Pilipilihoho
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 202
- 145
Wema Sepetu ni bingwa wa kutumia gharama kubwa kufanya filamu na kutengeneza kiu kubwa kwa mashabiki wake halafu then mradi unageuka kuwa kama album ya Detox ya Dr Dre, ambayo haijawahi kutoka hadi leo.
June 2012: Muigizaji wa Nigeria, Omotola Jalade akiwa na Wema baada ya kuwasili kutoka Nigeria kuhudhuria uzinduzi wa filamu ya Superstar ambayo hadi leo haijatoka
Miaka minne iliyopita, Wema alidai kutumia mamilioni ya shilingi kufanya filamu aliyoipa jina ‘Superstar.’ Na hata uzinduzi wake uliofanyika Hyatt Regency Hotel (Kilimanjaro) ulikuwa wa kifahari na wa aina yake. Mastaa karibu wote wa Tanzania walialikwa na kuona sehemu ya filamu hiyo.
Alitisha zaidi kwa kumleta msanii nguli wa Nigeria, Omotola Jalade aliyeshuhudia uzinduzi huo. Bahati mbaya hadi leo filamu hiyo haijawahi kutoka sokoni na mrembo huyo aliamua kuifungia kabatini.
Tupeleke mbele. Mwaka jana Wema alienda Ghana na kufanya filamu na staa wa huko, Van Vicker iitwayo ‘Day After Death’. Filamu hiyo ilifanyika December 2014. Kwa mujibu wa ratiba ya mwisho, ilikuwa itoke September mwaka jana.
Meneja wake, Martin Kadinda, alidai ilishindikana kutoka kwasababu ya kampeni za uchaguzi.
“Filamu mpaka sasa ipo tayari, lakini movie hii hatuwezi kuiachia kama anavyoachia movie nyingine.Lazima afanye launch na ilikuwa launch ifanyike toka mwezi wa tisa lakini toka mwezi wa sita mpaka sasa Wema yupo kwenye kampeni,” Kadinda aliiambia Bongo5.
“Kwahiyo tunasubiri mpaka hizo kampeni ziishe na uchaguzi upite Wema atakuwa anazindua products zake mpya halafu baada ya hizo products kuzinduliwa ndio filamu itazinduliwa rasmi,” aliongeza.
Lakini hadi sasa hakuna dalili za filamu hiyo kutokana na haiongelewi tena? Kunani? Tuna wasiwasi kuwa filamu hii inaweza kuungana kabatini na Superstar zikipeana moyo.
Bongo 5