Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Staa wa filamu na mrembo maarufu Tanzania, Wema Sepetu, ameibua mjadala mkubwa baada ya kuandika ujumbe mzito kwenye akaunti yake ya Snapchat ambao umeonekana kama kutangaza rasmi kwamba kwa sasa anaendelea na maisha kama single mother.
Kupitia Snapchat yake, Wema ameandika:
“Being a single mother was never a part of my plan, but being the BEST mother always was.”
Kwa tafsiri ya Kiswahili:
“Kuwa mama ninayelea mtoto peke yangu haikuwa sehemu ya mipango yangu, lakini kuwa mama BORA siku zote imekuwa ndoto na kipaumbele changu.”
Kauli hiyo imewafanya mashabiki wengi kuamini kwamba Wema kwa sasa ameamua kuweka nguvu zake zaidi katika malezi na kumlea mtoto wake, huku akisisitiza kuwa jambo la muhimu kwake ni kuhakikisha anakuwa mama bora.
Hata hivyo, mashabiki wameendelea kujiuliza kama ujumbe huo unamaanisha kwamba mambo yake ya kimapenzi na Whozu hayapo tena katika hali nzuri, hasa baada ya tetesi mbalimbali kuendelea kusambaa kuhusu wawili hao.