AHAh, ivi kwenye ule uzi ulikuja tena?
SIo ndio kama hvyo anataka aunt asiongee na kajala kisa wamegombana nae, wewe unatafsiri nn kama sio kutawala wenzie? Naona umepanick binamu utajibebaa
Ni kweli best, hata sasa nataka nitoke kidogo humu.
Asante sana.
Marafiki wa wema wote ni waswahili hata hafanani nao, sio class yake, ndio maana hawadumu.
Marafiki wa vigodoro nao ni marafiki? Group ya Wema ni kina Irene Kiwia, Faraja Kota, K-lynn and the like. Sio hizi takataka! Sijui hata analalamika nini? Aachane na hawa waswahili atafute marafiki wa class yake aone kama hawatadumu.
Nimekuja binamu warumi, kumbe hujaona ma-like ya kumwaga niliyokupa eeh, nimeona imefikia mahali mkawa mnaenda sawa na daktari wetu! ila natafuta muda mzuri nitulie nisome kuanzia nilipoishia, ule uzi inatakiwa usiwe na haraka kama unataka kutoka na kitu cha maana
Beautiful Onyinye wa Bongo , Wema Sepetu amefunguka kuwa , anajua siku zote yeye hana bahati ya kuwa na marafiki kwa kuwa hata akiwa nao mwishowe kunatokea mgogoro na kuachana huku kila mmoja akimuona mbaya.
Wema alisema anaumia sana kwa kuwa mara nyingi anawapenda sana rafiki zake kwa moyo mmoja lakini mwisho wa urafiki wao huwa ni mbaya sana tena huvunjika kwa kugombana.
Mimi nimeshajiona siku nyingi sina bahati kabisa, hata nikiwa na marafiki ambao nawapenda kutoka moyoni , mara nyingi wananigeuka na mama yangu amekuwa akinisihi mara nyingi sana , sasa naona bora nifuate ushauri ambao mama yangu ananishauri wa kuangalia watu wa kuanzisha urafiki nao , alisema Wema.
Chanzo: GPL
Kwa nn jaman, lol vibaya hvyo
Sijapanic nashangaa mtu mzima anatawaliwaje..
Mfano aunty kutwa anashinda kwa wema.... yaani ale msosi wa wema anye chooni kwa wema halafu akishiba akapuyange kwa kajala???
Mmmmmmh
Kweli kabisa.Tena marafiki wenyewe wanaishia kumharibu tu hata hawazii future yake.
Kiukweli hata mimi marafiki waswahili sina na siwataki kabisaaa...naepuka mambo mengi tu.
KWani kuna shida gani? KWani wao wana ugomvi? Huo ni ukoloni walahi wala si sawa
Bora aachane na marafiki angekua anasikiliza ushauri wa mamake asingefika hapo. Rafiki mzuri ni yule akufaaye kwa hali zote nzuri au mbaya ila hawa bongo movie hamna rafiki wa kweli.
Mjomba ukiishi kwa mtu kuna rules za kufuata.....kiufupi unauza sehemu ya uhuru wako (chezea kwenda chooni wewe)
Ila aunty angekuwa anaishi kwake.....
Ushosti na wema ni wa kukutana kutia story then kila mtu na kwake yasingemkuta.....angepangiwa masharti saa ngapi????
Kwa lugha nyingine siku nyingine waache kujisogeza kwa mtu (mtu mzima huofii kubakwa kwa uhuru wako??) Ingewaepusha na mengi ukizingatia ushosti wenyewe wa kumjini mjini huu
Nimejikuta namuonea huruma kiukweli.Lakini tatizo la Wema anapenda urafiki na mastar/malaya wenzie ambao mwisho wa siku huishia kugombana.
Kwanini asiwe na rafiki wa kawaida tu asiyependa mambo ya mjini? Tena awe mdada mwenye shughuli zake za kimaendeleo hakika angembadilisha sana.
AHaha mwenzangu, ni shidaaa, binamu kuna kitu kinakutatiza, naona haupo sawa kabisa
Tatizo aina ya marafiki, marafiki sio wote wabaya, mbona Nancy na akina k-lyn, nasreem ni marafik wa mda mrefu ila hawana ma beef ya kipuuz kama mama ubaya? YEye tu kachagua maisha ya kiji kijinga
NImekuelewa, wema anawasaidia sana rafiki zake to the point mpaka inakuwa kwamba anachotak yeye basi marafik zake wafuate coz anawasaidia vitu vingi, ki binadamu ni sawa ila aangalie marafik wa kuwa nao, marafik wa kufuatana matakon kutwa mpaka mnajambiana lazima mpeane mashart ya kipuuzi, mbona akina jide, nancy, jokate hawana ushoga wa kipuuzi na watu wa ajabu, kutwa wema na rafik zake wa tandale
Kweli japo wema ana mapungufu yake lakini huwa anawapenda marafiki zake sana.
Na ana roho nzuri huyu dada.Tusimvue utu wake kisa tu hataki rafiki yake awe na urafiki na adui yake.
Kiukweli hata mimi sitofurahi kumuona rafiki yangu ninayempenda na kila kitu namueleza halafu nimuone na adui yangu.Bora iwe salamu tu lakini ushoga wa kihiiivyo wewe utafurahi kweli Diva Beyonce?