Unajua kadiri unavopanda ngazi kwenda juu ndivyo unavyojulikana zaidi na ndivyo mema yako na mabaya yako yanavyofahamika zaidi. Yaani hili huwezi kulikwepa. Unakuwa public figure. Na kwa jinsi hiyo huwezi kukwepa maoni na mitazamo ya watu inayotolewa juu yako: mitazamo mizuri na mibaya. Cha maana ni kujijua, kubaki mwenyewe (what you are), na pale unapoona yafaa kurekebisha unarekebisha.
Yanayompata Wema ni jambo la kawaida katika maisha. yeye ni miss Tz 2006, ni public figure. Huwezi kuzuia watu kumjadili: kwa karama zake njema, na hata kwa mapungufu yake. Kwa yale ambayo ni negative ni juu yake kukaa na kutafakari "je ni kweli"? Kama ni kweli ayafanyie kazi. Ana bahati sana kuzungumzwa hivi wazi maana itamsaidia kujirudi kwa kufahamu udhaifu wake kama alikuwa haufahamu.
Kama yanayosemwa si kweli au yameongezwa chumvi, basi ni juu yake kuchambua mchele na pumba. Mchele aufanyie kazi, pumba aachane nayo. It is so simple. Hana sababu ya kukata tamaa kwa maneno ya watu. Na siamini kama kuna mtu mwenye nia mbaya ya kutaka kumchafua. Ila watu wanakuwa na wasiwasi naye kutokana na yale wanayoyafahamu. Kumbe hayo yawe kichocheo kwake kujiweka sawa zaidi. Tunahitaji balozi huko BBA si mchezo. Kufanya mambo ya ajabu kunaweza kuwa aibu si kwake tu bali kwa taifa zima.