Wema Sepetu: Sina bahati na marafiki

Wema Sepetu: Sina bahati na marafiki

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,213
Reaction score
18,466
Beautiful Onyinye wa Bongo , Wema Sepetu amefunguka kuwa , anajua siku zote yeye hana bahati ya kuwa na marafiki kwa kuwa hata akiwa nao mwishowe kunatokea mgogoro na kuachana huku kila mmoja akimuona mbaya.

Wema alisema anaumia sana kwa kuwa mara nyingi anawapenda sana rafiki zake kwa moyo mmoja lakini mwisho wa urafiki wao huwa ni mbaya sana tena huvunjika kwa kugombana.

"Mimi nimeshajiona siku nyingi sina bahati kabisa, hata nikiwa na marafiki ambao nawapenda kutoka moyoni , mara nyingi wananigeuka na mama yangu amekuwa akinisihi mara nyingi sana , sasa naona bora nifuate ushauri ambao mama yangu ananishauri wa kuangalia watu wa kuanzisha urafiki nao , " alisema Wema.

Chanzo: GPL
 
Attachments

  • 1431680339273.jpg
    1431680339273.jpg
    56.5 KB · Views: 4,083
Bora rafiki kuliko mwanasesere...
 
Dog is a good friend.

Ni kweli hata akikuona umehuzunika hukurukia rukia hukuchangamkia, akiona hauelekea hukunja mkia wake na ujilaza chini kusikilizia unanini leo, akiona unauziwa, wakwanza kupambana na anayekudhuru, lakini njoo kwa paka akikosa maziwa tu, anajiweka pembeni au anahamia baa kunakopatikana mabaki ya samaki.
 
Nimejikuta namuonea huruma kiukweli.Lakini tatizo la Wema anapenda urafiki na mastar/malaya wenzie ambao mwisho wa siku huishia kugombana.
Kwanini asiwe na rafiki wa kawaida tu asiyependa mambo ya mjini? Tena awe mdada mwenye shughuli zake za kimaendeleo hakika angembadilisha sana.
 
Shida nyingine aliyonayo wema anataka adui yake, pia awe adui yako!! hapo ndo wengi wanaposhindwa kuendana naye. Ila generally ukiondoa tabia yake ya umalaya nadhani wema ana huruma fulani hivi na upendo wa dhati kwa marafiki zake, sema ndo hivyo tena hilo la adui yake adui yako linawashinda wengi
 
Pole wema ila aunt alichofanya sio poa kaona kumkomoa ni bora amuumize kupitia kajala
 
Nimejikuta namuonea huruma kiukweli.Lakini tatizo la Wema anapenda urafiki na mastar/malaya wenzie ambao mwisho wa siku huishia kugombana.
Kwanini asiwe na rafiki wa kawaida tu asiyependa mambo ya mjini? Tena awe mdada mwenye shughuli zake za kimaendeleo hakika angembadilisha sana.

Tatizo anapenda kuwatawala marafiki zake, yani moyo wake utakavyotaka ndio anatak na marafik zake wawe hivyo hivyo
 
Kwema tu best, pole na majukumu coz kuna mahali umeandika leo umebanwa kidogo na majukumu

Ni kweli best, hata sasa nataka nitoke kidogo humu.
Asante sana.
 
Marafiki wa wema wote ni waswahili hata hafanani nao, sio class yake, ndio maana hawadumu.
Marafiki wa vigodoro nao ni marafiki? Group ya Wema ni kina Irene Kiwia, Faraja Kota, K-lynn and the like. Sio hizi takataka! Sijui hata analalamika nini? Aachane na hawa waswahili atafute marafiki wa class yake aone kama hawatadumu.
 
Back
Top Bottom