barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Katika Mahojiano yake na Waandishi wa Kampuni ya New Habari(2006) Ltd,Wema Sepetu anaanza kwa kusema
"Nilipokuwa na uhusiano na Marehemu Kanumba,nikiwa naishi na wazazi wangu,niliwaza kama wakijuwa nina Mimba wangejisikiaje?Na pia sikuwa tayari kwa kipindi hicho kuwa na mimba,na utoto pia ulichangia,nikatoa"
"Wanaume wote waliofuata hapo akiwemo Chalz Baba,Jumbe na Diamond sikuweza kupata huo ujauzito wala aina yoyote ya kichefuchefu,Lakini nilipoachana na Diamond alipokuwa na mwanamke mwingine nikasikia amepata ujauzito,kiukweli niliumia sana,nikafikiria kwamba mimi ndiye nina tatizo au ile mimba niliyotoa wakati wa Kanumba ilikuwa ndio pekee niliyojaliwa na Mungu,baada ya hapo nikaanza kumsumbua Daktari wangu,daktari alinipa dawa mbalimbali na kuweka sawa viamsho mwilini,lakini dawa hizo zikaishia kuninenepesha tu"
Wema Sepetu anaendelea kusema
"Wakati nikiwa na Idriss,nikashangaa baadhi ya watu wakaniambia nina mimba,lakini sikuamini nikaenda kupima nikiwa na lengo la kusafisha kizazi lakini daktari akaniambia vipimo vinaonyesha kweli nina ujauzito.Nilifikia uamuzi wa kusafisha kizazi sababu nilichoka kuitwa mgumba"
"Baada ya kukugundulika ujauzito huo nikapiga picha na kuzituma kwenye mitandao nikionyesha tumbo langu,ili kuwaonyesha watu kuwa si mgumba ambapo wengine walishika tumbo langu wakifurahia,hii ikanifanya kuwa na furaha na mpenzi wangu Idriss"
"Siku moja nilipoamka nilikwenda asubuhi kwa haja ndogo,cha ajabu nikahisi kama kitu kimeshuka na nilipoangalia nikaona damu.Hapo hapo nikampigia Mama na kumwambia mimba imetoka,alilonijibu ni kwamba alinambia mimba haitangazwi.Maneno hayo alishaniambiaga kwamba nisitangaze mimba niliyokuwa nayo lakini sikumsikiliza kwa kuwa nilitaka kuwaziba midomo watu waliokuwa wakinitupia maneno ya matusi."
"Niliumia sana ilipotoka ile mimba,kwani ni kitu nilichokuwa nakitaka kwa muda mrefu,nimechoka kuitwa mgumba,lakini sijakata tamaa najua ipo siku nitapata tena"