Weledi na ufahamu wa siasa katika CCM ya sasa ni bidhaa adimu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Weledi na ufahamu wa siasa katika CCM ya sasa ni bidhaa adimu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mghaka, Sep 26, 2011.

 1. M

  Mghaka JF-Expert Member

  #1
  Sep 26, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 320
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa ufahamu na ujinga si marafiki kama ilivyo kwa shetani na utukufu itawachukua miaka mingine 50 kwa CCM kurudia alama yake ya awali ya kujitambulisha kwa utu, hoja, ukweli na ufahamu uliokithiri. Vijana wote welevu wamekata kwenda kuwashujudia mafisadi na wameamua kuka upande ambao unatafuta haki kwa kujenga hoja na kukemea maovu. Kwa hali ilivyo sasa na mbele ya macho ya watu wengi ni kwamba CCM ilikubali kupeana mkono na shetani na alichowapa ni ubnafsi, uchoyo, uwongo, udhalimu na kila aina ya dhambi, yeye akachukua busara na weledi.

  Ukifanya biashara na shetani yeye ndiye hunufaika siku zote shetani hajui kupoteza. Ukimshangaa kwa kukosa busara yeye anakushangaa kwa kukubali kushirikiana nae na kupata mapokeo yake. Kilichobaki kwa CCM sasa ni kupokea makapi kutoka upinzani na kuimba vigelegele, wote tumeona kila kukicha CCM hutuma timu yake kutafuta wachezaji kutoka upinzani na kuambulia kupata wale ambao ni nusu welevu halafu kinapiga talalila kwa kuchukua makapi.

  Watu wote wenye ufahamu wa kutosha hawawezi kuwa` sehemu ya CCM na wanaiogopa kama watakatifu wanavyoogopa hata kivuli cha shetani karibu yao. CCM safisheni nyumba hiyo ili malaika wa bwana waingie kuwaongoza na kuwajaza ufahamu na busara. Hivi umewahi kuona siasa za wapi vyama vya siasa vinasajiri kutoka vyama vya siasa vingine kwa kutumia ushawishi wa fedha na si itikadi? hapo ndio nawachoka ccm
   
 2. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  ccm ni historia, si chama tena chenye mvuto
   
 3. M

  Makupa JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Chama chenye mvuto ni kipi
   
 4. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  "hapo zamani za kale, palikuwepo na chama kimoja kilichokuwa mstari wa mnbele kutetea watu wa nchi hiyo na hata nje ya nchi, na kilikuwa na itikadi zake ambazo kila mwana chama alizijua. ......................" leo hii wabunge kama majimarefu, mansoor, jah peoplpe, Lameck Airo and the like hawajui itikadi ya chama chao nsembuse wanachama? hii imekuwa historia kinaenda kuzikwa tu
   
 5. F

  Froida JF-Expert Member

  #5
  Sep 27, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Nadhani wakati wa maamuzi magumu ulishafika kila mtu anafahamu jinsi CCM walivyojaza magereza ndani ya mioyo yao wamefunga na uroho,uzandiki,unafiki,uongo,dharau,dhuluma,wizi,unyonyaji,ujambazi,uuaji,uzinzi,watu wa hovyo na chama chao cha hovyo,wana ajenda ya kuipeleka nchi kwenye vita ili wao na vibaraka wao waje waweze kuiba mali zetu na kupola mali zetu
   
Loading...