sio watu. Waliwadhuru kimwili, kiakili na kiroho! Walivuka mipaka! Waafrika walichukia; makaburu walijawa chuki vile vile! Sasa hawa unawafanyeje zaidi ya kuwafundisha na kuwabadilisha tabia?! Akafanya maamuzi magumu kwa maslahi mapana ya taifa lake ili nchi isonge mbele na sasa wako mbali! Hakufanya kwa maslahi yake binafsi ingekuwa hivyo hata Winnie angesamehewa vile vile! Taifa kwanza!

Labda tuambiwe kuwa nchini mwetu pia kuna chuki baina ya watawala na watawaliwa. Tuwekwe wazi kwamba watawala wanatuchukia kiasi cha kututenda wanavyotutenda!

Tukumbuke kuwa wale makaburu hawakuwahi kuwekwa madarakani kwa misingi yoyote ya demokrasia na haki! Hawakuwahi kujinadi mbele za watu kuwa watatenda hiki watatenda kile! Hawakuwahi kuahidi mbingu!

Mtawala aliyejipitisha kwa wananchi akiwa na maneno matamu ya kurubuni watu ili achaguliwe lakini aliposhika madaraka akawa anatenda kinyume NI SAWA NA MLIPA VISASI kwa wananchi wake!
Kwanini tunawadanganya watu? Alicho fanya Mandela kwa taifa lake kisi-justify yale maovu tunayowatendea wananchi waliotuamini na kutuweka kwenye 'utakatifu' tulionao!

Mwisho kabla ya kutamani MSAMAHA wa Mandela tufuate MAFUNDISHO ya Mwalimu!
 
Back
Top Bottom